Jeshi la Polisi kuwasaka ma 'admin' wa 'whatsapp'

Jeshi la Polisi kuwasaka ma 'admin' wa 'whatsapp'

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,701
Reaction score
59,214
Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza kuwa kamata na kuwachukulia hatua wale wote wanaoendesha makundi ya ngono na wanaoweka picha za uchi na kujiuza kwenye mitandaoni ya kijamii.

Akizungumza na EATV Saa 1 leo jijini Dar es salaam, Joshua Mwangasa ambaye ni Mrakibu msaidizi wa jeshi la Polisi nchini, kutoka kitengo cha uhalifu wa mtandao amesema wanaendelea na uchunguzi wa kuwabaini wale wote wanaoendesha biashara ya kujiuza na kuweka picha za uchi kwenye mitandao ya kijamii hususan kwenye Watsapp na Instagram.

Ameiambia EATV Saa1 kuwa tayari watu kadhaa wamekamatwa na wanaendelea kuhakikisha kuwa wanawabaini wote, kwani kujiuza na kuweka picha za uchi ni kosa la jinai kupitia sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.

Amesema, Sheria hiyo pia inapiga marufuku mtu yeyote kuweka mtandaoni video au picha inayoonyesha ukatili wa kingono kwa watoto, hivyo yeyote atakaye tenda makosa hayo na kubainika mara moja atashikiliwa na jeshi hilo.

Mapema mwezi Septemba, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alitoa onyo kwa wasanii nchini kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii na endapo hatofanya hivyo basi watachukuliwa sheria stahiki dhidi yao.

Ambapo Septemba 21, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Faidha Omary maarufu kama Sister Fey alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kukiuka maadili kwa kuchapisha maudhui yanayodhalilisha kwenye mitandao ya kijamii kwa amri ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Chanzo: EATV
 
Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza kuwa kamata na kuwachukulia hatua wale wote wanaoendesha makundi ya ngono na wanaoweka picha za uchi na kujiuza kwenye mitandaoni ya kijamii.

Akizungumza na EATV Saa 1 leo jijini Dar es salaam, Joshua Mwangasa ambaye ni Mrakibu msaidizi wa jeshi la Polisi nchini, kutoka kitengo cha uhalifu wa mtandao amesema wanaendelea na uchunguzi wa kuwabaini wale wote wanaoendesha biashara ya kujiuza na kuweka picha za uchi kwenye mitandao ya kijamii hususan kwenye Whatsapp na Instagram.

Ameiambia EATV Saa1 kuwa tayari watu kadhaa wamekamatwa na wanaendelea kuhakikisha kuwa wanawabaini wote, kwani kujiuza na kuweka picha za uchi ni kosa la jinai kupitia sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.

Amesema, Sheria hiyo pia inapiga marufuku mtu yeyote kuweka mtandaoni video au picha inayoonyesha ukatili wa kingono kwa watoto, hivyo yeyote atakaye tenda makosa hayo na kubainika mara moja atashikiliwa na jeshi hilo.

Mapema mwezi Septemba, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza alitoa onyo kwa wasanii nchini kuacha kutumia vibaya mitandao ya kijamii na endapo hatofanya hivyo basi watachukuliwa sheria stahiki dhidi yao.

Ambapo Septemba 21, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Faidha Omary maarufu kama Sister Fey alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kukiuka maadili kwa kuchapisha maudhui yanayodhalilisha kwenye mitandao ya kijamii kwa amri ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
 
Mpaka ifikapo 2020 tutakuwa tumeisoma namba sawasawa!
 
Si demokrasia hio ? Tumepewa technology na wazungu kutumia mitandao na lazima tuwaihe wao kwao kuweka picha uchi ni kawaida sana na si maendeleo tunataka pia kuiga wazungu wanavaa nguo mpya ila zimechanwa maksudi na wanawawke kuwa wako karne 21 lazima waige huko ndio dunia kuelekea huko kwa kasi sana watazuia watashindwa maana u tube ni mali ya wazungu
 
Kwann wametangaza sasa......

Hivi ukiwa unataka kumkamata mhalifu/wahalifu, unawatangazia kabisa ili wajiandae kujificha au lengo la hili tangazo ni kupiga beat?!

Mbinu za kiboya sana za kupambana na uhalifu.....
 
Ilikuwa haina haja ya kutangaza kama kuna dhamira ya dhati kuwakamata hawa wajinga, maana kule instagram ukipitia comment kadhaa unakutana nao" muuza ****" mara njoo "nkifundishe kutomban" mara kungwi na majina mengine.......sasa kwa nini jeshi la polisi wasiwa DM wale watu kimya kimya alaf badae ndio waje watutangazie kwamba huyu ndio ajiita fulani kupitia mitandaoni.?
 
Kwahiyo unataka kusema kuwa serikali waachie haya mambo ya biashara za ngono ya endelee au tukuelewe vipi?!
Kama wewe ni msomi wa kweli lazma utakubaliana na mimi kuwa kuthibiti biashara ya ngono ni vigumu sana,wao kama serikali wangeweka utaratibu wa kutoza kodi kubwa sana na wale ambao wangeshindwa kumudu kodi hiyo lazma wangejitoa kwenye ushindani...ikiwa hivyo itapendeza zaidi!
 
Back
Top Bottom