Jenga gorofa moja kwa gharama nafuu

View attachment 2977960
Asante mkuu
Idea ni isizidi SQM 50. Kuwe na minsitting room ft 10X8ft, bedroom ft 12Xft 14, dressing room ft 10X ft 6, bathroom ft 5X ft 6, staircase na balcony(au isiwepo kabisa. Pasiwe na mambo mengi. Imagine kitu kama hicho hapo juu
c.c mzabzab
So hapa ni kumaanisha juu una chumba kimoja cha kulala (cha mwenye nyumba) wengine watalala nyumba ya chini ok ni idea nzuri maana mtu unafanya kitu kulingana na uwezo.....ila akina dogo janja wanaweza laumu kimtindo kuwa ah dingi naye kaamua kukaa ghorofani peke yake.....
 
So hapa ni kumaanisha juu una chumba kimoja cha kulala (cha mwenye nyumba) wengine watalala nyumba ya chini ok ni idea nzuri maana mtu unafanya kitu kulingana na uwezo.....ila akina dogo janja wanaweza laumu kimtindo kuwa ah dingi naye kaamua kukaa ghorofani peke yake.....
Ewaaa, dogo janjaaz wasubiri nizeeke nishindwe kupanda ngazi, na hapo labda wajukuu zao ndio walale juu maana wao watakuwa makwao.
Pamoja na kufanya kulingana na uwezo wangu wa kawaida ila napenda sana privacy. Nataka kujitenga na chini nikiwa nafanya kazi zangu, starehe zangu na ujinga wangu mwingine.
Kwa eneo plain 120m inaweza kutosha?
 
Ewaaa, dogo janjaaz wasubiri nizeeke nishindwe kupanda ngazi, na hapo labda wajukuu zao ndio walale juu maana wao watakuwa makwao.
Pamoja na kufanya kulingana na uwezo wangu wa kawaida ila napenda sana privacy. Nataka kujitenga na chini nikiwa nafanya kazi zangu, starehe zangu na ujinga wangu mwingine.
Kwa eneo plain 120m inaweza kutosha?
Naamini itatosha na pengine kubaki maana itategemea material utakayotumia na finishing kwa mfano nondo tani 1 BS 500 kamal steel wanauza 2,450,000 ukiwa na connection nondo kwa mfano kampuni ya MM Steel kwa tani utapata kw TZS 1,750,000 so unaona kabisa hilo gepu la bei japo naamin za kamal steel zina ubora mkubwa.
Nilichojifunza magorofa mengi ujengaji wake hauzingatii viwango kiviiile au yanajengwa kieconomy kwa hiyo hii inapunguza gharama...
Kuna ghorofa jamaa kajenga kwa 50M ila bila finishing juu ina Bedroom 3 balcony mbili, office na hajaweka jamvi dah nilishangaa sana nikaelewa ndo maana maghorofa yanaota kama uyoga.....
maghorofa mengi ya residential/commercial i.e. fremu unakuta wanatumia nondo za mm 12 kwenye nguzo cha ajabu zaidi unakuta zimewekwa pc 4 tu badala angalau ya 6 na kuendelea !
Kuna ghorofa inajengwa masaki now ipo ghorofa ya 3 kuelekea ya 4 nguzo zote imewekwa nondo mm 12....
 
Wengi wanaogopa sana kujenga ghorofa wakizani labda mpaka uwe na pesa nyingi ndio ujenge. Ukiamua hakuna kinachoshindikana, kama umeweza kujenga nyumba ya chini,jua una uwezo pia wa kujenga ghorofa. Fanya yafuatayo kutimiza ndoto zako:-
  • Weka kwenye michoro wazo la nyumba yako (jichoree mwenyewe unavyotaka)
  • Tafuta injinia akuandalie BOQ (idadi ya matirio yatakayotumika),michoro, na ramani
  • Tafuta kibali cha ujenzi- itategemea na eneo uliopo
  • Anza kununua mawe, kokoto nyeusi, mchanga, matofari ya kuanzia, nondo. simenti-kwa ajili ya msingi
  • Nenda maeneo yanapojengwa magorofa, na umchukue fundi unayemuona anapiga kazi
  • Ingia makubaliano na huyo fundi-akupatie gharama ya msingi, ikiwezekana mkubaliane kwa siku.
  • Anza kazi ya msingi.
  • Weka rafu/ zege kwenye msingi
  • Anza kupandisha nguzo na tofali kwa awamu awamu kutokana na mzunguko wako wa pesa- unaweza kumtumia yule fundi wa mwanzo au ukatafuta mwingine
  • Ukifika kwenye lenta-inabidi upumzike
  • Anza kukusanya nondo,kokoto nyeusi, simenti,misumari
  • Angalia pa kukodi 'plate' au 'marine board',kwa siku gharama yake huwa ni sh. 400/= kwa moja, pia kukodi mirunda, mbao; inategemea na sehemu ulipo.
  • Mwite fundi kwa kazi ya 'slab'- hapa ndipo huwa pagumu sana kwenye ghorofa
  • Akishamaliza slab, pumzika utafute nguvu
  • Endelea na ujenzi wa juu
  • Paua mjengo wako
  • Endelea na hatua zingine za 'finishing'
  • Baada ya hapo jipongeze....kwa kutembelea mbuga za wanyama
Mkuu umemaliza kila kitu, hasa hapo kwenye mbuga za wanyama🤣 unapofikia mafanikio ni muhimu kujipongeza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom