mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,974
Wanabodi,
Natanguliza msamaha kwa wale wote watakaokuwa na tafsiri hasi ya uzi wangu.Ila kama wahenga walivyosema kuuliza si ujinga.Naomba kwa uzi huu,nisitafsiriwe kuwa mimi ni mdini bali ni kutaka kujua tu.
Ukipita pale mkabala na Ikulu ya hapa DSM ambapo kuna ofisi ya Makamu wa Rais,kuna ujenzi unaendelea.Mimi si mtaalamu wa majengo na majenzi,lakini taswira ya jengo inayoibukia na mwonekano wake,umekaa kama msikiti fulani hivi.
Maswali yangu ya msingi ni:Hivi hii ni aina mpya ya ujenzi ambayo pengine serikali yetu SIKIVU imeridhia?,au serikali imeona ni vema ijenge msikiti kwa kuzingatia makamu wetu ni mwislamu,hivyo kidemokrasia kwa kuwa suala la ibada ni muhimu basi familia ya makamu ipate sehemu ya kuabudia?
Nitashukuru kama kuna wajuvi watanielewesha,pengine macho yangu yana matege.
Ahsanteni.