Jengo la Kanisa la KKKT Mbezi Beach lafunguliwa rasmi

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Jengo la Kanisa KKKT Mbezi Beach limefunguliwa leo katika ibada ya jumapili asubuhi.
Kwa sasa hivi jengo hili linaaminika kuwa ndio linashikilia rekodi ya jengo kubwa la kanisa kuliko yote Afrika Mashariki.
Kutokana na habari katika misa hiyo ujenzi wake umetokana na michango wa waumini wenyewe , bila kupata msaada toka nje ya nchi.
Misa iliongozwa na Baba Askofu Malasusa akisaidiwa na Baba Askofu Mushendwa na Baba Askofu Dr Mwakabana.
Waziri Mkuu Mstaafu F Sumaye na Mama Mkapa nao walishiriki misa hiyo.
 
picha
 
CIMG0338.JPG

Click on the picture for a larger image
 
Wazungu wengi kila sehemu wanayojenga makazi mapya, basi viwanja vya michezo, majumba ya kufanyia mazoezi na michezo na makanisa yanaanza kujengwa pia.

Tanzania kila sehemu ni Makanisa na Misikiti. Halafu unataka eti siku moja tushinde kwenye kombi la Africa au Olympic.
 
Jengo la Kanisa KKKT Mbezi Beach limefunguliwa leo katika ibada ya jumapili asubuhi.
Kwa sasa hivi jengo hili linaaminika kuwa ndio linashikilia rekodi ya jengo kubwa la kanisa kuliko yote Afrika Mashariki.
Kutokana na habari katika misa hiyo ujenzi wake umetokana na michango wa waumini wenyewe , bila kupata msaada toka nje ya nchi.
Misa iliongozwa na Baba Askofu Malasusa akisaidiwa na Baba Askofu Mushendwa na Baba Askofu Dr Mwakabana.
Waziri Mkuu Mstaafu F Sumaye na Mama Mkapa nao walishiriki misa hiyo.

Je ndio hapo ambapo EL alileta mgogoro?
 
Mungu awabariki wote mlioshiriki kuchangia ujenzi wa hili jengo la kanisa, awajazie zaidi na zaidi pale mlipopunguza. May the Lord bless you abundantly.
 
sasa mimi nawaomba msijekubali kufungisha ndoa za mashoga humo kwenye nyumba ya Mungu, maana hiyo misaada kutoka huko kwa waliobaliki isije ikatubadilisha na kujikuta tunakubai matakwa yao, chonde chonde jamani, tusije haribu desturi zetu ndani ya hizi nyumba za ibada. Mungu awabariki na kulitangaza neno lake sawa sawa na sio kulipotosha ili kuukwepa ukweli. Big up wote mliojenga kanisa hilo
 
Je wachangiaji wakubwa sio wale ambao wanakwepa kulipa kodi kwa serikali? Biblia inasema wazi kuwa lazima ulipe kodi. Lakini kama unadanganya mahesabu halafu hutoi kodi serikalini halafu unakwenda kutangaza kanisani bado hujalibariki kanisa. Nadhani badala ya kujenga makanisa makubwa sana, tujenge mashule halafu tuweke theatre rooms kubwa na siku ya Jumapili tukasalie humo (multipurpose halls).
 
Binafsi nawapongeza sana washarika wa Mbezi Beach kwa kufanikiwa kuhitimisha ujenzi wa nyumba ya Bwana. Na sisi wa Usharika wa Ubungo ndio tupo kwenye mchakato wa kujenga nyumba ya Ibada. Mungu Mwenyenzi atuongoze ili tumalize salama kama tulivyoanza salama.
 
Bila hekima na neno la Mungu kuwepo miongoni mwa jamii hata ujenge mashule na mavyuo tutakuta tuna-train mabumunda na matango tu. Tunahitaji nyumba nzuri za Ibada kwani ndio msingi wa jamii yoyote ile. Na penye hekima ya Mungu kuna mengi mazuri ikiwa ni pamoja na amani na upendo. Kwahiyo nakuomba ukachangie jengo la nyumba ya ibada kwenye Usharika wako wacha kukimbia majukumu kwa vijisingizio vidogo vidogo
 
Jengo la Kanisa KKKT Mbezi Beach limefunguliwa leo katika ibada ya jumapili asubuhi.
Kwa sasa hivi jengo hili linaaminika kuwa ndio linashikilia rekodi ya jengo kubwa la kanisa kuliko yote Afrika Mashariki.
Kutokana na habari katika misa hiyo ujenzi wake umetokana na michango wa waumini wenyewe , bila kupata msaada toka nje ya nchi.
Misa iliongozwa na Baba Askofu Malasusa akisaidiwa na Baba Askofu Mushendwa na Baba Askofu Dr Mwakabana.
Waziri Mkuu Mstaafu F Sumaye na Mama Mkapa nao walishiriki misa hiyo.
Ni Baba Askofu Samsoni Mushemba. Na naamini ni miongoni mwa maaskofu wenye hekima na busara na waliyoiongoza KKKT kwa mafanikio ya hali ya juu. Ila pia niwapongeze maaskofu wote wa KKKT kila mmoja kwa dayosisi yake na Baba Askofu Malasusa kwa kuliweka kanisa katika mahali pa salama. Cha kuwaomba ni kudumisha umoja, upendo na amani pamoja na kufuata ushauri wa Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye kuhusiana na ukabila
 
sasa mimi nawaomba msijekubali kufungisha ndoa za mashoga humo kwenye nyumba ya Mungu, maana hiyo misaada kutoka huko kwa waliobaliki isije ikatubadilisha na kujikuta tunakubai matakwa yao, chonde chonde jamani, tusije haribu desturi zetu ndani ya hizi nyumba za ibada. Mungu awabariki na kulitangaza neno lake sawa sawa na sio kulipotosha ili kuukwepa ukweli. Big up wote mliojenga kanisa hilo

Hilo ni kweli kabisa halina ubishi. Lakini kama tumeweza kujenga kanisa kwa nini tunashindwa kujenga mifereji pembezoni mwa barabara, kuimarisha mfumo wa maji safi na taka, kubadilisha mfumo wa elimu, kujenga hospitali zetu, kuboresha ubora wa huduma za jamii,usawa wa kimaisha kati ya walio mijini na vijijini. Tunajuaje kama hizo pesa zilizotumika kujengea sio hizo tulizoibiwa? Ashakum si Matusi. Wazungu wanajua udhaifu wetu tuimarishe utamaduni aliotuachia baba wa Taifa wa Kujitegemea tuache uvivu na kupiga porojo.
 
Binafsi nawapongeza sana washarika wa Mbezi Beach kwa kufanikiwa kuhitimisha ujenzi wa nyumba ya Bwana. Na sisi wa Usharika wa Ubungo ndio tupo kwenye mchakato wa kujenga nyumba ya Ibada. Mungu Mwenyenzi atuongoze ili tumalize salama kama tulivyoanza salama.

Tumesikia na kuipongeza azma ya wanaUbungo , na muongozwe na Roho yule Mwema.
 
Mungu awbariki washarika wote waliohusika katika kufanikisha ujenzi wa nyumba ya Bwana. Tunaomba mtuombee pia sisi washarika wa sinza ili nasi tuweze kufanikisha ujenzi wetu.
 
naona hapo pichani kuna VIP parking, sikujua kumbe na makanisani kuna VIPs! mimi nilidhani kwenye maswala ya waumini wote ni sawa tu kama viumbe wa Mungu

anyway hongereni sana kwa ujenzi wa kanisa
 
Hiyo VIP PARKING ilikuwa kwa siku ile ya ufunguzi rasmi tu mkuu.
Palikuwepo waheshimiwa wakristo na Maaskofu ambao walitengewa sehemu hiyo, nafikiri viongozi hao wanastahili heshima hiyo.
 
Back
Top Bottom