PreGE2025 Jenerali Ulimwengu - no reforms no election 2025 wana madai ya msingi

PreGE2025 Jenerali Ulimwengu - no reforms no election 2025 wana madai ya msingi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
15 April 2025

Mwanzo Mwisho Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dk. Nshala Azungumzia Tume, Kesi ya Lissu​


View: https://m.youtube.com/watch?v=4mJ_iKQMpOo

Dk. Rugemeleza Albert Kamuhabwa Nshala mwanasheria mkuu wa CHADEMA akifafanua kipengele, hoja kwa hoja mbinu chafu za kudhoofisha upinzani kwa njia haramu zisizo za kuzingatia katiba ya nchi ili utawala wa CCM ubakie madarakani ...
 
14 Aprili 2025

JENERALI ULIMWENGU - NO REFORMS NO ELECTION 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=DVu9sNRqeXM

Chaguzi za 2019, 2020 na 2024 uvunjaji wa kushangaza wa kuvuruga uchaguzi yalifanyika bila haya, asema Jenerali Ulimwengu.

Serikali inatakiwa iwe na haya isifanye mambo ya aibu kama ya 2019, 2020 na 2024 yaliyotokea wamejivunjia heshima na hii inatupeleka mahali pagumu sana

Wale wanaopinga kuona haya kwa serikali ndiyo wanasulubiwa hii ni jambo la ajabu sana anasisitiza Jenerali Ulimwengu

Naamini kuna wachache ndani ya CCM wanaoipenda nchi yao ambao wanaweza kuwaambia wenzao wasio na haya ndani ya CCM wajirudi ili kunusuru nchi yetu

Nikichuja madai ya wanaodai No Reforms No Election 2025 kuna mambo ya msingi, mfano INEC ipachikwe jina Tume Huru hata ivishwe hirizi ya 'uhuru' ukweli uteuzi wa mwenyekiti wa INEC na wajumbe wake hawawezi kutenda haki kwa wasio CCM

Nimetembea nchi nyingi zilikuwa na wastaarabu kule Sierra Leone, Somalia , Central African Republic walikuwa watu wapole sana ila kulipotokea raia kuchoka uonevu tunaona jinsi nchi hizo zilizokuja kulipuka vurugu ktk nchi hizo

Serikali ya Rais Samia Hassan imedhamiria kuwakamata wapinzani wake wa kisiasa ili wasishiriki uchaguzi. Nchi yetu tayari ina vita vya wenyewe kwa wenyewe mfano watu kupotezwa, kutekwa Mzee Kibao, Deus Soka na wengine wengi ni kiashiria cha vita ya wenyewe kwa wenyewe Tanzania

Tanzania tunaona watu wachache sana wenye sigda kati paji lake la uso huku wanafanya mambo ya haramu kabisa kunyima haki kwa watu wengine.

Uchaguzi unaokuja haona udhu wowote bali una najisi na ni mchezo wa kuigiza. Muda upo wa kuweza kuitisha bunge na kufanya mabadiliko ya sheria na kanuni zinazosimamia mchakato mzima wa uchaguzi amalizia Jenerali Ulimwengu.

....akichaguliwa tena nchi itapata maendeleo......Jk
 
Back
Top Bottom