Jerry Muro, wapi alipo?

Kijana huyu ni mfano wa kuigwa wa waandishi bora. Hakuna wa kuingia kwenye anga zake. Mungu amsaidie.
 
@ Aine, Rosemarie, Paul Kijoka

Jamaa alikua anao uwezo kwa kukufanya umsikilize, Sio Muoga na Mwenye Kujaribu, Lengo lake Halikuwa baya ila lilikua kukomesha tabia ya Polisi, but badala ya polisi kumlinda wanamtoa kafara, lakini ipo SIKU
 
I used to enjoy alivokuwaga anareport, na tatizo ni watu kutokubali makosa na kudhani kwamba wanaingiliwa, Kikubwa ni kwamba wanafanya kama kumkomoa, WAPI UHURU WA VYOMBO VYA HABARI, Nini kosa la kijana wa Watu!??

suluhisho hapa ni Jerry Muro avae magwanda ...period
 
Yupo kitaa kachoka kweli kesi yake ni tar 17 may wasiwasi wangu wasijemfunga kimasikhara masikhara na hawa mafisadi
 
ishu ya jerry inasikitisha sana me najua alikuwa anafanya kazi kwa nafasi yake,hao mafisadi papa hata raisi amewashindwa jerry ndo angewaweza,alafu wakati mwingine hizi rushwa ndogo ndogo zinatuafect direct wananchi wa chini simaanishi kuwa zile kubwa hazituafect but hizi ndogo zinaweza kukufanya upoteze maisha au matatizo ya moja kwa moja.jerry ni shujaa bwana
 
Aliwekewa mtego ila jery ni kijana mzuri muandishi mzuri wa siku za usoni sema kapata ajali,tumuombee arudi azidi kutuhabarisha
 
Jery bonge la handsome,alijitahidi kwenye kazi zake

Hivi watu wakiambiwa mahandsome wapite mbele jerry nae atakwenda!!! Mmhh, sasa itabidi nielimishwe upya maana ya neno handsome. Tatizo la huyo dogo ni ulimbukeni wa umaarufu! Alitaka apande chat kwa kutumia sensitive issues ambazo yeye alidhani ni za kawaida. Mimi simwombei mabaya lakini hilo liwe funzo kwake kwamba pamoja uhuru wa habari bado hekima na busara vinahitajika katika kuamua habari gani iwe aired na kwa namna gani au habari gani isubiri muda mwafaka au habari gani isitangazwe kabisa.
 
Alifukuzisha kazi maafande wa barabarani waliokuwa wanapokea elf 2, 2. Hapo ndipo ukweli wa methali ya mficha maradhi kifo humuumbua unapojidhihirisha. Alitangaza maradhi ya wenzie kumbe yake makubwa zaidi.
 
Nampenda Jerry Muro ni shujaa wetu wanyonge. Yahu atamwinua hata kama Watu waovu wanamwangamiza. Jerry Upaterehema. Kumbuka Hakuna raha inayokuja bila kusota kidogo. Mkumbuke YUsuf Ktk Biblia alisota miaka 12 kwa hiyana ya mke mzinzi lakini baadaye alipeta. Jipe nguvu. Nasikitika kila nikimwona kiingia Kizimbani

Wewe usimfananishe Jerry Muro na Yusuph....Kwa muelekeo wa ile kesi huyu jamaa alijaribu kweli kuomba mlungula no way out...
 
Mkuu sana Sekulu...kichwa cha habari hukumtendea haki Muro! ... Kwa Tanzania hii kwanini usiwe aware kwamba yaliyomfika huyu bwana yanaweza kukufika nawe mkuu?..
 
Back
Top Bottom