Jeshi la polisi laendeleza mauaji Wilayani Kahama kata ya Isaka.

The tourist

Member
May 15, 2011
32
7
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina Mrisho amekutwa amekufa ndani ya kituo cha polisi Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.. Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema kuwa marehemu alikamatwa jana kwa tuhuma za kukamatwa na Bangi na Gongo... Kwa mujibu wa maelezo ya askari wanasema kuwa marehemu alijinyonga usiku wa kuamkia leo.. Nilipojaribu kumuhoji Mkuu wa Kituo alikataa kusema lolote kwa madai kuwa yeye hakuwepo.

Mpaka muda huu kituo kimezingirwa na wananchi ambao wengi wao wanalalama kuwa Polisi wamehusika katika mauaji hayo... Ulinzi umeimarishwa. Polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi kutoka wilayani wapo hapa..

Mshangao ni kwamba inawezekanaje mtuhumiwa ajinyonge akiwa chini ya ulinzi wa polisi?
21901_175478019264508_876628373_a.jpg
 
Arushaone

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
15,044
12,981
The trained cops are ruining the good reputation of our beloved country... To stop this, there must be immediate reshufle from I.G.P, to the police HQs (seniors), every police stations and posts across the country. We are tired of this now.
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,343
23,816
[h=2]Jeshi la polisi laendeleza mauaji Wilayani Kahama kata ya Isaka[/h]
Kwa kuuza magazeti hilo ni bonge la title. Lakini thinking of its repurcussions to the society ndo maneno kama ya Nasjaz yanatokea.
 
Last edited by a moderator:

Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,292
1,137
Jeshi la Polisi limeasi amiri jeshi mkuu na sisi wananchi tunapaswa kuchukua hatua za dharula kuvunja jeshi hili la wauaji
 
Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,716
Watanzania tulieni, Msilalamike. Acheni polisi watekeleze kazi yao kwa kuwa hiyo serikali ya CCM mliiweka madarakani wenyewe!!
 
CRN

Member
Oct 24, 2012
60
8
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina Mrisho amekutwa amekufa ndani ya kituo cha polisi Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.. Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema kuwa marehemu alikamatwa jana kwa tuhuma za kukamatwa na Bangi na Gongo... Kwa mujibu wa maelezo ya askari wanasema kuwa marehemu alijinyonga usiku wa kuamkia leo.. Nilipojaribu kumuhoji Mkuu wa Kituo alikataa kusema lolote kwa madai kuwa yeye hakuwepo.

Mpaka muda huu kituo kimezingirwa na wananchi ambao wengi wao wanalalama kuwa Polisi wamehusika katika mauaji hayo... Ulinzi umeimarishwa. Polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi kutoka wilayani wapo hapa..

Mshangao ni kwamba inawezekanaje mtuhumiwa ajinyonge akiwa chini ya ulinzi wa polisi?
21901_175478019264508_876628373_a.jpg
poleni kwa tukio hilo mkuu,lakini naomba kufahamu kitu kimoja,umeshangaa mtu amewezaje kujinyonga akiwa chini ya ulinzi wa polisi,kwani kule lockup askari huwa wanakuwa na lindo kwa ajili ya mahabusu? kama ndiyo, basi polisi watupiwe lawama na sheria ichukue mkondo wake mara moja,lakini pia kama Jibu ni siyo,basi polisi wako safe kabisa,na hao waliozunguka kituo kama ni kwa nia mbaya basi na wao wanapaswa kutwangwa shaba japo za miguu kwa kutaka kujichukulia sheria mikononi mwao,ni hayo tu.
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,872
4,530
Bila wananchi kujifunza kuwalipizia kisasi watawamaliza bure. Hii mijamaa katili kweli. Kila siku inaua tena kwa kutumia risasi zilizonunuliwa kwa kodi zetu. Kwanini tusilipize kisasi kwa mmoja mmoja kila anapoonekana ili wajue na wananchi wana akili na uthubutu? Kazi kwa waathirika. Watatumwangosi hadi lini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom