Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda, Muhoozi Kainerugaba, amesema nchi hiyo ipo tayari kujiingiza katika mgogoro wa Mashariki ya Kati ikiwa kutakuwa na jaribio lolote la kuiangamiza Israel.
Kupitia mtandao wa Machi 25, 2026, Muhoozi alieleza wazi msimamo huo:
"Mazungumzo yoyote ya kuangamiza au kuipiga Israel yatatuingiza vitani (upande wa Israel)."
Hata hivyo, ameongeza kuwa wanatamani vita vinavyoendelea katika eneo hilo vikome haraka:
"Tunataka vita vya Mashariki ya Kati vikome sasa. Dunia imechoshwa navyo."
Mgogoro huo unahusisha United States na Israel dhidi ya Iran pamoja na kundi la Hezbollah, hali inayozidi kuongeza taharuki kimataifa.
Muhoozi, ambaye ni mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amewahi mara kadhaa kutoa kauli zenye utata mtandaoni kuhusu masuala ya kijeshi na siasa za kimataifa, baadhi zikizua mjadala mkubwa kabla ya kufutwa au kufafanuliwa baadaye.
Kauli yake ya hivi karibuni imeongeza mjadala kuhusu nafasi ya Uganda katika siasa za kimataifa na ushiriki wake katika migogoro ya nje ya bara la Afrika.