Huyu ni mwanasiasa kijana na msomi pia ni meya wa manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, Tanzania. Aliyeyofanya Ilala yanaonekana kwa macho na wala huitaji kuandika hapa.
Pichani akitoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi. BRAVO Mstahiki Meya.
mdau,uwaambie wasioishi dar es salaam,tunaoish dar es salaam tunajionea upuuz,dar es salaam including Manispaa ya Ilala ni chafu mno,huyo Jerry kule tweeter anakiri kuwa kazi imemshinda,wewe unakuja kumsifia hapa si unafki huo,
nakupa kaz ndogo sana leo kama utapata nafas zungukia masoko yafuatayo
1.soko la Ilala
2.Soko la Bugurun
3.Soko la Kigogo
angalia hali ya uchafu pale,last week alisema tatizo ni mvua,ila uchafu wa dsm hauna mvua wala kiangazi
then nakupa kazi nenda mitaa ya kariakoo,hesabu idadi ya chemba zinazotoa maji machafu kiholela then muulize Jerry atakwambia kazi ya dawasco si yake,
Njoo kwenye ubovu wa barabara,pita barabara ya uhuru hasa maeneo ya mtaa wa Congo,pale hakuna mvua,hakuna kiangazi maji yametapakaa,wakat wa mvua ukiwa na Carina hupiti pale,ukimuuliza Jerry atakwambia tatizo sheria,nenda huko huko kwenye kata yake na maeno alikotokea,anzia ukonga mpaka Gongo la Mboto uchafu unamuandama,
sasa njoo kwenye usimamizi wa ujenz,hayo maghorofa yanayojengwa bila kiwango yeye kama kiranja wa manispaa anasimamia vip yasijengwe???,
Jerry alikua na ham na umeya,ila sasa mambo yamemshinda,nae amekua kama mameya wenzie wa hapa dsm,yaan wa Temeke na Kino,sasa wale ni wazee,huyu kijana mwenzetu ana nini???,