Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,030
- 59,682
Katika hatua nyingine, halmashauri hiyo imesema itawashtaki wamiliki wa mabango ya biashara walioshindwa kulipa ushuru ambao unafikia Sh984 milioni. Silaa alisema karibu kampuni 20 zinadaiwa ushuru wa mabango na halmashauri hiyo zikiwamo kampuni ya simu za mkononi, kampuni ya vinywaji na kampuni zinazohusika kuweka mabango.
Agizo la Magufuli kuhusu barabara Dar lisipuuzwe
Tuesday, 06 March 2012
TATIZO la usafiri jijini Dar es Salaam linalokwenda sambamba na kuongezeka kwa msongamano wa magari, limesababisha kero kubwa kwa wakazi na wageni wanaoingia katika Jiji hilo.
Tatizo hili sugu ni la muda mrefu na linaendelea kukua kadiri muda unavyozidi kwenda kana kwamba nchi hii haina sheria wala viongozi wanaojua kusimamia utawala bora na usimamizi wa sheria.
Mara nyingi viongozi wa umma kuanzia Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kupitia halmashauri ya Jiji na manispaa zake tatu wamekuwa wakipiga kelele na kutoa maagizo makali yasiyozaa matunda kutokana na ufuatiliaji na usimamizi mbovu.Kutokana na hali kuendelea kuwa mbaya, akizindua kituo cha mabasi cha Kimara juzi, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alimpa siku tano Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa Dar es Salaam kuwaondoa katika hifadhi za barabara watu wote waliozigeuza sehemu hizo kuwa maeneo yao ya biashara kinyume cha sheria.
Tunampongeza na kumuunga mkono Dk Magufuli kwa hatua hiyo muhimu, tukijua kuwa alichoagiza kitatekelezwa katika muda uliowekwa na isipofanyika hivyo atawachukulia hatua viongozi wa Tanroads kwa kutotekeleza agizo lake.
Sisi tunaounga mkono agizo la Waziri Magufuli kwa sababu hali halisi ilivyo sasa katika jijini Dar es Salaam ni kana kwamba hakuna uongozi, kwani karibu maeneo yote yenye nafasi yamegeuzwa kuwa masoko.
Kwa mfano, hivi sasa sehemu nyingi za kandokando ya biashara na hasa kwenye vituo vya mabasi na daladala yameguzwa masoko hivyo kusababisha kero kubwa kwa wasafiri.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba, katika vituo vya daladala vimejengwa vibanda vya wasafiri kukaa na kusimama kujikinga na jua au mvua, lakini karibu vyote vimegeuzwa kuwa vibanda vya mama lishe, wauza vipodozi, pipi na karanga na vitu vingine. Kibaya zaidi hakuna anayechukua hatua ya kuwaondoa.
Mfano mmoja wapo ni katika vituo vya daladala Buguruni, Ubungo, Manzese Tegeta, Mbagala na kwingineko, vibanda vyote vimegeuzwa kuwa vya biashara. Tanroads ambao ndiyo wenye dhamana ya kusimamia barabara na uongozi wa jiji na manispaa zake wapo, wanapita katika maeneo hayo na wanaona kinachoendelea, lakini wanajifanya hawaoni.
Barabara za pembezoni nazo zinageuzwa kuwa maegesho ya malori na sehemu mbalimbali zimeharibiwa kutokana na uzito wa malori ambao haulingani na viwango vya barabara hizo, na hakuna anayewachukulia hatua wala kuwaondoa. Serikali imewahi kutoa amri ya kuyaondoa na kuwachukulia hatua madereva na wamiliki wa malori hayo, lakini maagizo hayo yameguzwa kiitikio cha wimbo wa Taifa kutokana na kutotekelezwa, na wahusika wamekaa kimya tu.
Tunachosema ni kwamba, kama kweli kauli ya Dk Magufuli ina nguvu, itapendeza kuona utekelezaji unafanyika na hatua zikichukuliwa kwa watakaokwamisha, ili agizo hilo lisichukuliwe kuwa kelele za kisiasa zisizotekelezeka.
Yanayofanyika katika Jijini Dar es Salaam ni ishara tosha kuwa hakuna uongozi makini na waliopo wanaangalia masilahi yao ya kisiasa kwa kujipendekeza kwa watu wanaokiuka sheria ambazo wanaapa kuzifuta na kuzilinda wanapoingia madarakani.
Kama Tanroads wanashindwa kusimamia barabara wanazotengeza tuwaelewe vipi? Kama uongozi wa Jiji na wa manispaa wanashindwa kusimamia sheria hivyo kulifanya jiji kuwa na masoko kila mahali hata kandokando ya barabara, maegesho ya magari na sehemu nyingine zisizoruhusiwa tuwaelewe vipi zaidi ya kuwa wameshindwa kazi?
Tunakumbuka kuwa kabla Halmashauri ya Jiji kuvunjwa mwishoni mwa miaka ya 90, lilikuwa katika hali mbaya mpaka lilipowekwa chini ya uongozi wa tume uliyoongozwa na Charles Keenja ambayo ilifanikiwa kuyabadilisha mandhari yake kuwa safi. Kama iliwezekana kwa tume, halmashauri ya jiji yenye manispaa tatu inashindwa vipi?
Kibaya zaidi wanaofanya biashara katika maeneo hayo wanatozwa ushuru na mamlaka za halmashauri na kuwafanya waamini kuwa wana haki ya kuwa hapo kisheria; kwani huwezi kumtoza kodi mtu katika eneo lililopigwa marufuku zaidi ya kumwondoa.Tunashauri kwamba, agizo la Dk Magufuli litekelezwe bila kizuizi ili kujenga nidhamu ya Taifa.
Wajameni huyu meya huyu namfahamu, kiukweli ni kati ya hazina kubwa chache za vichwa vya ukweli CCM ilivyonavyo japo nakiri kwenye suala hili ameshindwa kujieleza vyema.
Sehemu yuko right na sehemu yuko wrong na Magufuli yuko right kwa asilimia 100%.
Ni kweli Halmashauri zina mamlaka yake ambayo hayapaswi kuingiliwa na serikali kuu ikiwemo mabunge yake (mabaraza ya madiwani) ambayo yanamamlaka ya kisheria kujitungia bylaws zake. Hivyo mabango yapo kisheria na yana mikataba halali na halmashauri husika, hivyo meya yuko right, mabango hayo hayawezi kungolewa kwa agizo la siku 7 kama Magufuli alivyogiza!.
Alichofanya Magufuli ni kusisitiza matakwa ya kisheria ya utekelezaji wa sheria mpya ya road reserve ya mwaka 2007 ambayo inakwenda kinyume cha by laws za halmashauri, hivyo licha ya sheria hiyo kupitishwa, halmashauri zilipaswa kutengua bylaws zake na kuzioanisha na sheria hiyo mpya, kitu ambacho hakikufanyika na badala yake Halmashauri zimeendelea kurenew mikataba ya mabango kwa sheria za zamani ili kuendelea kuvuna pesa nene!.
Hata hivyo ukweli wa mambo, uinguliaji mkubwa wa road reserve sio mabango, ni vibanda vya biashara na wafanya biashara ndogondogo ambao hawako covered kwenye by laws za halmashauri.
Alichotakiwa kusema huyu meya ni kuamuru utekelezaji wa kuwaondoa hao wafanya biashara kwanza na kusema mchakato wa kuyaondoa mabango ufuate matwakwa ya kisheria ili halmashauri zisiingie kwenye migogoro ya kisheria na kesi za madai kufidia hasara ya kuvunja mabango ya watu yaliyokuwepo kabla ya sheria hiyo kupitishwa!.

Pasco, hapo kwenye red natofautiana na wewe kabisa. Huyo dogo ni mzigo kwa nchi hii. Hana la maana zaidi ya kutetea mabango kwa sababu mabango ni ATM yake binafsi. Tumekuwa tunasikia kelele za kutaka vijana wapewe nafasi za uongozi then tunapata aina ya hii ya Jerry Silaa! Kafanya nini tangu awe meya wa Ilala zaidi ya kuuza sura kule michuzi blog? kasafisha mitaro? kaweka taa barabarani? kasaidia usafiri kwa wanafunzi ndani ya manispaa yake? Kaondoa foleni ya magari Ilala? Amefanya nini mpaka tuseme meya ni hazina?Wajameni huyu meya huyu namfahamu, kiukweli ni kati ya hazina kubwa chache za vichwa vya ukweli CCM ilivyonavyo japo nakiri kwenye suala hili ameshindwa kujieleza vyema.
.
Kama sheria ya bara bara imetungwa mwaka 2007, kwa nini hadi leo manispaa hawajarekebisha by-laws zao kuendana na sheria mama?
Pasco,Wajameni huyu meya huyu namfahamu, kiukweli ni kati ya hazina kubwa chache za vichwa vya ukweli CCM ilivyonavyo japo nakiri kwenye suala hili ameshindwa kujieleza vyema.
Sehemu yuko right na sehemu yuko wrong na Magufuli yuko right kwa asilimia 100%.
Ni kweli Halmashauri zina mamlaka yake ambayo hayapaswi kuingiliwa na serikali kuu ikiwemo mabunge yake (mabaraza ya madiwani) ambayo yanamamlaka ya kisheria kujitungia bylaws zake. Hivyo mabango yapo kisheria na yana mikataba halali na halmashauri husika, hivyo meya yuko right, mabango hayo hayawezi kungolewa kwa agizo la siku 7 kama Magufuli alivyogiza!.
Alichofanya Magufuli ni kusisitiza matakwa ya kisheria ya utekelezaji wa sheria mpya ya road reserve ya mwaka 2007 ambayo inakwenda kinyume cha by laws za halmashauri, hivyo licha ya sheria hiyo kupitishwa, halmashauri zilipaswa kutengua bylaws zake na kuzioanisha na sheria hiyo mpya, kitu ambacho hakikufanyika na badala yake Halmashauri zimeendelea kurenew mikataba ya mabango kwa sheria za zamani ili kuendelea kuvuna pesa nene!.
Hata hivyo ukweli wa mambo, uinguliaji mkubwa wa road reserve sio mabango, ni vibanda vya biashara na wafanya biashara ndogondogo ambao hawako covered kwenye by laws za halmashauri.
Alichotakiwa kusema huyu meya ni kuamuru utekelezaji wa kuwaondoa hao wafanya biashara kwanza na kusema mchakato wa kuyaondoa mabango ufuate matwakwa ya kisheria ili halmashauri zisiingie kwenye migogoro ya kisheria na kesi za madai kufidia hasara ya kuvunja mabango ya watu yaliyokuwepo kabla ya sheria hiyo kupitishwa!.
big joke again ..mkuu ni kweli inasikitisha yaani tunaenda enda tu hatujui tunaenda wapi ..nchi haina mwenyewe ..hili linaonyesha wazi kabisa kuwa hakuna mwenye maamuzi wala vision. watu wanaangalia hio calling mkono kwenda kimyani sijui kinywaniPia Kuna hii Miradi Mbuzi (Uchwara) Inayoendeshwa na Manispaa!! Mfano Huu Mradi unaoendelea wa uwekaji wa Vitofali Vya waenda kwa miguu Katikati ya Jiji, Say Ilala Maeneo ya posta!! Huu ni Ubadhirifu wa Hali ya Juu!! Kazi inafanyika bila Mpangilio wowote!! Jana nimepita maeneo ya British Library Nikamuuliza Msimizi wa kazi Pale, Ndugu yangu hii kazi Unayofanya unamichoro yoyote ambayo inazingatiwa!! Aliloniambia Karibu Nizimie!! Alinieleza Ndugu Yangu Tunafanya ili Mkono Uende Kinywani Kwani Michoro ina umuhimu gani?
Hapo hapo nikagundua huu ni Ufujaji wa hali ya juu wa Kodi Zetu!!
!
Tutatunga Hata sheria Mia Tano na Ushee Ila kama Hamna Msimamiaji Hakuna chochote Tutakachoambulia!! Suala sio Kutunga sheria!! Hapa suala ni nani anayeweza Kusimamia hata Hiyo Sheria mbovu Iliyopo? Jibu Ni hakuna!! Sasa kwa nini tupoteze Muda kutunga hizo sheria?Pasco,
Naona umemvalue sana jamaa na then mwishoni mwa thread yako ukadevalue jamaa yako Slaa
Nikirudi kwenye mada inawezekana Magufuli yuko right na meya naue ana sehem yake yuko right; Sheria ya barabara ilitungwa na inagovern barabara zote ambazo zinasimamiwa na mamlaka inayohusika na barabara Sheria imeweka na kupanga aina mbalimbali za barabara na ukubwa wake na nini umbali kutoka makzi au biashara yoyote magufuli yuko sawa kusimamia sheria mama inayotamka ni kitu gani kinapaswa au hakipaswi kuwepo kwenye barabara husika.
Meya kwa upande wake anasimamia na ana halmashauri yake ya Minispaa ya Ilala ambayo nayo kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa ina mamlaka yake ya kutunga bylaws ambazo zinatawala masuala yote ya uendeshaji wa manispaa yake na masuala ya biashara na utendaji wa kila siku wa Manispaa.
Kwa mujibu wa sheria inapotungwa sheria mama kwa mfano hiyo sheria ya barabara mamlaka za miji au manispaa au jiji zinatakiwa zihakikishe kuwa by laws zao haziendi kinyume na sheria mama na kama kuna kipengele chochote ambacho kinapingana na sheria mama jiji au manispaa au mamlaka za miji zinatakiwa kuziorekebisha sheria zao hatraka sana.
Kinachofanyika hapa inaonekana toka sheria hii inayohusiana na barabara itungwe bado mamlaka za majiji au manispaa kama ya Jerry hawajarekebisha bylaws zao hapo ni kwamba zinaenda kinyume na sheria mama na hapo kisheria ni kwamba by laws yoyote inayopingana na sheria mama ni void