The tourist
Member
- May 15, 2011
- 32
- 7
Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina Mrisho amekutwa amekufa ndani ya kituo cha polisi Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.. Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema kuwa marehemu alikamatwa jana kwa tuhuma za kukamatwa na Bangi na Gongo... Kwa mujibu wa maelezo ya askari wanasema kuwa marehemu alijinyonga usiku wa kuamkia leo.. Nilipojaribu kumuhoji Mkuu wa Kituo alikataa kusema lolote kwa madai kuwa yeye hakuwepo.
Mpaka muda huu kituo kimezingirwa na wananchi ambao wengi wao wanalalama kuwa Polisi wamehusika katika mauaji hayo... Ulinzi umeimarishwa. Polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi kutoka wilayani wapo hapa..
Mshangao ni kwamba inawezekanaje mtuhumiwa ajinyonge akiwa chini ya ulinzi wa polisi?