kombaME
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 2,115
- 2,815
Habarini humu,
Jesca ni msichana mwenye urembo wa kati ila mvuto wake mkubwa upo kwa nyuma, amejaa vizuri na miguu minene inayoshabihiana na mtuno wake kwa nyuma, mwenye hipsi za mduara zinazokubali kutoa mvuto kwa kila nguo aliyokuwa anavaa Jesca
.
Nilibahatika kukutana na Jesca katika harakati za maisha, moyo wangu ulikiri moja kwa moja kuwa namhitaji nikaomba namba zake za simu na baada ya miezi kadhaa tukawa wapenz, wapenzi wenye mapenzi ya dhati, alinipenda nilimpenda.
Maisha yetu yalinyooka na ndipo tukapanga kufunga naye pingu za maisha. Ukweli ni kwamba tulipita kwenye msoto mkubwa mpaka kufika sehemu tukasimama wenyewe, muda ulipofika nikajiandaa vilivyo kwenda ukweni, nilipokelewa vizuri sana process zote za kuoa nilizifuata ndipo mahali nilipotajiwa.
Nikarudi nyumbani ili kujipanga kutoa mahali, Jesca alibaki kijijin kuendelea kusalimia ndugu na jamaa maana alitoka huko akiwa mdogo sana, baada kama wiki 2 hivi kupita Jesca alirudi mjini kuendelea na maisha, kama kawaida alikuja hom ili tupange lini tupeleke mahali na taratibu zingine za ndoa.
Kipindi tukiwa katika pilika pilika hizo siku moja alipokea simu kutoka kwa dada yake aliyekuwa anaishi Afrika kusini ikimtaka aende mara moja kwani kuna mzigo wa hela nying anataka ampe aulete bongo then pesa wagawane na ndo utakuwa mchango wake wa harusi, na eti atakuwa amenisaidia mimi.
Nikamwambia Jesca mimi sihitaji msaada wowote kutoka kwa dada yake kuhusu ndoa yangu ila kama wewe unaridhika kwenda sawa nenda ila usichelewe, Jesca akakataa kwenda maana alisema haoni umuhimu kama vipi aende kaka Yao mdogo ila dada alikataa kabisa baadae hata wazazi wakaingilia kuwa Jesca aende. Ndipo alipoondoka na kwenda Afrika kusini. Na hapo ndoto yetu ya ndoa ilipoisha.
Kumbe kule alikuwa ameandaliwa mwanaume mwenye asili ya Asia, na kumbe yule mwanaume alikuwa yupo pale kwa muda tu baadae akamtoroka Jesca, hapo tayari ilikuwa imepita miezi 11 sijawasilina nao hata nilipouliza kwa wazazi wake walinambia nao hawajui kilichotokea huko.
Nikakata tamaa,sasa nimekutana na Jesca, nilishangaa sana siku niliyomuona, alinisimulia kila kitu kilivyotokea kwa kweli imeniumiza sana, bado nampenda sana nayeye bado ananipenda sana ila kuna tatizo, Jesca amebadilika.
Sasa hivi ni mlevi kupindukia, anavuta sigara nahisi hadi bangi anavuta, ana majibu ya mkato sana na daima huwa anaongea maneno haya. Nakupenda sana ila nimepoteza ladha yangu ya mwanzo, dunia imenipa tabia ya ajabu nahisi sikufai kwasasa japo uliniahidi utakuwa namim kwa kila hali ila sio hii Kisha hucheka.
Wapendwa nimechanganyikiwa, sijui nifanye nini.
Naombeni ushauri wenu.