Jerry Muro awaanika askari kwa rushwa, nini kitatokea?

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Kipindi kinaendelea TBC1, amewaonyesha 'live' askari wa Makambako - Iringa wanavyochukua rushwa na akasema hiyo ni awamu ya kwanza na watanzania wasubiri awamu ya pili, akiendelea kuwaanika wanaofanya hivi, je watamwacha aendelee kuwaumbua?

Safi sana Jerry!
 
Ebanaeee msemaji wa polisi Kamanda Abdallah Msika anaonekana kakerwa sana na video hizi. Hatua zitakazochukuliwa kwakuwa wahusika wameonekana sura huenda zikawa kali sana. Safi sana hii.

Sasa, msikose version ya usiku. Leo kaonyesha version ya rushwa wakati wa mchana
 
ndugu jerry ni great man toka alipokuwa
tatizo moja amekuwa akiwatangaza hivi mapolisi traffic hakuna
kinachofanyika,unafikiri mwema,kombe ,msika awajui
matraffi wamenunua magai yao ndio vituo vya polisi
njoo kawe kona ya kuingilia wanapaki suzuki zao ama
toyota premio,ukikamatwa unakwenda uko unawalipa
sasa kama wameruhusu askari kupaki gari zao pembeni
na watu kulipia nadani ya magari yao unafikiri matraffic wajinga
wanajua wanachofanya na nina wasiwaasi mwingi wakuubwa huko
juu watakuwa wakipokea cha kila siku,....rushwa aishi tanzania hata siku moja atuko sirias,,,msika anajua hili aje na lingine
 
yani kitakachofata ni madereva kulima faini kwa kwenda mbele au wataupdate staili mpya ya kuchukua rushwa baada ya hii ya jerry murro kuonekane used sana
 
safi...Nirahisi kuwa nasa Police wa barabarani..wanatia aibu...mimi binafsi nina uzoefu...achan na hao wapo police wa ajabu ipo siku tuta waletea ushaidi... Police hovyo....
 
Hiv hiki si kile cha ITV alirusha huko nyuma alipokuwa mwajiriwa wa ITV au ni kipya karekodi tena?? Na ninakumbuka IGP Said Mwema aliwafukuza kazi wale askari waliohisika kipindi kile.
 
kijana atatafutwa huyo kama ana gari ndo itakuwa kasheshe...kioo kikiwa na ufa kidogo ..faini ...Side mirror zimewekwa upande faini ..
kazi buti Jerry
 
Hiv hiki si kile cha ITV alirusha huko nyuma alipokuwa mwajiriwa wa ITV au ni kipya karekodi tena?? Na ninakumbuka IGP Said Mwema aliwafukuza kazi wale askari waliohisika kipindi kile.

Hiki ni kipya matukio haya aliyachukua tarehe 08.01.2010
 
Nasikia trafic ni lazima wapeleke faini za makosa saba kila siku, vinginevyo kazi huna, je ni halali hjeshi la polisi kila mwaka waseme tumefanikiwa kupata sh.....................kama faini ya makosa barabarani? badala ya kusema tumefanikiwa kuwaelimisha wenye magari kutokufanya kosa fulani. Pendekezo langu ni, kuondoa faini kabisa
 
Kipindi kinaendelea TBC1, amewaonyesha 'live' askari wa Makambako - Iringa wanavyochukua rushwa na akasema hiyo ni awamu ya kwanza na watanzania wasubiri awamu ya pili, akiendelea kuwaanika wanaofanya hivi, je watamwacha aendelee kuwaumbua?

Safi sana Jerry!
DAH!
naulilia mji wangu niliokulia.......!lolz
ngoja nikomae nichukue jimbo lile
 
Nasikia askari 11 tayari wamesulubiwa, na hiyo ilikuwa phase I. Phase II ikoje?

Ni kweli katika maamuzi ya kizimamoto, mkuu wa jeshi la polisi amewasimamisha kazi hao askari 11. Hivi hata mwaka haujapita, hao traffic wametumia style ile ile kama waliyotumia askari wa Kibaha, inawezekana kabisa hakuna hata ofisa mmoja wa ngazi ya juu anayajua haya mpaka aje Jerry Muro kuonyesha?
 
Acha wale moto,walikuwa wamefikia pabaya walikuwa wanataka rushwa kwa nguvu,mie kuna siku alinichomolea ufunguo kwenye gari kisa handbreak za gari niliyokuwa nayo hazifanyi kazi vizuri!!!
 
Iko hivi mkuu Mzawa Halisi:

Hizi issue za rushwa zinajulikana mpaka zinafanyikaje. PCCB ukiwauliza wanaweza kukwambia kesi kama hizo wanafahamu na wamefanyia utafiti siku nyingi na walishawasilisha mbele ili zifanyiwe kazi.

Si za polisi tu, hata scandal kubwa tu.

Kwanini iwe maamuzi ya zimamoto?

It went public!

Ikishaenda public na wananchi wakaona na wakaona serikali haichukui maamuzi basi maanake serikali hiyo ni "MFU" na ukizingatia huu ni mwaka 'muhimu' kwao basi wanaweza kuharibu kila sehemu.

Naamini unaweza kuuliza mbona maamuzi kama haya yasichukuliwe kwenye kesi kubwa, videos za scandals kubwa hizi zipo, wakizihitaji wanapewa; zikipelekwa kwenye vituo vya Televisheni vyetu hakuna hata kimoja kitakubali kuonyesha! Kila mmoja anaangalia 'maslahi yake ya biashara' na wengine 'maslahi ya wakubwa'. Basi inakuwa ngumu sana. Tunabaki kukabana na vijidagaa hivi (traffic) na polisi wanaokula rushwa za elfu 10 mpaka laki 1 etc wakati mijamaa inayokula rushwa inayoweza kujenga Hospitali ya kuhudumia taifa zima inatesa mtaani na ndugu zetu wanaangamia tukiwaangalia.

Ngumu kueleza...
 
Acha wale moto,walikuwa wamefikia pabaya walikuwa wanataka rushwa kwa nguvu,mie kuna siku alinichomolea ufunguo kwenye gari kisa handbreak za gari niliyokuwa nayo hazifanyi kazi vizuri!!!
Hiyo kali; huyo alikuwa na njaa. Ungemwambia aombe hela ya chai kuliko kutumia visingizio vya kipuuzi hivyo. Kama aliingia ndani ya gari ungewasha gari na kuondoka nae ukiwa ume-lock gari kabisa
 
Back
Top Bottom