sly boy
JF-Expert Member
- May 29, 2016
- 346
- 156
Jeshi la polisi nchini limetoa ufafanuzi kuwa halijazuia mikutano ya vyama vya siasa nchini walicho zuia wao ni mikutano ya hadhara ambayo walihisi hali ya usalama haikuwa nzuri.jeshi la polisi nchini limewataka wananchi kupuuza taarifa kuwa wao walizuia mikutano ya kisiasa.
==============
==============
June 2 2016, Jeshi la polisi nchini lilitoa tamko lililolenga kuzuia mikutano, maandamano ya kisiasa nchini kutokana hali za kiusalama kutokuwa sawa.
Leo July 09 2016, Jeshi la polisi nchini limetoa ufafanuzi kuhusu tamko la kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya kisiasa kuwa tamko hilo lililenga kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na tamko hilo halikupiga marufuku mikutano ya kiutendaji na kiutawala ya vyama vya siasa inayofanywa kwa mujibu wa katiba na kanuni za vyama husika.
Hivyo jeshi la polisi linawataka watu wasipotoshe watu kuhusu tamko hilo na pale hali ya kiusalama itakapotengemaa, mikutano na maandamano ya vyama vya siasa itaruhusiwa kufanyika.