Jerry Muro apokewa kwa shangwe na BAVICHA

Jerry Muro apokewa kwa shangwe na BAVICHA

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa zamani wa TBC, Jerry Muro ( kushoto) akito salamu zake kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji cha Bavicha Taifa iliyoketi Mjini Morogoro kuanzia Septemba 14 hadi 18, mwaka huu.

Kiongozi wa vijana nchini kupitia chama kikuu cha upinzani -CHADEMA John Heche , Septemba 17, 2012 alifungua Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichohudhuriwa na wajumbe kadhaa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kikao hicho kilipanga kujadili ajenda mbalimbali za Vijana na baadaye kufikia kutoa tamko la pampoja kuhusiana na masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Hata hivyo katika Kikao hicho , Bavicha kupitia Mwenyekiti wake wa Taifa , walimkaribisha Mwandishi wa Habari na Mtangazani wa zamani wa TBC, Jerry Muro ili aweze kuwasalimia wa wajumbe wa Baraza hilo walioanza kukutana tangu Septamba 14 hadi 18, mwaka huu.

Katika salaamu zake , Muro alisema, yenye ni mwanaharakati na mtu anayependa kusema ukweli, hivyo kwake mtu kama huyo ni lazima amuunge mkono kama ilivyo kwa vijana wa Bavicha wanavyosimamia kusema ukweli na kuamua kuwaunga mkono.

Jerry Muro muda wote alikuwa akizungumza kwa hisia kali huku akishangiliwa kwa shangwe kuu na vijana hao wa BAVICHA
 
He he bado anaogopa kuweka wazi....karibu kaka Ndesamburo anatafuta wa kumuachia jimbo.
 
Haya siku akija kuwakosoa CDM kwa chochote atakuwa kilaza maana nyinyi CDM kwa kushangilia upepo hamjambo.

Walikuwa kina Ulimboka,mara mkawaita wasaliti wanafiki,ngoja na Muro tuone mwisho mtamwita nani?
 
Lini tena? mbona CUF haitajwi ukiwa mwanaharakati na kudai chako basi unaipinga CCM ukiwa TBC basi CCM basi hata ukitoka ch**** ww CCM
 
Karibu kwa vijana wenzio achana na yale MADUWANZI ya MABWEPANDE yatakumaliza!!
 
Hapa mi sioni vijana naona wazee wanajadili mambo ya vijana,kwani umri wa vijana kwa mujibu wa katiba ya CDM ni miaka mingapi?
 
Wote ni vijana ila nyuso zao zimeharibiwa na hali mbaya ya maisha iliyosababishwa na Serikali inayoongozwa na chama cha CCM
Kwani hawana shughuli za kufanya za kuwaingizia kipato? ebu muangalie huyo kijana wa zamani mwenye skafu na huyo bibi bomba mwenye mtandio mweusi meza kuu. Mbona mnapenda kusingizia serikali wakati mambo mengine yako wazi si mkubali tu ni wazee.
 
Hivi unamfahamu Muro au unaropoka tu kama vile umetoka kuota!
 
Aaaa wapi, hao wote wana vyeti vipya vya kuzaliwa halisi vya zamani wamevichoma.Kaka hao wote ni toleo la 1962-1970 ni vijeba kwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom