NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,024
- 2,486
Nimesoma mahojiano baina ya raia mwema na Jenerali mstaafu Tumainieli Kiwelu. Mahojiano ni marefu, nimevutiwa sana uongozi wake katika vita dhidi ya Idd Amin na ukuu wa mkoa baada ya vita. Baada ya vita anasema “..unajua watu walikwishaonja kutoa roho za watu. Huwezi kucheza nao hivi hivi, ikabidi tupangane upya.” Akasema (Nyerere) “sasa wewe bwana umemaliza kazi hii nakushukuru…sasa ninataka kukupa kazi nyingine…nikamwambia sawa, nipo tayari kwa kazi yoyote, akaniambia utakwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Tanga. Nikamwambia naenda lakini hii kazi sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na mimi nikiona kuna tatizo nitakuja”.
Kiwelu Tanga
Akiwa Tanga kama mkuu wa mkoa Jenarali Kiwelu anasema changamoto kubwa kabisa ilikuwa uvivu wa wananchi wa Tanga. “Waswahili wangu wa Tanga ni wavivu, hawakuwa na maendeleo. Sasa walikuwa wanakaa pale kwenye nyumba zao za nyasi mjini, nikawaambia sikilizeni, hatuwezi kuishi hivi..mtu lazima afanye kazi na mjiwekee kipato na mtengeneze nyumba. Wakauliza tutatengenezaje na hatuna mashamba kwa ajili ya kutupatia kipato?” Jenerali Kiwelu akawatafutia mashamba huko Muheza. Akawatafutia mabasi yakawa yanawachukua mjini kwenda shamba na kuwarejesha. Pia akaamuru wapimiwe viwanja vyao ila nyumba zao za nyasi zisibomolewe bali wajenge za matofali kuzunguka zile za nyasi, wakifikia kupaua ndo wabomoe. Kwa hiyo kupitia mkakati huu nyumba za nyasi Tanga mjini na mpango holela ziliondoka na watoto wakasomeshwa kupitia kilimo.
Kiwelu Rukwa
Baada ya kuongoza Tanga kwa miaka mitatu alihamishiwa Rukwa. Huko wananchi wake walikuwa wachapakazi ila walikuwa wakichapa kazi bila utaratibu. Jenerali akaazimia Rukwa walime kwa ajili ya kujipatia kipato badala ya chakula tu. Anasema wakati huo Mbeya, Iringa na Ruvuma ndo ilikuwa ikiongoza kwa uzalishaji wa chakula (the big three), akaazimia mkoa wake uwe wa nne. Ilibidi kuanzisha darasa la wakulima, ambapo wakulima walifundishwa ukulima wa kisasa, kisha akaomba fedha kwa ajili ya mbegu ambapo mbegu walizonunua Kenya hazikutosheleza hivyo akaanzisha shamba la mbegu eneo la Mlundika hivyo upatikanaji a mbegu ukawa endelevu. Ili kutatua changamoto ya pembejeo, walinunua plau kutoka Zimbabwe. Mwaka wa tatu mazao yakawa mengi. “…nia yangu pale ilikuwa kupata mazao mengi ili kushindana na mikoa mingine ya kilimo, na ikibidi hata kuwazidi lakini kwa manufaa ya watu wangu hasa katika kuongeza kipato chao maradufu au zaidi.”
Baada ya hapo alienda Kagera lakini nimependa “legacy” yake katika mikoa aliyopitia. Kumbe umaarufu wa Rukwa katika uzalishaji wa chakula haukutokea hewani. Nimeona kuwa ni kiongozi aliyekuwa mwadilifu, mwenye maono (vision), uthubutu, amri na ushawishi. Pia nimependa pale alipoteuliwa na kusema hakuwahi kufanya kazi ile ila akifanya vibaya aitwe, akishindwa ataomba msaada. Nimeona kuna haja ya kiongozi wa nchi kuelewa huu ukweli kuwa kiongozi anaweza kuwa mzuri sana ila kwa kukosa uzoefu katika eneo husika akachemsha baadhi ya mambo, hivyo kustahili nafasi ya pili na kuelekezwa. Natamani kupata maoni ya “Waswahili wa Tanga” wa enzi za Kiwelu watupe uzoefu wao wakati wanapanda mabasi kupelekwa shamba, mpaka mazao yalipoiva, wakauza na kuweza kujenga na kusomesha watoto. Je, ilikuwa rahisi, hawakunung’unika na wengine hawakukimbia? Mambo ya hiki bure kile bure tuache, tuwezeshe wananchi kugharamia maendeleo yao wenyewe. Waliaji, walalamikaji na wanung’unikaji hawatakosekana lakini kwa weledi, maono na nia ya dhati ya viongozi wetu tutafika.