SI KWELI Jesca Magufuli sina amani, nawindwa mpaka Nyumbani

SI KWELI Jesca Magufuli sina amani, nawindwa mpaka Nyumbani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na chapisho linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook likiwa na ujumbe wenye nukuu inayosema “ Jesca Magufuli sina amani nawindwa mpaka Nyumbani”je ni upi ukweli wa chapisho hili
Jesca.jpg
 
Tunachokijua
Jessca Magufuli ni mbunge wa viti maalum anayesimamia kundi la vijana. Pia Jessica ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Madai

Kumekuwa na grafiki yenye picha ya Jessica Magufuli ikiambaana na ujumbe unadai kuwa mbunge huyo amesema kuwa hana amani anawindwa hadi nyumbani.

Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa Taarifa hiyo si yakweli.

Ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo 'key word search' umebaini kuwa hakuna chanzo chcochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo.

Aidha hakuna kumbukumbu yoyote ya hivi karibuni inayoonesha kuwa mbunge huyo alifanya mahojiano na chombo chochote cha habari kueleza madai hayo.

Ufuatiliaji zaidi umebani kuwa mbunge huyo hajachapisha pia hata kupitia mitandao ya kijamii mbunge huyo hakuchapisha taarifa yoyote ya aina hiyo.
"Ili kuthibitisha usahihi wa habari hii inayodaiwa kuwa potofu, ni muhimu kupata kauli ya moja kwa moja kutoka kwa Jesca Magufuli au mamlaka husika, badala ya kutegemea tetesi zinazosambaa mitandaoni."
 
Back
Top Bottom