Jengo la Ibada limeuzwa Kariakoo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jengo la Ibada limeuzwa Kariakoo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Malila, Dec 13, 2009.

 1. M

  Malila JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Jengo la Kanisa la TAG Kariakoo mkabala na s/msingi Uhuru,limeuzwa kwa Mpemba mmoja. Mchungaji wa kanisa hilo alipohojiwa alisema wameuza kwa lengo la kujipanua zaidi. Limeuzwa kwa Tsh 850 milioni. Majengo ya ibada yanapouzwa kwa wafanyabiashara si jambo zuri,hata kama lengo ni kujipanua,basi wangegeuza eneo hilo kuwa kitega uchumi chao kama kanisa. Kuna waumini wengi wataumizwa na uamuzi huu,na la mwisho ni uhakika mdogo wa kupata eneo lingine kariakoo kwa pesa hiyo.

  Si ajabu hela hiyo ikatafunwa kabla ya kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

  source; Mtanzania ya jumapili ya tarehe 6/12/2009.
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Labda walijadili Kanisani kwao na kufikia muafaka wa kuliuza. Makanisa yana viongozi na viongozi wanaongoza watu, na watu ni sisi tulio hapa duniani.

  Mwisho, nafikiri si vema kuweka conclusion kuwa hela za mauzo zitatafunwa bila ya kueleza na/au ambatanisha sababu yakinifu.
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Bwana yesu aliuzwa na msaliti wake yuda kwa vipande 30 sembuse jengo la kanisa! Wauzaji kama ni kweli mimi naona kama wana hatia ya usaliti maana kwa hiyo pesa waliouza huwezipata eneo jingine kariokoo. Hawaoni wenzao Rc,Anglican na Lutheran wakiyatunza maeneo kama hayo mijini kwa ajili ya kumbukumbu kihistoria? Kwa nini hawakuwa na wazo la kujipanua kwa kuongeza eneo na badala yake wawe na wazo la kujitoa na kurudisha majeshi kwenye viwanja visivyopimwa?
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Yesu akasema....
  siku za mwisho watu watakuwa wenye kupenda fedha, na upendo wa wengi utapoa..... mtakapoona chukizo la uharibifu limesimama PATAKATIFU ndipo mjue ule mwishi umefika.!
   
 5. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hao waumini/wafuasi wa kanisa hilo watawanywe kwenye branch nyingine za TAG na hizo hela walizo pata wagaiwe maskini na watoto yatima!
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280


  Dalili za fedha kupotea zinatokana na alivyosema mchungaji wa kanisa hilo kuwa,wanataka kujipanua kwa kununua eneo lingine bila kutaja eneo jipya linauzwa sh ngapi na liko plot gani Kariakoo.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,056
  Trophy Points: 280
  mission yao ya huduma ni nini?
  kama lengo ni kuwavuta wengi kwa Yesu, kwa nini waliuze?
  sidhani kama Kariakoo kuna kanisa lolote la Assemblies of God zaidi ya hilo.
  Naona kama Kristo ameibishwa ki aina fulani vile!!!
   
 8. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mpemba kanunua kanisa kwa ajili ya kujenga eneo la biashara au msikiti? Kwani wameshabadilisha hati juu ya matumizi ya hiyo ardhi au ndiyo yale mabo yetu ya Hovyo hovyo?
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mnastaajabia hilo. Mbona kuna mengisana Ulaya yanageuza kuwa majumba ya starehe au biashara.
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Dec 14, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Waumini wameongezeka na kijikanisa kile ni kidogo tena sana, kuna kelele nyingi mno, ibada haziendi kwa amani, kikao cha baraza la wazee walibariki kuuzwa kwa kanisa lile na waumini wakaunga mkono , kwa pesa hizo zote limepatikana eneo lingine katikati ya mji penye utulivu na pesa ile itaanzishia ujenzi wa nyumba mpya ya BWANA, kanisa si mali ya mtu binafsi , ni nyumba ya bwana.....hizo hadithi zingine kua pesa italiwa so and so, aah sio lengo la kuuzwa hilo eneo.
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ni kweli lengo ni ibada nzuri mahali penye utulivu. Ungekuwa umesoma gazeti lenyewe,ungeona vile Askofu mkuu alivyoulizwa alijibu nini. Pili tahadhali sio lazima itokee. Mchungaji mwenyewe kakili kuwa kuna manung`uniko kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo.

  Ok nadhani tuwaachie wenyewe waumini wa kanisa hilo. Ila kwa maoni yangu si busara kuuza maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ibada,ndo maana ukienda vijijini kuna visehemu vya watu wanaoabudu mizimu na haviguswi vinaheshimika.
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,289
  Likes Received: 22,056
  Trophy Points: 280

  kaka hatuongelei habari za ulaya, tunaongelea habari za kariakoo
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nadhani wazee wa kanisa na waumini walihesabu na kuona pesa ni nyingi na watajenga banda la milioni tano hala yoooote iliyobakia wataitolea maelezo kwamba imefanyika kazi ya Bwana.

  Jamani nyie Mungu anaona na anakaa kimya ktk hekima zake akisubiri siku ya hukumu kuwapasha ukweli wa kila hatua bofyo mnazopiga sasa.

  Kama kanisa lilikuwa dogo na watu wakaongezeka si wangewapunguzia waumini wapya ktk makanisa mengine ya TAG!!!! au huko waendako si mbali na kariakoo ambapo wana waumini kedekede? naomba kujulishwa pls
   
 14. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mchungaji alipoulizwa zaidi amegoma kutoa maelezo. Tukisema kila kinachofanyika Ulaya tukibebe bila kuuliza itakuwa haina maana. Lile eneo lingeachwa ili wale waumini wachache walio karibu na hapo walitumie kwa ibada na huduma mbalimbali.
   
 16. l

  libaba PM Senior Member

  #16
  Dec 14, 2009
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yeye si mwanasiasa kwamba anatumikia umma wa w TZ wote, yeye ni kiongozi wa kiroho na anawajibika moja kwa moja kwa umma wa kanisa. ana haki yakukataa kuhojiwa kwa malengo asiyo yafahamu, taarifa za uuzwaji wa eneo hilo zimekua zikitolewa mara kwa mara kwenye ibada pale UHURU. Kwa waumini wa pale kila mtu anaelewa taratibu zote ambazo mchungaji alizichukua katika kukamilisha mpango huo.
  Hebu tufikiri pamoja kikanissa kile kinabeba watu 150 wqlioketi kwa ibada na sasa wakristo wamefikia 400 kwa mfano, unategemea kuna ibada hapo, sasa busara kuendelea kuminyana humo ama kutafuta eneo jipya ili kuliendeleza kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo vya Wakristo.
  RC wao wanaamuaga kuwanunua majirani wanaowazunguka, kwasababu wanapesa, wamewahi kufanya hivyo pale vingunguti na maeneo kadhaa ambayo yanawabana na kuwafanya kushindwa kufanya maendeleo.
   
 17. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hivi kweli kariakoo nako kuna kanisa? TAG ni lokole type, kariakoo hakuwafai. Tatizo ni hizo pesa tu ila ki uumni nafikiri wana haki ya kufanya hivyo.
   
 18. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  unajua kitakacho wasumbua hao jamaa ni wapi wakajenge hilo kanisa na kweli itakuwa rahisi kwa muumini wa hilo kanisa kulifata lili[po hilo kanisa jipya?
  hapo kwa kweli wamechemsha kama walikuwa wanaona hilo kanisa ni dogo basi angalau wangepageuza kuwa sehemu ya biashara kwa kwenda kuchukua mkopo benk huku wakijenga kanisa lingine
  kwa hiyo fedha na njaa za wachungaji wetu pamoja na wazee wa kanisa akyaMungu tutasikia tu, haya ni kama yale ya Mtikila anapiga kelele mwisho wa siku anaenda kwa RA kuomba fedha za kanisa aibu sana kwa hawa wachungaji
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Alafu wameuza bei chee sana kutokana na position lilipo hii bei ni ndogo sana. Kwa sasa K.Koo mtaa wa Mchikichi au Congo tunazungumzia Bilioni 1.4 sasa kama wamejiuzia bei ya mbuzi hiyo wamekwisha. Nyie subilini mtaona huyo Mpemba nae akaliuza kwa wadau kwa Bilioni na ushee.
   
 20. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #20
  Dec 14, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kabla hawajauza tayari waliishapata eneo jipya la kujenga kanisa lao, hizi habari hutolewa pale kanisani, na kwakweli waumini wengi wameelewa dhamira safi ya zoezi hilo.
   
Loading...