Jeshi la Polisi Lafanikiwa Kukusanya Bilioni 29.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam Lazaro Mambosasa amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja Jeshi hilo limefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 29, zilizotokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ambayo watuhumiwa wake walikiri kufanya.View attachment 982306

Mambosasa ameyasema hayo leo Desemba 31, 2018, Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa jeshi hilo na mafanikio yake katika kipindi cha mwaka mmoja.

"Kipindi cha mwaka mmoja fedha tulizofanikiwa kukusanya ni bilioni 29, kwa watuhumiwa wa makosa ya kukamatwa kwa vyombo vya usafiri na wenyewe wakakiri kufanya makosa hayo".

Aidha Kamanda Mambosasa ameogeza, "naomba wadau tushirikiane kwa pamoja kuhusu wahamiaji haramu, kwa hapa DSM kuna wimbi kubwa la matapeli ambao ni raia wa kigeni na wanafanya uhalifu, hili eneo si la kufumbiwa macho, unakuta mstaafu katoka kuchukua kiinua mgongo, anatapeliwa".

"Wanachi wanaumizwa kweli mmoja hapo chini kuna mstaafu ametapeliwa milioni 120, na mnigeria ambaye ameingia nchini na anaishi bila kibali."

Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amewaonya wananchi watakaosherehekea mkesha wa mwaka mpya kwa kufyatua mafataki badala yake ametoa dakika 5 kwa watakaotaka kufanya tukio hilo kuanzia saa 6 kamili usiku hadi saa 6.05 usiku.
Jukumu la polisi si kukusanya mapato. Ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Kutangaziwa makusanyo ni aibu kwa jeshi. Taarifa ya takwimu za kushuka kwa makosa ya uharifu lingekuwa jambo la msingi.
 
Nimekuelewa

Sent from my SM using Tapatalk

Mbaya zaidi ni kuwa kwingine ukifuata kinachotakiwa utaepuka faini na adhabu. Kwetu hata ufanyeje utatozwa tu faini. Kwetu hakuna rules za game. Kwetu ni rules of the jungle.

Kwetu wakusanya faini wanaweza amka na lengo la 30,000/= kwa kila gari isiyokuwa ya serikali.

Wanaokumbwa na adha hii kila leo hawanayo neno zuri kwenu, na laiti mngezijua dua wakuu kwenu wangeacha haka ka usanii ka kuomba kuombewa.
 
Wao wamekusanya bilioni 29 kwa mwaka mmoja wakati Maywether kamtwanga mjinga mmoja tu muda si mrefu kajipatia billion 20.6:hii dunia hatuko sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapogeuza makosa kuwa SOURCE OF INCOME, ndo tunapata guts za kutangaza mapato yatokanayo na makosa....
 
Jukumu la polisi si kukusanya mapato. Ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Kutangaziwa makusanyo ni aibu kwa jeshi. Taarifa ya takwimu za kushuka kwa makosa ya uharifu lingekuwa jambo la msingi.

Ni kama hospital nazo zianze kujivunia mauzo ya dawa badala ya kuokoa uhai wa raia, JW nao wajivunie idadi ya mifugo waliyoteka mpakani, walimu wajivunie ada walizokusanya nk
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam Lazaro Mambosasa amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja Jeshi hilo limefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 29, zilizotokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ambayo watuhumiwa wake walikiri kufanya.View attachment 982306

Mambosasa ameyasema hayo leo Desemba 31, 2018, Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa jeshi hilo na mafanikio yake katika kipindi cha mwaka mmoja.

"Kipindi cha mwaka mmoja fedha tulizofanikiwa kukusanya ni bilioni 29, kwa watuhumiwa wa makosa ya kukamatwa kwa vyombo vya usafiri na wenyewe wakakiri kufanya makosa hayo".

Aidha Kamanda Mambosasa ameogeza, "naomba wadau tushirikiane kwa pamoja kuhusu wahamiaji haramu, kwa hapa DSM kuna wimbi kubwa la matapeli ambao ni raia wa kigeni na wanafanya uhalifu, hili eneo si la kufumbiwa macho, unakuta mstaafu katoka kuchukua kiinua mgongo, anatapeliwa".

"Wanachi wanaumizwa kweli mmoja hapo chini kuna mstaafu ametapeliwa milioni 120, na mnigeria ambaye ameingia nchini na anaishi bila kibali."

Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amewaonya wananchi watakaosherehekea mkesha wa mwaka mpya kwa kufyatua mafataki badala yake ametoa dakika 5 kwa watakaotaka kufanya tukio hilo kuanzia saa 6 kamili usiku hadi saa 6.05 usiku.
Hyu sio kamanda badala aeleze ni kwa kiasi gani wamepunguza uhalifu na ajali barabarani yeye anakimbilia tumekusanya hela kiasi hiki kwa mwaka kama wao sasa ni mamlamka ya mapato hyu hii kazi ya upolisi haiwezi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa natokea kinondoni pale Salenda kwenye taa eti Police ananiambia nimevuka taa nyekundu tena bila aibu.

Taa ilikuwa kijani; ile navuka tu line taa ya njano ikawaka nikaendelea sababu siwezi kusimama ila inaniashiria nivuke maana nipo katikati.

Tulibishana sana na yule askari kwamba ni sheria gani inayosema nisimame kwenye taa ya njano? tena mbele ya mstari? maana taa ya njano imewaka nikiwa nishavuka mstari.

Jamaa likakomaa eti twende mahakamani; tulikuwa tunatoka safari ndefu watoto wamechoka sana nikaliambia liandike tu niwahi home watoto wakapumzike.

Hawa jamaa wanalazimisha makosa sababu wanajua huwezi kwenda mahakamani usumbufu.

Mungu anawaona.
 
Mbaya zaidi ni kuwa kwingine ukifuata kinachotakiwa utaepuka faini na adhabu. Kwetu hata ufanyeje utatozwa tu faini. Kwetu hakuna rules za game. Kwetu ni rules of the jungle.

Kwetu wakusanya faini wanaweza amka na lengo la 30,000/= kwa kila gari isiyokuwa ya serikali.

Wanaokumbwa na adha hii kila leo hawanayo neno zuri kwenu, na laiti mngezijua dua wakuu kwenu wangeacha haka ka yaani ka kuomba kuombewa.
Ni kweli ulisemalo
Mimi licence yangu haina point hata moja na sasa ni mwaka wa 15
Kila kwenye camera inakutahadharisha kabla na huwezi kusumamishwa hovyo.
Unapata faini kwa kosa ulilotenda na huonani na police kabisa bali ni camera ndio zinakuchapa.
Kama huna insurance au road tax wanaijua gari mara moja na utasimamishwa na faini juu

Kanuni huku ni tofauti na nyumbani
Huko unasimamishwa utafikiri mpo vitani kila saa wapo kuvuna tu hata kosa dogo
Poleni kwa kweli

Sent from my SM using Tapatalk
 
Back
Top Bottom