Jeshi la Magereza kuanza kuwalipa wafungwa Nchini

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa magereza nchini ina mpango wa kuanza kuwalipa wafungwa ili wakitoka gerezani waweze kujikimu kiuchumi.

“Tumeshaanza kupata matunda ya kazi zao, tumeanzisha vitenga uchumi vingi kila gereza Tanzania, tunakoenda tutaanza kuwalipa, hii itasaidia pindi wanapotoka wanakuwa na kiasi cha kuanzia maisha,” Meja Jenerali Suleiman Mzee.

Kuhusu wanaotoka gerezani kisha kujihusisha na matukio ya uhalifu baada ya kitoka amesema mara nyingi inatikana na jamii inayomzunguka. “Magereza tumefanya kazi yetu inayotakiwa, kinachotakiwa ni jamii kubadilika, maana akitoka anaikuta jamii ileile ambayo ilifanya afanye makosa awali."

Source: ITV
 
Kwanza waanze kujilisha wenyewe kwa kuzalisha chakula cha kutosha, kwa sasa Seriakali inatumia Bajeti kubwa sana kuwalisha wafungwa na mahabusu, hivyo kwanza ni vyema Jeshi la magereza likajikita kwenye uzalishaji wa chakula cha kutosha ili kuokoa fedha zinazo tumika sasa, Kila Gereza nchi lijilishe kwa kuwatumia wafungwa kulima na kuzalisha kisha tukivuka lengo ndipo tufikirie kuwalipa.

Wafungwa ni nguvu kazi muhimu hivyo endpo kila gereza likahakikisha linawatumiwa wafungwa kwenye kilimo cha kisasa naamini wataokoa fedha nyingi sana.
shime kila gereza lijiwekee mkakati wa kuwatumia wafungwa kikamilifu ktk kilimo,kwanza wazalishe chakula cha matumizi yao wenyewe badala kutegemea fedha za Serikali kuwalisha na kuwahudumia.

kila kiongozi apimwe kwa lengo hilo.
 
Magereza wanajitegemea kwa 80%...mpka sasa

hiyo iliyobaki ni gawio kutoka government
 
Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa magereza nchini ina mpango wa kuanza kuwalipa wafungwa ili wakitoka gerezani waweze kujikimu kiuchumi.

“Tumeshaanza kupata matunda ya kazi zao, tumeanzisha vitenga uchumi vingi kila gereza Tanzania, tunakoenda tutaanza kuwalipa, hii itasaidia pindi wanapotoka wanakuwa na kiasi cha kuanzia maisha,” Meja Jenerali Suleiman Mzee.

Kuhusu wanaotoka gerezani kisha kujihusisha na matukio ya uhalifu baada ya kitoka amesema mara nyingi inatikana na jamii inayomzunguka. “Magereza tumefanya kazi yetu inayotakiwa, kinachotakiwa ni jamii kubadilika, maana akitoka anaikuta jamii ileile ambayo ilifanya afanye makosa awali."

Source: ITV
Mods unganisha huu Uzi..

Mama anaupiga mwingi
 
Kumbuka sio kila geleza lipo sehemu yenye kilimo, mfano ukonga wanaenda kulipa wapi ??
Stadi mbalimbali ,zingekua zinatolewa kulingana na mahali gereza lipo..
Mfano Ukonga.
Bustani (Mbogamboga)
Ufigaji Samaki pamoja na Kuku
 
Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee amesema kuwa magereza nchini ina mpango wa kuanza kuwalipa wafungwa ili wakitoka gerezani waweze kujikimu kiuchumi.

“Tumeshaanza kupata matunda ya kazi zao, tumeanzisha vitenga uchumi vingi kila gereza Tanzania, tunakoenda tutaanza kuwalipa, hii itasaidia pindi wanapotoka wanakuwa na kiasi cha kuanzia maisha,” Meja Jenerali Suleiman Mzee.

Kuhusu wanaotoka gerezani kisha kujihusisha na matukio ya uhalifu baada ya kitoka amesema mara nyingi inatikana na jamii inayomzunguka. “Magereza tumefanya kazi yetu inayotakiwa, kinachotakiwa ni jamii kubadilika, maana akitoka anaikuta jamii ileile ambayo ilifanya afanye makosa awali."

Source: ITV
Kwa sasa wasipewe hata mia ila watumiwe kuzalisha kwa kadiri iwezekanavyo ili jeshi liwe lafaida si omba omba serikalini huku linalisha mijitu mizima kibao
 
Magereza sio sehemu ya concentration camps.Ni sehemu ya kurekebisha tabia za wafungwa na sio kuzalisha mali.Ndo maana Zanzibar wanaita vyuo vya mafunzo.sio sahihi kugeuza wafungwa kuwa watumwa kuzalisha mali.Adhabu ni kunyimwa uhuru tu inatosha sio kufanyishwa kazi kama punda eti wajilishe.Siku ukiwa huko utajua ubaya wa hiyo dhana ya utumwa kwa wafungwa
 
Serikali ina ardhi ya kutosha, maeneo yapo mengi sana na makubwa, ukivuka chanika tu kuna pori la kutosha kulima mihogo n.k
NA sio hapo mjini chanika, itengenezwe program maalum ya kilimo na nguvu kazi iwe ni wafungwa, yatengenezwe mashamba makubwa ya ngano, mpunga, na nafaka zinginezo ili badala ya kuwafungia ndani na kuwalisha kwa miaka pengine kumi mpaka thalathini wawe katika hali ya uzalishaji wa mazao ya nafaka kwa ajili yao na taifa kwa ujumla hapa sasa tukiwalipa ni sawasawa.
 
Back
Top Bottom