Nilikuwa katika pilika za hapa na pale, nikakutana na vijana wanaongelea juu ya uozo uliomo ndani ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, akawa anawaeleza wenzake kuwa kuna waraka umetolewa na wafanyakazi wa Mahakama ya Rufaa waliochoshwa na uonevu na ubinafsi wa viongozi wao. Kwa bahati nzuri nimeupata waraka huo wenye kurasa 13, nitaupiga picha niuambatanishe kama inawezekana kwa kuwa sina scanner. Kilichonigusa katika waraka huo ni UUZWAJI WA MAHAKAMA YA RUFAA KWA KEMPISKY HOTEL. Nikaelekezwa nimuone engineer wa Mahakama naweza kupata details lkn sijampata ila nilionana na dada mmoja yeye ni Mhasibu pale, nilipomdodosa akaniambia ni kweli na amesikia mpaka michoro ya jengo jipya watakalojengewa Mahakama na huyo mwenye Kempsiky ipo tayari. Na sio kwamba watapewa cash, bali watajengewa jengo wanalotaka wao katika kiwanja chao ( yaani cha mahakama) kilichopo karibu na Gymkana. Tena huyu mdada akaniambia hiyo habari inazimwa then inaanza kwani kuna mkono wa Jaji mkuu mstaafu na Jakaya.
Inasikitisha sana kwa kuwa hili jengo ni la kihistoria na pia mahali lilipo ni very potential kuondolewa kirahisi hivyo. Kuna harufu ya Rushwa kabisa katika hili. Mwenye habari zaidi atujuze na pia wadau wenye uwezo wa kulifuatilia suala hili kwa undani zaidi kazi ni kwenu.