Jeshi la Polisi kwa uonevu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeshi la Polisi kwa uonevu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Sep 14, 2010.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Polisi wawalilia wakubwa
  Posted by GLOBAL on September 14, 2010 at 9:41am
  Send Message View GLOBAL's News

  Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
  Baadhi ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kambi ya Ukonga waliohamishwa kutoka katika kikosi hicho kwenda vikosi vingine ndani ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamelaani na kulalamikia vikali uongozi wao kwa kuwaamuru kuhama katika nyumba walizokuwa wakiishi kikosini hapo.

  Habari kutoka katika Kikosi hicho cha Kutuliza Ghasia Ukonga, zinasema kuwa chanzo cha malalamiko hayo ni pale waliposomewa taarifa ya uhamisho ambayo iliwataka kuhamia sehemu za kazi walizopangiwa.

  Aidha, chanzo chetu cha habari kimesema kuwa kimsingi si sahihi askari anapohamishwa kuachia nyumba hasa ikizingatiwa kwamba hajaenda nje ya kanda hii.

  “Ajabu ni kuwa baada ya kusomewa taarifa ya kuhama katika nyumba za FFU Ukonga, hatujalipwa kitu chochote kile kwa ajili ya kwenda kupanga nyumba nyingine uraiani,” alisema mmoja wa askari hao ambaye hakupenda jina lake kuwekwa wazi.

  Aidha, kufuatia kuhamishwa huko, baadhi ya askari hao wamemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, (IGP) Said Mwema kuingalia kati suala hilo kutokana na kile walichodai wameathirika kisaikolojia kwa kupewa uhamisho kisha kutimuliwa katika nyumba.

  Kwa upande wake, kamanda mmoja mwanadamizi wa kikosi hicho aliyeomba jina lake kutoandikwa gazetini alisema kuwa kimsingi askari wa kutuliza ghasia wote wanapaswa waishi kambini , maana kuna wakati huhitajika katika oparesheni maalum kama vile kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

  Hata hivyo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameingilia kati na kusema kuwa askari hao wapewe barua za kuripoti katika maeneo yao ya kazi kama kawaida lakini suala la kuhamishwa katika nyumba lisitishwe hadi ufumbuzi utakapopatikana.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sasa kama wao kwa wao wanafanyiana hivyo, what cn one expect inapokuwa ni raia huku mtaani!
  Ndio maana nilikataa ujeshi mimi, labda nikiwa mjeshi niwe IGP...BASI!
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wakitaka mabadiliko wanajua kwa kuegemea
   
Loading...