Jenga gorofa moja kwa gharama nafuu

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,323
40,173
Wengi wanaogopa sana kujenga ghorofa wakizani labda mpaka uwe na pesa nyingi ndio ujenge. Ukiamua hakuna kinachoshindikana, kama umeweza kujenga nyumba ya chini,jua una uwezo pia wa kujenga ghorofa. Fanya yafuatayo kutimiza ndoto zako:-
  • Weka kwenye michoro wazo la nyumba yako (jichoree mwenyewe unavyotaka)
  • Tafuta injinia akuandalie BOQ (idadi ya matirio yatakayotumika),michoro, na ramani
  • Tafuta kibali cha ujenzi- itategemea na eneo uliopo
  • Anza kununua mawe, kokoto nyeusi, mchanga, matofari ya kuanzia, nondo. simenti-kwa ajili ya msingi
  • Nenda maeneo yanapojengwa magorofa, na umchukue fundi unayemuona anapiga kazi
  • Ingia makubaliano na huyo fundi-akupatie gharama ya msingi, ikiwezekana mkubaliane kwa siku.
  • Anza kazi ya msingi.
  • Weka rafu/ zege kwenye msingi
  • Anza kupandisha nguzo na tofali kwa awamu awamu kutokana na mzunguko wako wa pesa- unaweza kumtumia yule fundi wa mwanzo au ukatafuta mwingine
  • Ukifika kwenye lenta-inabidi upumzike
  • Anza kukusanya nondo,kokoto nyeusi, simenti,misumari
  • Angalia pa kukodi 'plate' au 'marine board',kwa siku gharama yake huwa ni sh. 400/= kwa moja, pia kukodi mirunda, mbao; inategemea na sehemu ulipo.
  • Mwite fundi kwa kazi ya 'slab'- hapa ndipo huwa pagumu sana kwenye ghorofa
  • Akishamaliza slab, pumzika utafute nguvu
  • Endelea na ujenzi wa juu
  • Paua mjengo wako
  • Endelea na hatua zingine za 'finishing'
  • Baada ya hapo jipongeze....kwa kutembelea mbuga za wanyama
 
Hebu fanya Kama unawapa ushauri walimu,manesi namna ya kujenga ghorofa mkuu.
Kama ana chanzo kimoja cha fedha,inabidi afanye hivi:-
  • Kwanza inabidi ajikatae mwenyewe,awe bahili
  • Asitumie zaidi ya laki 2 kwa mwezi
  • Awe na plan ya kujenga ghorofa isiyozidi mita 10 kwa 8
  • Kama anakiwanja, aanze kukusanya matirio
  • Akifikia kwenye slab, akope benki au chanzo chochote anachokiamini
  • Baada ya hapo aendelee na ujenzi na hatimaye amalize.
Kujenga atajenga, ila tofauti ni kwenye muda wa kumaliza ujenzi; anaweza kutumia miaka hata 6
 
Motivational speakers bana.
Bwana wee yaani anachapa marimba ya mzungu kirahisi ukidhani hiyo slab ni kitu rahisi. Mziki wake ni sawa na kuanza kujenga nyumba nyingine. Nondo na mifuko ya cement inavyoteketea ni noma. Katika ufala niliowahi kufanya maishani ni kujenga nyumba ya ghorofa....yaani ni bora tuu ningezika mamillion ya slab kwenye mbususu
 
Kama ana chanzo kimoja cha fedha,inabidi afanye hivi:-
  • Kwanza inabidi ajikatae mwenyewe,awe bahili
  • Asitumie zaidi ya laki 2 kwa mwezi...
Duh hivi Maisha yao unayafahamu mkuu?Take home yenyewe hawana Ni madeni matupu,Familia inawaangalia etc.Nyumba ya kawaida tu inawashinda wanakuja kujenga kwa pesa za kustaafia.

Karibu mtaani ujionee Hali halisi boss.
 
Bwana wee yaani anachapa marimba ya mzungu kirahisi ukidhani hiyo slab ni kitu rahisi. Mziki wake ni sawa na kuanza kujenga nyumba nyingine. Nondo na mifuko ya cement inavyoteketea ni noma. Katika ufala niliowahi kufanya maishani ni kujenga nyumba ya ghorofa....yaani ni bora tuu ningezika mamillion ya slab kwenye mbususu
Teh teh labda ungempa hesabu zako za kihali halisi ndio angejua mziki hua unakuaje huko field mkuu.
 
Bwana wee yaani anachapa marimba ya mzungu kirahisi ukidhani hiyo slab ni kitu rahisi. Mziki wake ni sawa na kuanza kujenga nyumba nyingine. Nondo na mifuko ya cement inavyoteketea ni noma. Katika ufala niliowahi kufanya maishani ni kujenga nyumba ya ghorofa....yaani ni bora tuu ningezika mamillion ya slab kwenye mbususu
Ni kweli, slab inakula hela sana; ndio maana tunashauri badala ya kununua marine board, kodi 'plate'; Pia ili usipate makali ya gharama kwa wakati mmoja, anza kununua matirio kwanza hata kwa miezi 5, baada ya hapo itafundi kwa kazi.
 
Duh hivi Maisha yao unayafahamu mkuu?Take home yenyewe hawana Ni madeni matupu,Familia inawaangalia etc.Nyumba ya kawaida tu inawashinda wanakuja kujenga kwa pesa za kustaafia.

Karibu mtaani ujionee Hali halisi boss.
Ndio maana nakazia pale,ukiruhusu mfuko wako wa fedha utoboke..utatoboka kweli; kama pato lake 'net' laki 5, atumie laki 3 kwenye ujenzi
 
Ni kweli, slab inakula hela sana; ndio maana tunashauri badala ya kununua marine board, kodi 'plate'; Pia ili usipate makali ya gharama kwa wakati mmoja, anza kununua matirio kwanza hata kwa miezi 5, baada ya hapo itafundi kwa kazi.
Siku mie namwaga slab mifuko 116 ya cement inondoka mbele ya macho yangu ndio nilipojua haya maghorofa yote ni kujijaza upepo tuu unless ni for business.

Bora ujilie mbususu tuu kwenye nyumba yako ya chini ya mil100. Muhimu kuwe na kipupwe vyumba vyote na maji yanatoka kwa presha basi.
 
Back
Top Bottom