Jeshi la Polisi: Hatujapiga marufuku mikutano ya kisiasa ambayo iko kwa mujibu wa katiba za vyama

June 2 2016 Jeshi la polisi nchini lilitoa tamko lililolenga kuzuia mikutano, maandamano ya kisiasa nchini kutokana hali za kiusalama kutokuwa sawa.

Leo July 09 2019 Jeshi la polisi nchini limetoa ufafanuzi kuhusu tamko la kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya kisiasa kuwa tamko hilo lililenga kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na tamko hilo halikupiga marufuku mikutano ya kiutendaji na kiutawala ya vyama vya siasa inayofanywa kwa mujibu wa katiba na kanuni za vyama husika.

Hivyo jeshi la polisi linawataka watu wasipotoshe watu kuhusu tamko hilo na pale hali ya kiusalama itakapotengemaa, mikutano na maandamano ya vyama vya siasa itaruhusiwa kufanyika.
Duuuuuh, hawa jamaa wanajua kweli kweli ku-play na mindset za wadanganyika...!! Sasa wameanza pole pole kuandaa mazingira ya kuuhalalisha mkutano wa chama kubwa baada ya kuona jamaa wa chama nyingine wamepania kuusimamisha kwa kukosa uhalali....!!
 
Hawa polisi wetu wanatumia nini kufikiri?kongamano la chaso iringa na dodoma ilikuwa mkutano wa hadhara?vp zuio la mkutano wa act ?au nawenyewe ulikuwa wahadhara?huu sasa ni utoto.waache kupelekeshwa na wanasiasa wanaweza kuingiza nch ktk machafuko
 
Jeshi la polisi nchini limetoa ufafanuzi kuwa halijazuia mikutano ya vyama vya siasa nchini walicho zuia wao ni mikutano ya hadhara ambayo walihisi hali ya usalama haikuwa nzuri.jeshi la polisi nchini limewataka wananchi kupuuza taarifa kuwa wao walizuia mikutano ya kisiasa.
==============

Ule wa zitto kijitonyama unaitwaije? Au ule ni mkutano wa maskofu?
 
"Hali ya usalama ikitengemaa". !!!!

Kwahiyo kipindi ambacho CCM wanataka kukusanyika (Vikao/Mkutano) ndo hali ya usalama inatengemaa, ila wengine wakikusanyika usalama unayumba .?!?!

Tuache ukada, tufanye kazi ya upolisi sio uchama ..!!
 
Hivi Kwanini Mfumo Wa Vyama Vingi Usifutwe??. Maana Kwa Issue Kama Hizi, Binafsi Naona Kama Hakuna Sababu Za Kuendelea Kuwa Na Vyama Vingi Wakati Vyama Vyenyewe Vinapigwa Vita Kama H.I.V
 
Mikutano ya hadhara ipo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ibara ya 11 kifungu cha 1 ili viweze kupata wanachama wapya
 
Jeshi la polisi nchini limetoa ufafanuzi kuwa halijazuia mikutano ya vyama vya siasa nchini walicho zuia wao ni mikutano ya hadhara ambayo walihisi hali ya usalama haikuwa nzuri.jeshi la polisi nchini limewataka wananchi kupuuza taarifa kuwa wao walizuia mikutano ya kisiasa.
==============
What?
Maswali juu ya jeshi la polisi ;
1. CHASO dodoma , Morogoro na Moshi mjini walifanyaje?
2. Kikao cha ACT wazalendo cha ndani cha kujadili bageti na kusababishia Zitto kupelekwa central ilikuaje?

N. B; Ifike mahala polisi na watawala waache kuwapotesha wananchi juu ya watendayo kwa umma.
 
Wanachokitafuta ipo siku watakipata.

Wanahamu sana ya kuyatumia maderaya na mabomu ambayo hayakutumika wakati wa uchaguzi.
 
1468072457292.jpg
 
Wanawaogopa bavicha.hata wajitetee vipi safari ya dodoma ipo palepale ,kama kufa tukafie huko huko.
 
Back
Top Bottom