Jerry Slaa kujenga soko Kisutu

Jerry Slaa kujenga soko Kisutu

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,537
Reaction score
6,479
Hili ndilo soko la kisasa ambalo Jerry Silaa amesema anataka kukumbukwa kwa kulijenga.

Jerry-Slaa.jpg
Nimejiuliza maswali kadhaa:

1. Hivi, wakati ulimwengu wa kisasa unahangaika na kusindika bidhaa na kuziuza kwenye malls kubwa zikiwa packed vizuri, sisi Watz bado tuna ndoto ya kujenga masoko ya kizamani ya kuuza mchele kwenye vibaba, nyanya za kuhesabu, ndizi za kuhesabu kila kitu kama lile soko la Kariakoo?

Kwanini wasingekuwa na mawazo ya kujenga shopping malls (kama ile ya Mlimani City) ili watu wapange pale kufanya biashara? Faida ambayo ataipata kwa hao wauza nyanya na mchele katika kodi ya pango ni ndogo kuliko ambayo angeipata kwa wafanya biashara wakubwa ambao wangeweka maduka makubwa ya biashara za kisasa hapo.

Sasa hii ndio mindset ya watu tunaowapa uongozi, wanawaza mambo ya kizamani tu. Mambo ya karne hii mpya hayapo kichwani mwao.

=========

Jerry Slaa kashea hii ramani ya soko la kisasa la Kisutu!

Jerry-Slaa.jpg

Baada ya kuvunjwa kwa baraza la halmashauri ya Manispaa ya Ilala July 6,2015 na aliyekuwa meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Slaa kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amepost miongoni mwa kazi zitakazotekelezwa kwa wananchi ikiwemo huu ujenzi wa soko la kisutu ambalo muda si mrefu litaanza kufanyiwa maandalizi ya kujengwa.

Chanzo:
MillardAyo
 
Anajenga kwa fedha zake? Sema jiji kujenga soko la kisasa kisutu!
 
yeye amepost hiyo picha ya soko analosema litajenga muda si mrefu na anasema atakumbukwa kwa lipi? akimaanisha kuwa kuna kitu kikubwa ameifanyia ilala katika umeya wake. kujenga soko la kuuza mchele wa vibaba na nyanya za kuhesabu badala ya maduka ya kisasa yanayojengwa na nchi za wenzetu.
 
nafarijika sana nikiona watu wana mitizamo chanya kama hii. naamini ipo siku tutaendelea tu. big up Haki sawa, Hute na wote mliokosoa huu mpango wa kufikiria kizamani
 
Isiishie kwenye makaratasi

Acha upimbi wewe, Jerry Slaa siyo meya tena baraza la madiwani limevunjwa jana.

Huu upumbavu akashare na wapumbavu wenzake Ccm ndio awaletee dharau hizi badala ya kuonesha alichofanya anatuletea picha mpuuzi mkubwa huyu.
 
nafarijika sana nikiona watu wana mitizamo chanya kama hii. naamini ipo siku tutaendelea tu. big up Haki sawa, Hute na wote mliokosoa huu mpango wa kufikiria kizamani

Hamna kitu, kawa meya wa Ilala, cha maana alichofanya nini? Sanasana kapiga hela kwenye gari za zoa taka, ndio maana wapigaji wenzie wakamshtukia, wakaona anafaidi, wakaamua kuichukua. Hii ndio CCM zaidi ya uijuavyo.
 
Ameshindwa usafi Kariakoo, DDC Kariakoo watu wanapiga fedha wanajiondokea, kwenye vitabu wanasema wanakodisha kwa Tshs 200,000/ kwa mwezi wakati mteja anatoa mil. 1 kwa mwezi, laki 8 zote wanatia mfukoni.
 
Watu wa aina hii ndo wale waliokuwa wakisema wanataka rais kijana. Tatizo ni akili. Slaa ukimuangalia anafaidi ile hali ya CCM. immunity. Anapata immunity ambayo inalazimika kumshangilia kiasi kwamba hata leo ukimuuliza udhaifu wake haujui kabisa na anaweza kukueleza kwamba ana ufahamu mkubwa. Wengine kama akina Millard wanamfuata tu na kumtangaza bila hata kujua ubora wake, lakini hakika ufahamu hauongezeki kwa kutajwa redioni.

Kama ulivyosema, sijui ujenzi wa soko kama hili utakuwa unatatua tatizo gani? Kuna ajira itakayoongezeka hapo? Hapana! Lakini kuna ufisadi ambao siku hizi unakumbukwa na viongozi wote wa aina hii. Ujenzi wa majengo umekuwa ni miradi muhimu sana ili pesa zichotwe. Hapo kuna 20% za hao wanataka tuwakumbuke.
 
Kumepambazuka ndio anataka kudanganya watu...wakati wa umeya wake Ilala haijawahi huwa chafu kama sasa. Alijimilikisha makampuni ya takataka tukawa hatuwezi kuyahoji, Barabara mashimo matupu, aliingia taa za barabarani zinawaka, leo zote zimekia miti tu isiyo matunda.

Ameshindwa kubuni njia bora za kuondoa adha ya foleni, amekuwa akianzisha miradi ya kupata fedha ya kuweka matufali kwenye pembe za barabara zenye mashimo... yaani barabara yenyewe haipo lakini pembeni anaweka matofali ..wizi mtupu. Ameanzisha na watu wa fire ati kila nyumba ilipe fire, badala ya kutuambia tununue vifaa vya moto yeye tutoe tozo

Hilo soko atalojenga ni pia ubadhirifu na wizi ameuza kiwanja hicho ili waendedhe matajiri ...yatakuwa kama soko la machinga Ilala mpaka leo lipo tupu.. wewe unafikiri muuza nyanya ataweza kulipa kodi kwa investor anayetaka kurejesha fedha zake? Wamepeana tenda za parking, fedha hazijulikani zinafanya kazi gani.

Fedha za billbords na mabango ni mabilioni kwa mabilioni, hazijulikani zinakwenda wapi. Huyu jamaa kumrejesha tena kwenye uongozi basi tutakuwa wendawazimu... nadhani ndio maana kaenda Ukonga huko... labda watu watamchagua kwa u handsome
 
Jerry the Spender anakumbuka shuka when is too late .
 
Tatizo sio Jerry, tatizo ni wakazi wa jiji la Dsm!
 
Muda wa uongozi unaisha ndiyo anataka kujenga? Au ndio anaanza kampeni kwa muhula ujao?
Hizi ni dalili za kuwafanya wananchi ni wajinga kupundukia!
 
Mbona Muda wake wa Umeya wa mkoa wa Ilala umemalizika; je, atalijenga akiwa raia wa kawaida bila Mapato? Basi ni vema pia akatuambia ni vyanzo vipi atavitumia kukamilisha ndoto zake hizi zilizomshinda kwa miaka mitano ya uongozi wake.

Hana sera huyo; anachotaka ni kuwaadaa wana Ukonga ili apate ridhaa ya kwenda kusema ndioooooooo bungeni, kama kawaida ya CCM wenzake.
 
Kabla hujaanza conclusion ni vyema ungeanza na kuuliza soko hili litakuwa na facilities gani. Pili ukae ukijua sio watanzania wote wakiwemo wakazi wa Ilala wana fursa ya kwenda mlimani city. Bado watu wanahitaji masoko yao wanunue nyanya na michele. Na labda hujawahi kwenda soko la kisutu. Hakuna mchele wala nyanya za vibaba.

Wanapima kwa kilo na naamini soko la kisasa litawapa fursa kubwa zaidi wasindikaji wa ndani kuuza bidhaa. Tutajenga hili, tutajenga Ilala na Buguruni na tutajenga Mchikichini sisi wa Gongolamboto tukanunue mitumba wakati wakubwa mko mlimani city.
 
Inatarajiwa kuleta ushindani mkali sana kwa "magodown" yaliyopo njia panda ya kwenda chuo kikuu cha mlimani (UDSM).

Wanajenga lini wakati muda wa madiwani pamoja ma Meya umeisha na madiwani wapya bado hawajachaguliwa.
 
Back
Top Bottom