Jesca Msambatavangu ndiye nyoka wa SHABA, CCM Iringa Mjini

Mleta mada ni chadema huyo mama Jesca Msambatavangu ndie alimsaidia Msigwa kushinda ubunge iringa mjini na chadema kupata ushindi mkubwa sababu alikuwa timu Lowasa. Mnataka arudi mpite kwa mtelemko 2020.Huyo mama alikuwa CCM Kama kibaraka wa chadema na Lowasa.Yeye na mwenzie Kabongo ambaye alikuwa mweka hazina wa CCM wa pesa za uchaguzi waliifanyia kitu kibaya Sana tena CCM iringa mjini na kwa kazi nzuri ya usaliti Mara baada ya uchaguzi Kabongo alipewa ubunge viti maalum na chadema . Chadema mumeanza kampeni arudi baada ya kuona 2020 iko around the corner.Msigwa anahaha ndio maana kutwa anaitisha mikutano ya hadhara anayobeba watu Toka maeneo ya mbali ili mikutano yake ionekane ina umati wa watu .Hajiamini.Nina wasi hata huu Uzi aweza kuwa Msigwa ndie kaandika akampa Dr.Nko alete uzi humu kwa niaba yake.Dr fanya kazi ya kutibu watu acha kuzurura vilabuni na vijiweni
Kama ni kibaraka wa lowasa huoni sasa ndo muda mwafaka kumpa nafasi kwasababu mapenzi Yake hayapo CDM Bali kwa lowasa ambaye amedharudi Ccm?
 
Salaam wana jamvi!
Naandika uzi huu wa kitafiti kama sehemu ya JAMII TALKS, nikiwa na furaha ya ushindi wa timu yangu Liverpool kutinga fainal ya CL kwa kishindo dhidi ya Barcelona.

Nirudi kwenye mada, last week nimetimiza miezi 4 toka nihamie Iringa kikazi nikiishi eneo la Mkimbizi, nimehamia Iringa nikitokea Mkoa wa Arusha.
Miezi 2 baada ya uenyeji nilianza kufuatilia siasa za Iringa Mjini na siku ya Jumamosi nilibahatika kwa mara ya kwanza kufuatilia mkutano wa Mbunge wa hapa Mheshimiwa Peter Msigwa uliofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa.
Mkutano wa mbunge Msigwa ulikuwa na watu wengi na ulikaa kisiasa zaidi ingawa huyu Mchungaji sio wa kupuuzwa na kubezwa na CCM kama utafiti wangu unavyoonesha.
Kinywa cha Msigwa mina maneno ya kuudhi na kukera ambayo kwa wafuasi wake bado yanawapa morali na hamasa.
Jimbo la Iringa Mjini ni dogo lenye Kata 18 na Tarafa 1 pekee na limezungukwa na majimbo Kalenga,Kilolo na Isimani ambayo yote yapo CCM kwa Wabunge na Halmashauri.

Kwenye utafiti wangu ndipo nikakutane na jina la JESCA MSAMBATAVANGU almaafuru Madame Jesca.
Nikataka nimfahamu ni nani ndipo nikaanza kumfuatilia kupita maeneo mbalimbali ya wenye kunywa bia hadi ulanzi, wenye kula Mkate hadi Kande, wenye kukaa Uzunguni,Uhindini hadi Uswahilini, wenye kuangalia mpira hotelin hadi vibandaumiza.
Nikaona nafasi ya huyu Madame Jesca kama ndiye NYOKA WA SHABA kwa CCM hapa jimbo la Iringa Mjini.
Nimeambiwa huyu Mama amewahi kuwa Diwani wa kuchaguliwa Kata ya MIYOMBONI KITANZINI ambapo ndio Kata ya mjini aliingia mwaka 2012 kwenye uchaguzi mdogo na kuhudumu hadi mwaka 2015 alipochukua fomu ya kuomba ridhaa ya wana CCM kuwa mgombea Ubunge lakini hakufanikiwa.
Mwaka huo 2012 akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa na mwaka 2017 mwezi Machi alivuliwa uanachama wake na Kikao cha NEC kilichoketi Dodoma.
Madam Jesca alipata bahati ya kuwa mjumbe wa Bunge la Katiba 2014.
Kisiasa nje ya kuvuliwa uanachama wake inasemekana huyu Mama badi alibaki na imani yake ya Chama Cha Mapinduzi ingawa alikuwa hashiriki mikutano ya kisiasa lakini aliisemea pale CCM ilipokosolewa na kudhihakiwa na wapinzani.
Tarehe 18 Disemba,2018 Madam Jesca aliwekwa chini ya uangalizi maalum wa chama chini ya kikao cha NEC kilichoongozwa na JPM baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha baada ya kuvuliwa uanachama na wenzake 12 wakiitwa Wasaliti.
Ila kwenye sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM mlezi wao Mzee Mizengo Pinda alimtambulisha na kumpandisha mbele kuwasalimia wanachama wa CCM wa Iringa Mjini.
Wanachama walimshangilia sana na kumuomba mzee Pinda aseme kama chama wamemsamehe na kama bado wanamuombea msamaha kwa Mwenyekiti JPM.
Vijana wa Iringa mjini na Kina Mama ambao ndio wapiga kura wengi wanasema Madam Jesca anafikika kwa ukaribu na hujali sana shida za watu wanyonge, hajivuni na kipato chake zaidi ugawana na wahitaji.
Pia wanasema ni mtu wa kujichanganya kwenye shughuli za kijamii pasipo majivuno.

Nimebahatika zaidi kumfahamu Madame Jesca Msambatavangu mwenye umri wa miaka 43, mkulima na mjasiriamali mwenye shule ya msingi iliyopo Ipogolo na sekondari iliyopo Kitwiru zinajulikana kwa jina la STAR INTERNATIONAL SCHOOLS pia ana duka la kubadilishia fedha( Bureau de Change) ambayo ipo jengo la NSSF Iringa Mjini.
Analima ndani na nje ya Iringa kilimo biashara.

Huyu ndiye JESCA MSAMBATAVANGU ambaye CCM wanatakiwa kumfanya Nyoka wa shaba ili awavushe na kukomboa jimbo la Iringa Mjini.
Kwa utafiti wangu sijaona mwingine zaidi yake ingawa wapo wanaosemwa.
Alipata ajali ya kisiasa ila amesimama imara.

Wasalaam,

Dk Julius Nnko
Hospital ya Rufaa Iringa
Mkimbizi.View attachment 1091253View attachment 1091254

Ndugu yangu, ningekushauri tu uangalie zaidi kilichokupeleka Iringa ambacho ni kusimamia afya za binadamu.

Hayo masuala ya siasa, hasa za hapo Iringa, huwezi kuyaelewa na yaache yalivyo - siyo kwamba tunakukatisha tamaa ama kukupuuza, bali tunakwambia ukweli.

Hujui lolote la siasa za iringa, humjui Msigwa wala humjui huyo unayemwita Madame Jesca - HUMJUI!
 
Dk. Julius Nnko hayo mambo ya Iringa waachie wahehe wenyewe.
Nikupe tu siri Msigwa bila kumuibia kura hapo Iringa atatawala hadi afe, wahehe hawatakagi ujinga.
Mwakani CCM wamepanga kumpa ubunge Dr.Mahiga kwa gharama yoyote, mwambie Jesca najua yupo humu, asipoteze hela zake bure, mbunge ni Mahiga.
Mahiga ambaye amechezea ujana wake kwingine , leo kakongoroka ana miaka karibu 90 ndio apewe jimbo !
 
Dk. Julius Nnko hayo mambo ya Iringa waachie wahehe wenyewe.
Nikupe tu siri Msigwa bila kumuibia kura hapo Iringa atatawala hadi afe, wahehe hawatakagi ujinga.
Mwakani CCM wamepanga kumpa ubunge Dr.Mahiga kwa gharama yoyote, mwambie Jesca najua yupo humu, asipoteze hela zake bure, mbunge ni Mahiga.
msigwa si Mngoni yule watu wa iringa bwana
 
Salaam wana jamvi!
Naandika uzi huu wa kitafiti kama sehemu ya JAMII TALKS, nikiwa na furaha ya ushindi wa timu yangu Liverpool kutinga fainal ya CL kwa kishindo dhidi ya Barcelona.

Nirudi kwenye mada, last week nimetimiza miezi 4 toka nihamie Iringa kikazi nikiishi eneo la Mkimbizi, nimehamia Iringa nikitokea Mkoa wa Arusha.
Miezi 2 baada ya uenyeji nilianza kufuatilia siasa za Iringa Mjini na siku ya Jumamosi nilibahatika kwa mara ya kwanza kufuatilia mkutano wa Mbunge wa hapa Mheshimiwa Peter Msigwa uliofanyika kwenye uwanja wa Mwembetogwa.
Mkutano wa mbunge Msigwa ulikuwa na watu wengi na ulikaa kisiasa zaidi ingawa huyu Mchungaji sio wa kupuuzwa na kubezwa na CCM kama utafiti wangu unavyoonesha.
Kinywa cha Msigwa mina maneno ya kuudhi na kukera ambayo kwa wafuasi wake bado yanawapa morali na hamasa.
Jimbo la Iringa Mjini ni dogo lenye Kata 18 na Tarafa 1 pekee na limezungukwa na majimbo Kalenga,Kilolo na Isimani ambayo yote yapo CCM kwa Wabunge na Halmashauri.

Kwenye utafiti wangu ndipo nikakutane na jina la JESCA MSAMBATAVANGU almaafuru Madame Jesca.
Nikataka nimfahamu ni nani ndipo nikaanza kumfuatilia kupita maeneo mbalimbali ya wenye kunywa bia hadi ulanzi, wenye kula Mkate hadi Kande, wenye kukaa Uzunguni,Uhindini hadi Uswahilini, wenye kuangalia mpira hotelin hadi vibandaumiza.
Nikaona nafasi ya huyu Madame Jesca kama ndiye NYOKA WA SHABA kwa CCM hapa jimbo la Iringa Mjini.
Nimeambiwa huyu Mama amewahi kuwa Diwani wa kuchaguliwa Kata ya MIYOMBONI KITANZINI ambapo ndio Kata ya mjini aliingia mwaka 2012 kwenye uchaguzi mdogo na kuhudumu hadi mwaka 2015 alipochukua fomu ya kuomba ridhaa ya wana CCM kuwa mgombea Ubunge lakini hakufanikiwa.
Mwaka huo 2012 akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa na mwaka 2017 mwezi Machi alivuliwa uanachama wake na Kikao cha NEC kilichoketi Dodoma.
Madam Jesca alipata bahati ya kuwa mjumbe wa Bunge la Katiba 2014.
Kisiasa nje ya kuvuliwa uanachama wake inasemekana huyu Mama badi alibaki na imani yake ya Chama Cha Mapinduzi ingawa alikuwa hashiriki mikutano ya kisiasa lakini aliisemea pale CCM ilipokosolewa na kudhihakiwa na wapinzani.
Tarehe 18 Disemba,2018 Madam Jesca aliwekwa chini ya uangalizi maalum wa chama chini ya kikao cha NEC kilichoongozwa na JPM baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha baada ya kuvuliwa uanachama na wenzake 12 wakiitwa Wasaliti.
Ila kwenye sherehe za miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM mlezi wao Mzee Mizengo Pinda alimtambulisha na kumpandisha mbele kuwasalimia wanachama wa CCM wa Iringa Mjini.
Wanachama walimshangilia sana na kumuomba mzee Pinda aseme kama chama wamemsamehe na kama bado wanamuombea msamaha kwa Mwenyekiti JPM.
Vijana wa Iringa mjini na Kina Mama ambao ndio wapiga kura wengi wanasema Madam Jesca anafikika kwa ukaribu na hujali sana shida za watu wanyonge, hajivuni na kipato chake zaidi ugawana na wahitaji.
Pia wanasema ni mtu wa kujichanganya kwenye shughuli za kijamii pasipo majivuno.

Nimebahatika zaidi kumfahamu Madame Jesca Msambatavangu mwenye umri wa miaka 43, mkulima na mjasiriamali mwenye shule ya msingi iliyopo Ipogolo na sekondari iliyopo Kitwiru zinajulikana kwa jina la STAR INTERNATIONAL SCHOOLS pia ana duka la kubadilishia fedha( Bureau de Change) ambayo ipo jengo la NSSF Iringa Mjini.
Analima ndani na nje ya Iringa kilimo biashara.

Huyu ndiye JESCA MSAMBATAVANGU ambaye CCM wanatakiwa kumfanya Nyoka wa shaba ili awavushe na kukomboa jimbo la Iringa Mjini.
Kwa utafiti wangu sijaona mwingine zaidi yake ingawa wapo wanaosemwa.
Alipata ajali ya kisiasa ila amesimama imara.

Wasalaam,

Dk Julius Nnko
Hospital ya Rufaa Iringa
Mkimbizi.View attachment 1091253View attachment 1091254
Hivi hakuna sub forum ya COM? Hilo kichefu chefu ni shida.
 
Wakimsikia Msigwa na CAG Vigogo wa Chama kya Mapinduzi huwa wananywea.
 
Kama ni ubunge ccm ya magufuli ikiutaka inaupata tu.
Hivi ni kwa nini wana CCM huwa mnapenda kutengeneza picha kwamba Magufuli ni mtu wa kutumia mabavu? Yaani maana ya hii sentensi ni kwamba hata watu Iringa wakikataa ili mradi "CCM ya Magufuli" inautaka ubunge itaupata tu.

Nyie watu mmejaza chuki na hamu ya kutumia mabavu kwenye vichwa na mioyo yenu kiasi kwamba hata kusema mnatumiwa na shetani itakuwa ni kuwapendelea!
 
CCM hawamuhitaji huyo Jesca wala nini...inachohitaji ni polisi na vijana wa Green Guard tu, majimbo na kata zote na vijiji vyote Tanzanua wanachukua
 
Hivi ni kwa nini wana CCM huwa mnapenda kutengeneza picha kwamba Magufuli ni mtu wa kutumia mabavu? Yaani maana ya hii sentensi ni kwamba hata watu Iringa wakikataa ili mradi "CCM ya Magufuli" inautaka ubunge itaupata tu.

Nyie watu mmejaza chuki na hamu ya kutumia mabavu kwenye vichwa na mioyo yenu kiasi kwamba hata kusema mnatumiwa na shetani itakuwa ni kuwapendelea!
Ndio hali halisi hiyo mkuu, mimi sio mwana CCM ila najua 2020 CCM inashinda majimbo na kata zote... Tumeona kwenye chaguzi ndogo mambo yanavyokuwa
 
Uyu Dada aachane na siasa, nje ya siasa atafanikiwa sana kwakua ana akili na kipaji cha kutafuta fedha, siasa za bongo zinampotezea muda.
Naunga mkono hoja.Nimezaliwa iringa na kukulia iringa lakin kwa mara ya kwanza nilipata kumfaham huyu dada (enzi akiwa dada) nikiwa kidato cha 6 tosamaganga.She is very smart kwenye masuala ya utafutaji na huko ndiko haswa anapaswa aelekeze nguvu zake.hiz siasa ni kwel naona kama zinampoteza tu ingawa ninkama ilivyo ada,ukitaka kuw mfanya biashara wa level za juu sana kibongo bongo nafasi ya kisiasa ina matter sana kukubeba ili kukurahisishia baadhi ya mambo.Na hicho ndio nadhan ana struggle nacho huyu mama.Otherwise she is smart kwakwel kwenye utafutaji
 
Ukiona ni garasa basi ndio sahihi huyo.
Wewe endekeza ushabiki maana mimi nipo kitafiti zaidi

Upo kiutafiti wakati polisi na tume ya uchaguzi wanaambiwa na rais mgombea wa ccm ndio atangazwe mshindi? Huko hufanyi utafiti bali unajiuza. Ccm chini ya Magufuli haiwezi siasa za ushindani fullstop.
 
Dk. Julius Nnko hayo mambo ya Iringa waachie wahehe wenyewe.
Nikupe tu siri Msigwa bila kumuibia kura hapo Iringa atatawala hadi afe, wahehe hawatakagi ujinga.
Mwakani CCM wamepanga kumpa ubunge Dr.Mahiga kwa gharama yoyote, mwambie Jesca najua yupo humu, asipoteze hela zake bure, mbunge ni Mahiga.
Kwani Msigwa ni Mhehe?!
 
RC Hapi, nakuomba uendelee kuwanyoosha madaktari wa Iringa, hasa wa hiyo hospitali ya Rufaa ya Mkoa
 
Hao ndio waliivuruga ccm huko iringa. Wapo tayari kuvunja misingi ya chama wanapoona mahali kuna maslahi. Akiwa mwenyekiti wa ccm mkoa kipindi cha kutafuta kura za maoni wagombea alidiriki kumzimia magufuli jenereta ye akiwa kambi ya lowasa. Kitendo kile kilimkwaza sana magufuli. Kwao ccm wanaona hayo makundi yalikuwa yanazamisha chama na kukifanya chama miliki ya watu wachache. Kama ni ubunge ccm ya magufuli ikiutaka inaupata tu. Ye aendelee kujifunza kuheshimu watu maana hujui kesho ya mtu.
Mimi sio mwana ccm na sijawahi kua mwana ccm hata mara 1 but niseme hivi, kwanza nikiri kwamba hata mimi namfahamu JEsca Msavatavangu ( wengi wanakosea surname yake ). Namfahamu tokea akiwa kinda kabisa akiwa anavaa sketi nyeusi na blouzi nyeupe (usiniulize sana kuhusu hizo rangi za nguo zake) ni mwanamke jasiri sana na mengi aliyozungumza Dr (though Dr najua kajitambulisha kimkakati Zaidi ) ni ya kweli as far as I know her. Hivi Mhe raisi wakati ule na Lowassa si walikua chama kimoja? Wakati wa kutafuta KURA za maoni, kuna dhambi gani wana chama wakiwa na makundi? Kama kuna kitu mnakikosea sana wana ccm ni hiki, kwamfano Loawassa angepita na kua raisi may be, je asingemchagua mhe rais wa sasa hvi kua waziri? Acheni mambo ya kizamani na ya kijima, wakati wa kutafuta mgombea, makundi hayaepukiki, iwe kwenye dini, siasa, mpirani na kote, makundi yatakua mabaya tu endapo baada ya uchaguzi watu watayaendeleza, period.
 
Kwanza
karibu sana Dk Julius Nnko Iringa , na kwa upekee Mkimbizi,

Sisi ndo wazaliwa wa hiyo mitaa.

Siasa za Iringa bwana changamoto, Sababu pekee iliyomfanya Msigwa achaguliwe Iringa kwa mara ya Kwanza, ilikuwa kwa sababu wahehe walipewa mtu wasio mtaka, walikuwa wanamtaka Mwakalebela, wakapewa mama Mbega ambae kwa wakati ule walikuwa wamemchoka.

Kwa sasa ni kweli Madam Jesca ana ushawishi mkumbwa, ila historia yake ya uchaguzi wa mwaka 2015, inaweza ikawa kikwazo ktk kukubalika na wana CCM iringa,

Pili kuna Madam Ritha Kabati, nae anatajwa tajwa sana midomoni mwa watu, na anakubalika miongoni mwa makundi ya Vijana na Akina mama, huyu ndo mpinzani nambari moja kwa Jesca ndani ya CCM, Amekuwepo bungeni kwa miaka kumi sasa kama mbunge wa viti maalum mkoa, nafasi ambayo ameitumia vyema kujinadi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom