Jerry Muro: TEF ni kikundi cha watu wanne

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,424
JUKWAA LA WAHARIRI NI ZAIDI YA ULIJUAVYO

Leo nimeona niseme HADHARANI, japo najua ntapingwa na KIKUNDI cha wachache ila WALIO wengi watanielewa, NATAKA kusema nikijuacho kuhusu JUKWAA LA WAHARIRI, na nataka kusema HADHARANI na niko TAYARI kufikishwa Mahakamani kwa kusema ukweli.

Kwanza nijenge msingi wa HOJA yangu mapema hapa kwa kusema wazi kuwa TEF kama jukwaa la Wahariri halina TATIZO kabisa, tatizo ni baadhi ya Aina ya Viongozi walioko TEF ambao tayari Tunajua ITIKADI na MRENGO wao, wako baadhi ambao hawana kazi za kufanya hivi sasa na Tunajua wanategemea TEF kuendesha maisha yao, tofauti na zamani wakiwa Wahariri,

Wako baadhi wameamua kwa makusudi kufanya TEF jukwaa la baadhi ya vyama vya siasa kwa kuwa nao ni wanufaika wakubwa wa hivyo vyama, pia wako baadhi ya viongozi wa TEF ambao ni "MAKUHADI" wa wafanyabiashara na baadhi ya wanasiasa, Hapa ndio naweka Jiwe la Msingi, sasa tuendelee.

Nyuma ya JUKWAA la wahariri kuna kikundi cha watu wachache hawazidi watu wanne, Natamani kutaja majina yao lakini Roho Mtakatifu ananikumbusha kuwa na HEKIMA katika hili,

Hawa watu wanne walianzisha "KIKUNDI " hiki ambacho kinaitwa Jukwaa la Wahariri (TEF) ambalo Leo NAKIRI hadharani kulifananisha jukwaa hili Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) na kujivisha Majukumu ya kuwasemea, na kuwatetea waandishi pamoja na kulinda maslahi yao mapana jambo ambalo kwangu mimi halikuwa tatizo.

Tatizo na Mashaka limekuja pale ambapo BAADHI ya waasisi wa kikundi hiki WALIPOAMUA kwa maslahi yao kulitumia Jukwaa kwa FAIDA ZAO BINAFSI.

Ujio wa Jukwaa hili, ulisababisha kuziondoa katika chati baadhi ya Taasisi zilizokuwa na Nguvu kisheria katika kusimamia na kutetea maslahi ya waandishi wa Habari nchini mfano Vyama vya Waandishi wa Habari, na Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari nchini,

Hizi taasisi zipo NAKIRI ila hazifanyi KAZI ipasavyo kutokana na KUMEZWA na jukwaa la Wahariri, Mimi naujua UKWELI wa hili na hata baadhi ya Viongozi wa hizi Taasisi wamekiri kuwa Uwepo wa Jukwaa la Wahariri umefiisha Juhudi zao za kazi, kwasababu ya Ushawishi na Nguvu ya baadhi ya Wahariri waliokuwa kwenye Jukwaa la wahariri kutumia vibaya uhariri wao kuwa Karibu NA baadhi ya viongozi wa KISIASA kwa maslahi binafsi,

Kama wanabisha Naomba niwakumbushe wahariri waliokuwa sehemu ya Kikundi cha wana mtandao ndani ya Chama fulani zamani kidogo, pia niwakumbushe katika uchaguzi Mkuu uliopita 2015 tuliona baadhi ya Wahariri wakiwa PR agents wa wagombea wa Urais.

Hii DHAMBI walioifanya baadhi ya Wahariri ambao wako katika jukwaa la Wahariri imesababisha LAANA katika Tasnia Nzima ya Habari nchini, laaana ambayo sasa inaendelea kuwatafuna kwa kuondoa Umoja miongoni mwa, na kuwaaibisha MBELE ya Umma wa watanzania., Haya ni matunda ya LAANA na mkicheza laana inatabia ya kuzunguka mpaka vizazi vya nne Yaani watoto wenu, wajukuu na vitukuu na vilembwe katika tasnia ya Habari.

TUKIO LA TEF NA MAKONDA
Tangu kutokea kwa sintofahamu Kati ya Makonda na Clouds Media Niliona HARAKATI za TEF, na nakumbuka niliingia kwenye mgogoro Mkubwa wa kurushiana maneno na kaka yangu DEODATUS BALILE makamu mwenyekiti wa TEF kwa hatua walizochukua awali pasipo kufanya uchunguzi wa kilichotokea, nikapaza sauti sana kumwambia BALILE wawe watulivu wasikurupuke, nikaishia kutukanwa matusi ya nguoni na kuambiwa niko Upande wa Makonda,

NADHANI SASA UMMA WA WATANZANIA UMEONA HEKIMA YANGU NA YA BALILE KUPITIA TUKIO LA MKUTANO WAO WA JANA NA MKUU WA MKOA, AMEPATA AIBU KUBWA SANA AMBAYO KAMA ANGENISIKILIZA WAKATI ULE LEO ANGEKUWA SHUJAA.

TEF walichukia sana kwa mtazamo wao Tasnia ya Habari kuchezewa, PASIPO KUJUA NANI KAICHEZEA. Wakamkoromea sana Makonda, Wakamshitaki Makonda , Wakamhukumu Makonda kutokana na kumkuta na hatia. Wakamwadhibu Makonda.

Cha Kushangaza TEF wenyewe tena WAKAANZA kuangaika kumtafuta Makonda, nadhani hii ni HUENDA Baada ya kuona MBUYU Umegoma kutingishika na KUTOA Chapaa Nani anajua hili zaidi ya miyoyo yao tu, mana wahenga wanasema Siri ya mtu ni kichaka.

Makonda akawakaribisha wakazungumza na baada ya MAKUBALIANO wakaandaa Mkutano wa kuzika tofauti zao, na cha KUSHANGAZA nikamsikia Mzee wangu THEOPHIL MAKUNGA akitangaza kusamehe na KUTENGUA KIFUNGO cha Makonda pasipo hata Makonda KUOMBA RADHI kama wengi walivyotarajia.

Naomba watanzania mnielewe yote HAYA wanafanya wao tef!!!! kushitaki, kuhoji, kusikiliza, kupata na hatia, kuadhibu, kuachia huru NK. (MWIBA UNAPOINGILIA NDIO MWIBA UNAPOTOKEA)

Sitaki KUBEZA kila walichokifanya TEF, natambua kuna kazi NDOGO nzuri ambazo TEF imezifanya wanstahili KONGOLE katika madogo yao waliyoyafanya Mazuri, ila TEF imefanya MABAYA mengi sana kuliko Madogo Mazuri.

KUHUSU MAKONDA
Makonda kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Yako Mazuri mengi ameyafanya kama kiongozi wa Mkoa, na pia kuna changamoto amekutana nazo kama Kiongozi wa Mkoa, na moja wapo ni hili la Clouds,

Nilishasema na Naomba nirudie kuna suala la Makonda na Ruge kama marafiki, na pia kuna suala la Mkoa wa Dar es Salaam na Clouds media kama taasisi na WOTE Tunajua ni kutokana na MAHUSIANO MAZURI ya awali ndio Yaliziunganisha hizi taasisi mbili Yaani Mkoa wa Dar es Salaam na Clouds Media kufanya kazi kwa ukaribu zaidi, na ni ukaribu huu ambao ulisababisha mpaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuweka vifaa vyake vya kazi Clouds Media,

Naomba niseme kama palikuwa na changamoto ilikuwa ni changamoto NDOGO SANA kiutendaji ambayo Haikupaswa kutendewa hivi ilivyotendewa na wahusika wote wawili pamoja na WAPAMBE WAO, mana hawa watu wawili na hizi taasisi mbili zinahitajiana katika utendaji wa kazi, na wanahitajiana katika maisha,

Na ndio maana Mhe Rais, Dkt John Pombe Magufuli aliliona hili yeye MWENYEWE na kuamua KULIMALIZA, YEYE ALIJUA TATIZO LIKO WAPI NDIO MANA ALILIMALIZA KWA KUWAAMBIA PENDANENI NA NENDENI MKAWATUMIKIE WANANCHI, NA AKASEMA ANAWAPENDA WOTE.

NAOMBA NIWAULIZE TEF?
1. Hivi Mheshimiwa Rais aliwambia kina Makonda na Ruge nendeni MKAOMBANE RADHI?

RUGE MUTAHABA
Jana nilimsikiliza na kumuelewa sana RUGE, nanukuu maneno ya Mwandishi Mwenzangu hapa "Ruge Alikidhi tarajio langu binafsi, aliheshimu nafasi ya TEF katika kuondokana na kadhia iliyokuwapo na kwa namna ya pekee akitambua namna Rais JPM alivyojishusha, akamtambua, akamuita mtu asiyekuwa na hata nafasi ya uongozi katika serikali ya kitongoji na kuagiza apatane na Msaidizi wake, RC Makonda, Ruge anastahili pongezi.

KWENU TEF
Nadhani wakati Umefika kwa TEF kuanza kuuelimisha umma kuwa TEF ni sehemu tu ya wanahabari nchini, lakini si wanahabari wote ni TEF.

Kama kuna yoyote nimekwaza katika hili, natanguliza RADHI.

Imeandikwa na
Jerry C. Muro
Mwandishi wa Habari
10/08/2017
 
"Makonda kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Yako Mazuri mengi ameyafanya kama kiongozi wa Mkoa, na pia kuna changamoto amekutana nazo kama Kiongozi wa Mkoa, na moja wapo ni hili la Clouds"
Hii ni changamoto au ni kosa alilolifanya bro kufifisha kosa nalo ni kosa.
 
Balile huwa anajipambanua kama mtu makini ndiyo maana wengine tulisema mapema kabisa kwamba kukubali kutumika kutamfanya adhalilike tu. Kiko wapi?

ILA waandishi wa bongo mna njaa sana.

Sahara media ilipofugiwa na TRA wafanyakazi walienda mahakamani wakidai hawajalipwa miezi sita lakini baada ya SMG kufunguliwa tena wote wamerudi kazini. Ina maana mmelipwa madai yenu? Mnaishije kama siyo kwa kuuza utu wenu kama hivyo?
 
Nimependa aya ya pili kutoka mwisho kuwa si kila mzungu unaemuona ni padri au sio kila alievaa koti jeupe ni daktari wengine ni wauza nyama.

Na ndio maana hao TEF wapo lakini star tv iliendelea kumuonyesha bashite ulihali sifuri huyu alushapigwa ban na vyombo vyote vya habari
 
Umeandikwa ukweli mtupu.

Nyie viongozi wa TEF acheni njaa zenu na mfanye kile kilichokusudiwa mwanzo kufanywa na TEF.

Zama zimebadilika,tumewabaini kifuatacho mtajiharibia.

Hapa Kazi tu ujanja ujanja wa kutumika ushaexpire,MTAUMIA.
 
Huyu naona amekuja kumtetea makonda sema anazunguka mbuyu anaogopa RAIA wataliamsha dude
Muro we tushakujua. Tulikupima hekima zako ukiwa yanga

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Back
Top Bottom