WanaJF,
Wakati mwingine tuwe na kiasi katika kumlaumu ama kumpongwza mtu, naomba niwakumbushe kwamba system ya nchi hii ni ngumu sana na zaidi ni nyimi sana. Kuna wakati chadema walitamka kutokutambua matokeo yaliyompa urais JK na kwa maana ingine kutomtambua kabisa rais. Lakini mwisho wake ni JK yuleyule ndio mwenye final say hata kwenye kuweka mapesa kwenye mifuko ya maendeleo ya majimbo chini ya wabunge wote.
Silaa sikutegemea atafanya lolote la kushangaza ikiwa huko nyuma hakuna chochote kilichofanyika cha maana sana. Anashindwa kufanya mambo mengi kwa sababu nguvu yake haishindi system ma mkae mkijua ccm iko makini kuwakwamisha chadema katika kila jambo. Aibu tuliyovuna ya chadema kwenda ikulu kumshauri mtu wasiyemtambua inatosha kuonyesha kwamba Silaa hana cha kufanya hata awe anashinda vijiweni kwa sie akina choka mbaya.
Ndio nasema ni afadhali katiba yetu mpya, kama ni kweli itaandikwa, ipunguze madaraka ya rais ili pawepo na universal balance. Kama tutapoteza muda kutaka kujua Silaa kafanya nini kwa mwaka mmoja tu ihali hata serikali haiwezi kulipa mishahara kwa watumishi wake tutakuwa tutakuwa ni wavivu wa kufanya tafiti na kutoa mijadala.
Siku zote, hatutaweza kumpima mtu utendaji wake kwa kumvizia ama kumlinganisha na mwenzake, tunampima mtu kulingana na mipango mkakati yake na hali halisi. Hapa JF nishaona sana watu wanaanza kupoteza sifa ya u great thinkera na badala yake gossips zimekuwa ni sehemu ya mijadala yetu, tuwe wakweli, kama Silaa anauza sura basi ni sawa mwacheni auze sura kwani nyie mlikuwa wapi kumhoji wakati mnamchagua? Ama niulize hili, mlikuwa wapi kumdodosa kabla ya kukmasim madaraka hayo makubwa.
Mwisho napenda kuwashukuru wote mliochangia thread hii, na ni wakati huu sasa ambapo naitisha wote msitishe kuchangia kwa kuwa hakuna hoja nziti za kumlaumu mtu ndani ya mwaka mmoja. Kama mtu ataendelea kuchangia hoja hii ni sawa kwa kuwa katiba inaruhusu mawazo binafsi yasiyovunja sheria.
Nawatakia mwaka mpya wenye baraka na mafanikio, na kwa Silaa, nakuomba punguza kwenda kwenye kumbi za starehe na gari la umma wakati usio wa kazi, gari hilo ni nyenzo kwako katikz kufanyz kazi zako rasmi za umeya na sio mara Double Tree, mara mlimani city, mara rose garden, babu unajishushia.
Ni mimi,
Pangu Pakavu,
Nawasalimia.