Jengo la Kanisa la KKKT Mbezi Beach lafunguliwa rasmi

Hiyo VIP PARKING ilikuwa kwa siku ile ya ufunguzi rasmi tu mkuu.
Palikuwepo waheshimiwa wakristo na Maaskofu ambao walitengewa sehemu hiyo, nafikiri viongozi hao wanastahili heshima hiyo.

asante sana kwa kunifahamisha..
 
Jengo la Kanisa KKKT Mbezi Beach limefunguliwa leo katika ibada ya jumapili asubuhi.
Kwa sasa hivi jengo hili linaaminika kuwa ndio linashikilia rekodi ya jengo kubwa la kanisa kuliko yote Afrika Mashariki.
Kutokana na habari katika misa hiyo ujenzi wake umetokana na michango wa waumini wenyewe , bila kupata msaada toka nje ya nchi.
Misa iliongozwa na Baba Askofu Malasusa akisaidiwa na Baba Askofu Mushendwa na Baba Askofu Dr Mwakabana.
Waziri Mkuu Mstaafu F Sumaye na Mama Mkapa nao walishiriki misa hiyo.

Mkuu kama unamanisha ni kwa makanisa ya KKKT, inawezekana kwa rekodi zako, lakini kama ni kwa makanisa ya madhehebu mengine, then hiyo comment siyo kweli kabisa, itakubidi utembee uone!
Bwana awabariki wapendwa waliojitoa katika kufanikisha hilo jengo la ibada ... Amen!
 
Kuna sehemu zingine Dar Es Salaam watoto wanakaa chini,hawana madawati.Na hilo kanisa ligharimu zaidi ya mamilioni!Waumini wengi hapa ni elites.!Sishangai baadhi ya pesa ,indirect, ni za taxpayers ,zimechotwa na wafisadi!
 
Hawa watoto wa Mbagala,wangejengewa shule na waumini hawa wa Mbezi Beach,ndio ujumbe wa Kristu,sio majengo ya kifahali.Tanzania sasa Ukristu ni pesa!!!!
Hii ndio hali halisi kule MBAGALA ..na ndio Tanzania ya 2009

enough with mijadala ya ufisadi...hali halisi on the ground ni hii...
maendeleo.jpg

mwanamasalaView Public ProfileSend a private message to mwanamasalaFind all posts by mwanamasalaAdd mwanamasala to Your ContactsGive Away PointsExperience
Points: 84,116, Level: 100
red_left.png
red.png
red_right.png
Level up: 0%, 0 Points needed
grey_left.png
grey.png
grey_right.png
Activity: 12%
green_left.png
green.png
green_right.png
Ranking Shop
 
Kuna sehemu zingine Dar Es Salaam watoto wanakaa chini,hawana madawati.Na hilo kanisa ligharimu zaidi ya mamilioni!Waumini wengi hapa ni elites.!Sishangai baadhi ya pesa ,indirect, ni za taxpayers ,zimechotwa na wafisadi!

Mawazo mgando mkuu!
Remenber the old adage ,charity begins at home.
Na hii ni hatua kubwa sana kwa waTanzania kutotegemea misaada toka nje, na inawezekana.Badala ya kuendeleza fikra finyu ,iga uendelee, kwa vile kwa vyovyote mradi huu umeonyesha mshikamano wa hali ya juu sana mpaka ulipofika.

Katika post yako ya pili nafikiri nina uhakika kuwa penye kuongelewa mchicha wewe unaongelea maembe!
Kwa mantiki ya kawaida kabisa inabidi urudishwe darasa ili ulielewe somo na kulifaulu!!
Watoto hao masikini wewe unajua sababu yao kwa nini wamekaa chini.
Je wewe umefanya nini juu ya hili?
Ni vyema usiwe na mawazo ya Kimachinga wa mitaani kufikiri kuwa maendeleo yataletwa na kundi fulani tu la watu na wewe utabaki kulalamikia "hali ngumu".
Do someting about it!
Mwanamasala sina uhakika kama umekielewa vizuri kilichoko kwenye thread.Inaniwia vigumu kama unayaelewa vizuri mazingira ya thread hii.
Kama ningekuwa mwalimu ningekupeleka shule ya wenye mtindio wa ubongo maana unongelea mambo ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na mtoa thread.
WEWE kama mwanamasala umetoa kiasi gani kuondoa hali hiyo.
Ni vyema usiwe na Machinga Mentality ya kuwa wewe unaweza kufanya chochote bila wewe vile vile kujitoa katika kuchangia kurekebisha hali hiyo.Machinga ni mtu yoyote anayefanya biashara bila leseni wala kulipa kodi kwa udru wa hali ngumu mjini.
Kutoa lawama na kunyooshea vidole kwa mambo mema yaliyo fanyika sihesabu kaka ukomavu wa kifikra.
Jifikirie wewe mwenyewe umefanya nini na si umefanyiwa nini.
Naamini wewe una umeme na una kaa mahali pazuri na ndio maana umeadika maoni yako, je wewe unastahili hayo?
Maana utakuwa unawapunja wale wasio na nyumba wala umeme majumbani kwao, hii ni pamoja na ukweli kuwa mantiki hii kama ulivyo ielezea katika maoni yako ni dalili za mtu aliyekata tamaa ya maisha wakati uwezo anao.
 
Gwakisa umechemsha!vizuri mama Mkapa alihudhuria!Pengine alitoa mchango vilevile.
You know for sure Mama Mkapa ni fisadi papa.Kama kwenda darasani ,nimeshasoma vya kutosha ,ila sina Phd fake!

Kama wewe ni Mkristu,nafikiri usiwe na jazba,nilichokuwa nataka kulinganisha ni kanisa lako na watoto wa Mbagala shuleni.sijui nini kimekuuma
 
Kimtizamo wako inawzekana nimechemsha, lakini ni huo mtizamo wa kuchanganya mchicha na embe.
Ufisadi wa Mama Mkapa wewe ndio unaufahamu vizuri zaidi maana inaelekea unamfahamu hivyo .

Suala la kusoma kwako mkuu lina utata kidogo, usipoweza kupambanua logic si ajabu utasoma sana lakini hutaelimika, in which case you will end up being irrelevant and a nuisence to society.
BADO SWALI LANGU NI WEWE UMEIFANYIA NINI NCHI YAKO!
 
Gwakisa ,sikuelewi!kama unaipenda nchi yako basi usijidai humjui Mama Mkapa na ufisadi wake!Logic also is to reason beyond the acceptables!Kama unaona jengo la kanisa lako ni bora kuliko watoto wa shule Mbagala kupata madawati,it is your right to do so!
Una siasa za Kivukoni,mimi sina hizo.Good luck na jengo la kanisa lako la bilioni shs.
I guess utaingia mbinguni ukisali humo
 
KWA MARA NYINGINE TENA MKUU, UMEIFANTIA NINI NCHI YAKO?
Nchi na wale watoto hawajengwi kwa domo tu, na kwa taarifa yako sehemu ya kanisa si kusali tu bali hata kutatua masuala ya kijamii na ndio maana naona kusoma kwako ba hakujakusaidia wewe kuelimika.
 
perhaps i could ask you the same:What have you done to your country?to contribute building your mega church?
 
Mwanamasala,

..kwanza, wapongeze KKKT kwa moyo wao wa kujitolea na kuchangia ujenzi wa Kanisa zuri kiasi kile.

..pili, wahimize watumie moyo huohuo kuchangia ktk maeneo mengine yenye matatizo kama shule ya Mbagala ambapo watoto hawana madawati.

..naamini kabisa ungefanya hayo mawili ujumbe wako ambao una nia nzuri kabisa ungepokewa vizuri zaidi na watu kama Lole Gwakisa na wengine.

..I dont think it should be a case of either or. inawezekana kujenga Kanisa pamoja na shule.

..pia lazima tuelewe kwamba KKKT inatoa mchango mkubwa sana ktk sekta za Afya, na Elimu, hapa Tanzania.
 
Hongereni sana wenzetu wa Mbezi Beach kwa kanisa zuri hivi, Mungu awabariki sana. Baada ya kuiona picha ukweli nikakumbuka maneno ya Mfalme Yehoshafati katika 2Nyakati 20:8-9, ambapo alikuwa akimkumbusha Mungua "si wewe uliyetuambia tukujengee jengo hili zuri, mahali tutakapoliweka jina lako?. Ili kukiwapo upanga, tauni n.k tukulilie nawe utasikia". Jina la Mungu linastahili kukaa mahali pazuri na penye heshima yake, nanyi mmefanya. Hii ni changamoto kwetu wakristo wote mahali pote tulipo kujipanga na kumjengea Mungu jengo linalostahili heshima yake, mbona majengo yetu tunajitahidi yawe mazuri kwa kadri tunavyoweza!.
Nimeona hili limewakera baadhi ya watu hata kutia wana huruma sana,ikanikumbusha wakati Mariamu akikivunja kibweta cha MARHAMU na kumwagia mafuta haya ghali bwana Yesu miguuni. Kuna waliona ni upotevu wa fedha, kwamba kingeuzwa na kupewa maskini. Mnakumbuka jibu la Bwana Yesu, nasema wala tusichoke kujenga kila tutakapoweza kufanya hivyo. TUNAJENGA MAHALI TUTAKAPOLIWEKA JINA LA MUNGU WETU,ILI KUKIWAPO UPANGA, TAUNI N.K TUTAKWENDA KWAKE NA KUMLILIA NAYE ATASIKIA.
 
Kuna waliona ni upotevu wa fedha, kwamba kingeuzwa na kupewa maskini. Mnakumbuka jibu la Bwana Yesu, nasema wala tusichoke kujenga kila tutakapoweza kufanya hivyo. TUNAJENGA MAHALI TUTAKAPOLIWEKA JINA LA MUNGU WETU,ILI KUKIWAPO UPANGA, TAUNI N.K TUTAKWENDA KWAKE NA KUMLILIA NAYE ATASIKIA.
Ubarikiwe sana mkuu kwa kuliinua jina la Bwana.
 
Jengo la Kanisa KKKT Mbezi Beach limefunguliwa leo katika ibada ya jumapili asubuhi.
Kwa sasa hivi jengo hili linaaminika kuwa ndio linashikilia rekodi ya jengo kubwa la kanisa kuliko yote Afrika Mashariki.
Kutokana na habari katika misa hiyo ujenzi wake umetokana na michango wa waumini wenyewe , bila kupata msaada toka nje ya nchi.
Misa iliongozwa na Baba Askofu Malasusa akisaidiwa na Baba Askofu Mushendwa na Baba Askofu Dr Mwakabana.
Waziri Mkuu Mstaafu F Sumaye na Mama Mkapa nao walishiriki misa hiyo.
Hongereni wana KKKT
 
Back
Top Bottom