Mamzalendo na Zogwale nakubaliana na nyie na uchungu wa nchi yetu, tatizo kubwa ni mfumo. Labda mnikosoe kama nimekosea, miaka ya 90, 80 na 2000 ilikuwa ni rahisi kupitisha hoja kwani wabunge walikuwa wa chama kimoja. Sasa hivi mimi na wanaJF tunaongea haya kwa sababu ya technologia ya mawasiliano imetupa uwezo wa kuchangia mengi. Mfano hela za NSSF ni za wanachama, nani anawakilisha wanachama kwenye maamuzi ya miradi kama hiyo? hakuna hata mmoja ni sijui directors wanaoteuliwa na Rais (tena wengi wa kwa kujuana na wanaua kabisa mashirika ya umma aliyoacha mwalimu). Sasa hivi tuna chances kubwa za kutumia bunge kwa kuwa kuna wapinzani na sisi pia humu kwenye forums na forums nyingine tunasikika ingawa hatupo huko. Projects kama hizo ziletwe bungeni, jamani tunataka kufanya mradi huu kwa pesa za NSSF italeta faida hii na hii na wastaafu wetu watakuwa kwenye maisha mazuri kutokana na faida. Project inawekwa mezani inapitiwa na kurekebishwa na kuwa approved, sidhani kama wabunge wote watakuwa mambumbumbu kukubali kila kitu bila ku scrutinize. Tatizo kubwa viongozi wana maslahi yao, hata kama kuna upungufu watakubali tu ifanikiwe hata kuhonga na ikipita kwa Rais yeye ni kuletewa hotuba kusoma na shallow benefits ya mradi kama wa NSSF na simlaumu kwani yeye siyo technical person anategemea aliowachagua kesho tunalalamika Rais alifanya hivi leo lile jengo halina watu au watu wamekataa kufanya biashara hapo basi utasikia jengo limebinafsishwa na mtu analipa pesa ndogo, na watu private wakipata hiyo opportunity wanafanya vitu vya ajabu na kutajirika faster kwani wako creative na innovative nini cha kufanya hapo na wanaangalia faida siyo sisi kupata sifa na kuiba kwenye miradi kama hiyo. Unaweza kuamini serikali inatoa tender labda ya vifaa kama sh. milioni 100 na bidhaa hiyo hiyo inauzwa milioni 40, mfanyabiashara anaondoka ma million 60 faida, gap ni kubwa lakini katikati kuna watu wanakula..nchi imeoza hakuna uzalendo natamani sana capitalism angalau majirani zetu Kenya wanasiasa wana hela zao hata wasipofanya siasa na kuiba ni ngumu kwani kila kitu kiko wazi.