Jeshi la Polisi Lafanikiwa Kukusanya Bilioni 29.

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Posts
4,514
Reaction score
23,702
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam Lazaro Mambosasa amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja Jeshi hilo limefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 29, zilizotokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ambayo watuhumiwa wake walikiri kufanya.
mambosasa.jpg

Mambosasa ameyasema hayo leo Desemba 31, 2018, Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa jeshi hilo na mafanikio yake katika kipindi cha mwaka mmoja.

"Kipindi cha mwaka mmoja fedha tulizofanikiwa kukusanya ni bilioni 29, kwa watuhumiwa wa makosa ya kukamatwa kwa vyombo vya usafiri na wenyewe wakakiri kufanya makosa hayo".

Aidha Kamanda Mambosasa ameogeza, "naomba wadau tushirikiane kwa pamoja kuhusu wahamiaji haramu, kwa hapa DSM kuna wimbi kubwa la matapeli ambao ni raia wa kigeni na wanafanya uhalifu, hili eneo si la kufumbiwa macho, unakuta mstaafu katoka kuchukua kiinua mgongo, anatapeliwa".

"Wanachi wanaumizwa kweli mmoja hapo chini kuna mstaafu ametapeliwa milioni 120, na mnigeria ambaye ameingia nchini na anaishi bila kibali."

Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amewaonya wananchi watakaosherehekea mkesha wa mwaka mpya kwa kufyatua mafataki badala yake ametoa dakika 5 kwa watakaotaka kufanya tukio hilo kuanzia saa 6 kamili usiku hadi saa 6.05 usiku.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam Lazaro Mambosasa amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja Jeshi hilo limefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 29, zilizotokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ambayo watuhumiwa wake walikiri kufanya.View attachment 982306

Mambosasa ameyasema hayo leo Desemba 31, 2018, Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa jeshi hilo na mafanikio yake katika kipindi cha mwaka mmoja.

"Kipindi cha mwaka mmoja fedha tulizofanikiwa kukusanya ni bilioni 29, kwa watuhumiwa wa makosa ya kukamatwa kwa vyombo vya usafiri na wenyewe wakakiri kufanya makosa hayo".

Aidha Kamanda Mambosasa ameogeza, "naomba wadau tushirikiane kwa pamoja kuhusu wahamiaji haramu, kwa hapa DSM kuna wimbi kubwa la matapeli ambao ni raia wa kigeni na wanafanya uhalifu, hili eneo si la kufumbiwa macho, unakuta mstaafu katoka kuchukua kiinua mgongo, anatapeliwa".

"Wanachi wanaumizwa kweli mmoja hapo chini kuna mstaafu ametapeliwa milioni 120, na mnigeria ambaye ameingia nchini na anaishi bila kibali."

Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amewaonya wananchi watakaosherehekea mkesha wa mwaka mpya kwa kufyatua mafataki badala yake ametoa dakika 5 kwa watakaotaka kufanya tukio hilo kuanzia saa 6 kamili usiku hadi saa 6.05 usiku.

Naomba kuuliza, nikisimamishwa na askari wa usalama barabarani akaniambia nimeoverspeed kwenye eneo la 50, halafu nikamwambia hapana si kweli, naye akasimamia msimamo wake huo, nikiomba ushahidi anasema amepigiwa simu, then baadaye akaniambia omba msamaha nikusamehe inakuwa inaashiria nini?
 
Hili ni la kukemewa sio sifa kukusanya pesa hizo nyie sio TRA sasa ile kauli "utii bila shuruti" hauna maana hata ile polisi na jamii siyo maana ni mwendo wa kubambika na kuandika makosa ili kukusanya pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NI AIBU MMOJA WA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI KUJIVUNIA MAKUSANYO YANAYOTOKANA NA ET "MAKOSA".
INAONEKANA SASA NI RASMI HIYO NI SEHEMU YA MAKUSANYO.
Kwa kweli siku hizi makosa ya barabarani umekuwa ni mtaji kwa nchi nyingi duniani.

Sio tu nyumbani hata Ulaya wanaongoza kwa kukusanya na faini ni kubwa mno kiasi ambacho siku hizi kuna kosa la speed tu unapewa faini ya £1000 sawa na 3m ya tz

Yaani huku ni mwendo wa heshima barabarani kama umeolewa na police hahaha

Sent from my SM using Tapatalk
 
Hata hivyo nadhani anazungumzia Dar tu.
Yeye anahusika na dar tu, aliepaswa kuongea ni Kamanda Sirro.[emoji18] [emoji53] [emoji52]

Ila hio kauli aliosema WAMEKIRI MAKOSA. Sikubaliani nayo kabisa. Tumebambikizwa makosa kibao hasa na TRAFFICK POLICE.
 
wakajengee nyumba za askari na sio kuwalaza binadamu wenzao tena na familia kwenye nyumba za mabati makuukuu!!
 
Kwa kweli siku hizi makosa ya barabarani umekuwa ni mtaji kwa nchi nyingi duniani.

Sio tu nyumbani hata Ulaya wanaongoza kwa kukusanya na faini ni kubwa mno kiasi ambacho siku hizi kuna kosa la speed tu unapewa faini ya £1000 sawa na 3m ya tz

Yaani huku ni mwendo wa heshima barabarani kama umeolewa na police hahaha

Sent from my SM using Tapatalk

Tofauti ya kwetu na ughaibuni ni huku kubambikiziana. Kwetu wamekubuu. Hiki ndicho kinachogomba.
 
Naomba kuuliza, nikisimamishwa na askari wa usalama barabarani akaniambia nimeoverspeed kwenye eneo la 50, halafu nikamwambia hapana si kweli, naye akasimamia msimamo wake huo, nikiomba ushahidi anasema amepigiwa simu, then baadaye akaniambia omba msamaha nikusamehe inakuwa inaashiria nini?
Inaashiria alikua anakupima ili ukitetemeka akupige mkeka.

Juzi kati nlipigwa mkeka kisa nimebeba BAG la nguo (Size Ya Kati) kwenye kiti cha abiria (Gari Ndogo). Na nilikua peke yangu sikua na abiria hata mmoja.

Kuna makosa mengine ONYO tu inatosha kumrekebisha mtu, sio lazima kupigwa mkeka, ila kwakua TRAFICK wamekua kitengo cha kukusanya mapato inakua zahma.
 
Back
Top Bottom