Jenerali Kiwelu: Nilimnyima Sokoine siri za kijeshi vitani

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
  • Asema katika Vita ya Kegara udhibiti wa mawasiliano na taarifa ulikuwa wa kiwango cha
Raia Mwema: Hali ilikuwaje kule eneo la mapambano wakati wa vita ya Kagera?
Jenerali Kikwelu: Kazi ilikuwa ngumu sana. Maana vijana wangu waliokuwa kule mbele, wale askari wa JWTZ walikuwa katika nusu morali, maana ukishatoka kwenye mstari wa mbele ukarudi nyuma morali ya vita inapungua.

Kwa hiyo kazi ya kwanza ilikuwa kuwajenga kisaikolojia. Kazi ya pili ilikuwa ni kupata reinforcement (kuongeza nguvu) kazi ambayo niliyomwachia Ernest Mwita Kiaro, hata CDF naye alikuja akakaa mahala fulani pale Bukoba (jirani), kwa hiyo Dar es Salaam tulimpa kazi Mwakalindile ndiye aliyekuwa anakaimu kama Chief of Staff, halafu Kiaro, chifu wa mgambo kazi yake ilikuwa kukusanya mgambo wote nchini, akina Mwakalindile ni kukusanya JKT, Polisi na Magareza, wote walikuja kule.

Ninaposema kulikuwa na changamoto kubwa sana ni kwamba hawa askari hata siku moja hawakuwahi kuwa eneo la vita ama eneo la mafunzo ya kivita kwa pamoja. Kwa hiyo, ilikuwa kazi kubwa, ndiyo maana ikatuchukua muda pale kabla hatujaruka daraja, ilikuwa ni lazima nifanye mafunzo ya pamoja ili kuwaweka watu (askari kutoka Magereza, Polisi, Mgambo na JKT) waweze kufanya kazi pamoja.

Lengo ilikuwa kuondoa fikra za kitabaka vitani, kuachana na mambo ya huyu mgambo au JKT. Kwa hiyo nilianzisha range ya kupiga silaha, mtu unampa risasi kumi anapiga zote wash out (anakosa kulenga shabaha), maana sisi (jeshini) tuna kitu kinaitwa bull, inner, outer n.k… sasa huyu unampa risasi zote anapiga wash out, tunampa nyingine, akipiga ile target namwambia umepiga bega (target hasa ni kifuani kwenye moyo au kichwani) sasa wakati mwingine ukimpa risasi tano… mbili anapiga ndani, nikasema sasa wameiva.

Kwa hiyo ilikuwa ni mafunzo ya msingi. Kwa mfano, ukiwa porini na ndege ya adui inakuja ufanye nini.

Unaulizwa ukiona ndege ya adui inatoka kule wewe unakwenda wapi? Namna gani mnaweza kusonga mbele, mnajihami vipi na namna gani mnaweza kupumzika kwa sababu askari hawezi kupumzika chini ya kivuli cha mti. Sasa baada ya mafunzo hayo ya pamoja, tukaridhika askari wetu wameiva, tukaanza kusonga mbele kutoka Katoro hadi tukafika karibu na mpakani, tukaweka kambi ambayo mpaka leo ipo pale, nyuma ya Mtukula.

Raia Mwema: Labda ungeeleza kuhusu Daraja la Kagera kushambuliwa na adui?

Jenerali Kiwelu: Daraja hili wakati nimefika tu, kutoka kupewa ile amri (ya kwenda vitani)… nimefika Kaboya, siku hiyo hiyo jioni nikatoka kwenda kutazama daraja. Nikafika darajani upande wa kulia kama unakwenda Mtukula umbali wa kilomita moja, nikaliona daraja ambalo baada ya dakika 15 nikiwa pale likalipuka, kwa hiyo sikuweza kuwahi kuweka askari pale darajani.

Wakati nafika pale na mtu mmoja anaitwa Kanali Kitete tunatazama…nataka sasa kufanya mbinu namna gani nitavuka daraja ili majeshi yangu yakae upande mwingine.

Basi nikarudi zangu Kaboya kwa ajili ya kuanza kufanya mkakati mwingine maana pale daraja limekwishavunjwa, nikaripoti daraja limevunjwa…hakuna daraja kuanzia sasa. Ndipo tukaanza mipango mingine kuhusu daraja, tukaleta madaraja ya muda na mtu mmoja anaitwa Brigedia Rajabu ndiye aliyekuja na vifaa hivyo kutoka kikosi chetu cha uhandishi na tukamweka sehemu ya umbali wa kama kilomita tano kutoka kwenye daraja, ndipo alipofanya mafunzo yake ili baadaye kufunga daraja la muda.

Raia Mwema: Ilichukua muda gani hadi kufanikisha daraja hilo la muda?

Jenerali Kiwelu: Unajua kuna wanazungumza kwa ushabiki mambo ya vita tu wakati hawajui chochote kuhusu vita, watu hawa mimi nawaita majitu, hawajui maana ya vita. Wapo wengine wanafikiri jeshi hii la Tanzania lilikuwa tayari kwamba unakwenda tu kwenye vita, sasa ukiwaambia kwamba jeshi hili tulipokwenda kwenye vita tulikuwa na mchanganiyo wa watu wote hawa, halafu pia kuleta vifaa vya kuvuka daraja, kuwafundisha namna ya kuweka daraja, kuleta vifaru, ndipo wataona ugumu wa kazi iliyokuwapo.

Pale ni lazima uwe na nguvu ya kutosha kuhakikisha kwamba mkiruka (daraja) hakuna kurudishwa nyuma. Kama nilivyotangulia kusema wale askari wetu waliokuwa kule awali, walikuwa wachache na walivurumishwa na adui kiasi cha morali yao kuwa chini kivita, kwa hiyo ilikuwa ni lazima nihakikishe sasa watu wangu ni imara, vifaa viko.

Tulikuwa tunafanya mipango na ukaguzi pamoja na makamanda wangu, akina Jenerali Marwa, Jenerali Luhanga, Mayunga, Walden… tunakwenda hadi tunafika pale kwenye daraja kwa sababu Idi Amin alirudisha majeshi yake (Uganda) akiamini kazi imekwisha. Sasa tulikuwa na makamanda wangu hao tunakwenda pale kupanga mikakati, lakini, swali kwamba wapi tupite (kuvuka daraja) na lini sikuwaambia.

Hakuna mtu aliyejua hata Edward Sokoine (aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Mwalimu Nyerere) alikuja akaniuliza …. sasa General nafikiri tumechelewa sana kuruka (daraja), sasa unaruka lini na unapitia wapi?

Nikamwambia hiyo ni siri ya kijeshi… akasema hata mimi? Nikamwambia ndiyo mzee. Kwa hiyo mimi nilikuwa napita kando ya ule mto kwa gari hadi Murongo, halafu watu wanapiga mabomu kila sehemu lakini hawajui tunaruka wapi kupitia wapi.. .tuliweka watu (askari) hadi eneo la Kakunyu huku Bukoba Vijijini, kwa hiyo kuna ambao walijua tunaruka kupitia huko. Hatimaye nikaona sehemu ya kuruka ni pale pale walipovunja (daraja), lakini sikuwaambia wapiganaji wetu.

Sasa imefika siku ya kuruka, ndani ya saa 24. Nikawaita makamanda wangu nikawaambia sasa inabidi turuke kwenda kumshambulia adui, vifaa na kila kitu tayari, na askari kama tulivyofanya mafunzo wako tayari. Makamanda wakasema tunangoja tu amri yako, nikasema amri itatoka, wakauliza na kutaka niwaambie tunaruka kupitia eneo gapi, nikasema nitawaambia.

Ilipofika saa tano usiku nikawaambia makamanda… Marwa utakuwa katikati, Mayunga ukiruka tu unakwenda kushoto kuelekea eneo la Mbarara, Walden ukiruka tu unaelekea eneo la Minziro, Luhanga ukiruka tu unafuata njia ya Marwa halafu makamanda wengine watakuwa tayari kusubiri lolote (reserve). Baada ya maelekezo hayo nikawataka waende kuwaambia askari wao kwamba tunaruka leo (usiku huo), nikamwita Mhandisi Mkuu Rajabu na kumwambia utatandaza daraja lako (juu ya mto) saa nane usiku…akafanya kazi hiyo.

Saa nane usiku mpaka kufika saa tisa kuelekea saa 10 (takriban saa mbili hivi mfululizo) vikosi vikaanza kuruka kwa mujibu wa amri ya operesheni (operation order) ilivyotamkwa. Ilikuwa bahati mbaya nilipoteza askari mmoja tu pale wakati wa kuvuka daraja.

Baada ya hapo tulifanya mashambulizi, kazi ya kwanza ilikuwa ni kukamata eneo. Nimeeleza kazi niliyopewa nilitakiwa kurudisha heshima ya nchi hii na heshima ya nchi ni kurudisha mipaka yetu pale ilipokuwa awali na hivyo tukahakikisha tumefika Mtukula, wengine wamefika Minziro na wengine mpakani na Uganda kule.

Sasa jukumu la msingi la kurejesha mipaka ya nchi likawa limekamilika na Rais Julius Nyerere akaja kule na akasimama eneo lenye kilima pale na tukamweleza kwamba sasa mzee kazi ya kwanza uliyotutuma tumeimaliza, mipaka yetu sasa iko salama, akasema vizuri lakini huyu “mshenzi” huyu ametuharibia mambo mengi sana si bado yuko kule (nchini mwake), basi kazi bado haijakwisha.

Ndipo tukaingia hatua ya pili, maana sehemu ya kwanza ya ukombozi wa nchi yetu ikawa imekwisha ikafuata hatua hiyo ya pili ambayo ni kumwadhibu adui.

Raia Mwema: Je, baada ya kazi hiyo ya kwanza kukamilika ulirejeshwa kwenye nafasi ya Mnadhimu Mkuu (Chief of Staff)?

Jenerali Kiwelu: Pale kilichofanyika ni kwamba baada ya kumaliza ile kazi ya awali, tukaingia sasa kazi ya kuandaa na kutekeleza operesheni ya kuvuka mpaka ambayo ni tofauti na opereshani ya kumwondoa adui nyumbani kwako.

Sasa unakwenda nyumbani kwake lazima uwe na mkakati, sambamba na nguvu ya kutosha kwenda kwake, kwa hiyo rais ikabidi afanye utaratibu wa kumtafuta kamanda wa kuingia Uganda, mimi si ndiye niliyekuwa Chief of Staff na mkuu wa majeshi akiwa Twalipo ambaye naye hayuko makao makuu, kwa maana hiyo akiwa huku mbele (vitani) kule makao makuu hakuna maandalizi yoyote, nani anaanda nini… nani anafanya nini.

Kwa hiyo ilibidi nirudi Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam na pale (vitani kuelekea ndani ya Uganda) nikamkabidhi Msuguri, mimi nakamwambia nakwenda (makao makuu) kukufanyia kazi ya kuandaa vifaa, wewe kazi yako ni kwenda ndani kumwadhibu Idi Amin. Nikarudi makao makuu nilikuwa na mtu mmoja alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi, Kanali Bakari, basi tukafanya kazi na Bakari, tunkaenda hadi nchi za nje kutafuta nguvu…. zana za kivita.
Wako marafiki walitusaidia, sina sababu ya kuwataja sana lakini kati ya nchi rafiki tulizokwenda ni pamoja na Urusi, China, Korea na Bulgaria. Ikabidi tukusanye vifaa na ndipo hapo wananchi walichangia mambo mengi sana, wapo waliojitolea magari yao, vyakula, mifugo kama ng’ombe ili kuwawezesha wapiganaji wetu kule mstari na hatimaye Msuguri akuvuka mpaka akiwa na uhakika wa nguvu za kutosha na uangalizi huku nyuma anakotoka.
Raia Mwema: Kwa wakati huo wewe ndiye uliyekuwa makao makuu Dar, sasa uliwezaje kudhibiti link (viunganishi vya taarifa) za silaha mlizopata kutoka nje ya nchi?
Jenerali Kiwelu: Kwanza wakati nikiwa pale Kagera tulikuwa tumedhibiti sana uvujaji wa taarifa. Unajua kuna mkutano mmoja mkubwa wa kimataifa ulikuwa unaendelea pale Arusha uliokuwa umehusisha nchi nyingi huku vita pia ikiendelea na hao washiriki wa mkutano hawakujua chochote kilichokuwa kikiendelea nilidhibiti uvujaji wa taarifa, viongozi wengine tuliwapa amri maalumu hakuna kufika kwenye eneo la vita na wala kupewa taarifa yoyote, ni kama tulivyokuwa tunapambana kuwasaidia kule Msumbiji siku moja tukakuta mzee mmoja wa kizungu kule Tunduru anayo redio ameijichimbia ndani, kumbe alikuwa anawasiliana kwa maana ya kupeleka taarifa, tukamkamata.

Hata pale Karagwe, tulikuwa na watu fulani pale ambao ni kanisa fulani sitaki kuwataja nao pia walikuwa na redio ya mawasiliano, ukiona utafikiri mtu anapiga kinanda kumbe anapeleka taarifa, kwa hiyo tukafunga njia zote za mawasiliano, nikasema hakuna mawasiliano ya aina yoyote na taarifa zozote kwenda Ikulu nitapeleka, tulihakikisha taarifa hazivuji vinginevyo tusingeweza kuvuka pale.

Raia Mwema: Vipi kuhusu Yoweri Museven (Rais wa sasa wa Uganda), alikuwa sehemu ya mapambano?

Jenerali Kiwelu: Museven yeye alitokea huku nyuma kapitia Karagwe kalala kijijini pale wakati Mayunga amekwishavuka mpaka, akaungana na Mayunga, ukweli ni kwamba Jeshi la Tanzania na chini ya Luteni Jenerali Mayunga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kupita Mbarara na kutoka hapo kuelekea Kampala, na wengine wakapita Minziro kwenda kuungana kule. Museven hakuwa na jukumu la kuongoza ni kama alisaidia mambo kadhaa yakiwamo masuala ya taarifa.

Raia Mwema: Vipi kuhusu uteuzi wako kuwa mkuu wa mkoa?

Jenerali Kiwelu: Baada ya vita, tukawapokea vijana kutoka Uganda pale Bunazi, nikafanya kazi ya kuwasambaza na kuwarudisha kule walikotoka, wengine Ruvuma, Kigoma na maeneo mengine ya nchi. Tukahakikisha wamerudi na kupewa haki zao.

Baada ya kumaliza pale Bunazi, nikarudi Dar es Salaam kwenye kitengo changu cha Mnadhimu Mkuu, sasa makamanda wote wakawa wamerejea kutoka vitani. Ikabidi sasa jeshi lipangwe upya….unajua watu walikwishaonja kutoa roho za watu huwezi kucheza nao hivi hivi, ikabidi sasa tupangane upya.

Namna gani jeshi litakavyoendeshwa na kwa hiyo, Amiri Jeshi Mkuu akapanga upya…akasema sasa wewe bwana umemaliza kazi hii nakushukuru…sasa nataka kukupa kazi nyingine…nikamwambia sawa, nipo tayari kwa kazi yoyote, akaniambia utakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nikamwambia naenda lakini hii kazi sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na mimi nikiona kuna tatizo nitakuja. Kwa hiyo nikaenda zangu Tanga ndipo wakati huo yakafanyika mabadiliko, Twalipo akatoka pale akawa Waziri wa Ulinzi, Msuguri akawa Mkuu wa Majeshi halafu na Jenerali Kombe akawa Mnadhimu Mkuu, tukaendelea.

Raia Mwema: Nini hasa unachojivunia katika wadhifa wako wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga?

Jenerali Kiwelu: Tanga kuna mambo mengi. Lakini moja kubwa ni kwamba pale Tanga wale Waswahili wangu wa Tanga ni wavivu, hawakuwa watu wa maendeleo. Sasa walikuwa wanakaa pale kwenye nyumba zao za nyasi mjini, nikawaambia sikilizeni hatuwezi kuishi hivi…mtu lazima afanye kazi na mjiwekee kipato na mtengeneze nyumba.

Wakauliza tunatengenezaje na hatuna mashamba kwa ajili ya kutupatia kipato? Nikafanya uamuzi, nikaenda barabara ya kuelekea Muheza kuna mashamba ya mkonge pale na hapakuwa na mtu anayelima, nikasema nitachukua haya mashamba na wala sikuuliza ni ya nani.

Nikawaambia nyie mtakwenda kulima pale na kutakuwa na mabasi asubuhi na jioni ya kwenda na kurudi shambani, na kwamba wakishavuna watapata chakula lakini nikataka watengeneze nyumba zao na watoto wasome kwa kipato watakachopata.

Nikamwambia ofisa husika apime viwanja, lakini nikawaambia nyumba zao wasizivunje isipokuwa wajenge kuta kwa kuzizunguka na baada ya kufika hatua ya kupaua, wanaweza kuvunja nyumba za ndani yake za nyasi, ndivyo nyumba nyingi za Tanga zilivyojengwa kwa wakati huo.

Nilikaa pale kwa miaka nadhani mitatu tangu mwaka 1980 kisha nikahamishiwa Rukwa ambako nako pia kuna mambo mengi niliyofanya. Uzuri wa Rukwa watu wa kule ni wachapa kazi lakini tatizo lao walikuwa wanachapa kazi bila utaratibu. Nikawaambia msilime tu mahindi ya kutosha nyumba yako tu bali limeni kwa malengo ya kupata kipato. Nikawataka walime kwa utaratibu, wajue masuala ya mbegu, maandalizi ya shamba.

Lakini haikuwa kazi rahisi kwa sababu ilibidi tutengeneze kitu kama shule kijijini kwa ajili ya kumfundisha mtu kulima, kuandaa shamba, kupanda, kupalilia hadi kuvuna, ni miezi minne…watano amevuna ameweka kwenye kihenge, anakuwa amefaulu. Sasa mtu anapokuwa anajifunza kulima alikuwa akijifunza kilimo cha kisasa, kupanda kwa mistari, kutumia mbolea, kutumia dawa za kudhibiti wadudu na baada ya kuvuna, ajue namna ya kutunza mazao.

Sasa katika kuandaa mashamba wengine walikuwa wanatumia majembe madogo ya kukokotwa kwa ng’ombe na wengine majembe ya mkono, uongozi ngazi ya mkoa ilibidi tufanye utaratibu na tulifanikwa kwenda kununua majembe kutoka Zimbabwe ya kukokota kwa ng’ombe na ya kupandia. Niliomba fedha nikapewa za mbegu ambazo kule hakuna, nikaagiza mbegu kutoka Kenya lakini hazikuwa zinatosha, nikaenda kwenye wizara (ya kilimo) natafuta mbegu nako hakuna.

Lakini nikaona sio siku zote kwenda kutafuta mbegu, nikaanzisha shamba la mbegu eneo la Mlundikwa, mwaka wa pili tukawa sasa tunaweza kupata mbegu zetu na tukajua namna ya kuziweka katika madaraja ya ubora.

Sasa baada ya kuwa na uhakika wa mbegu tukaingia hatua ya matumizi ya majembe ya ng’ombe, tulipomaliza mwaka wa kwanza na wa pili, ule mwaka wa tatu tukafaulu na kupata mazao mengi, maana nia yangu pale ilikuwa ni kupata mavuno mengi ili kushindana na wenzangu wa mikoa mingine ya kilimo, na ikibidi hata kuwazidi lakini kwa manufaa ya watu wangu hasa katika kuongeza kipato chao mara dufu au zaidi.

Raia Mwema: Kwa hiyo kuwapo kwako Rukwa kulisababisha mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa mingine mikubwa ya kilimo kama Mbeya, Ruvuma na Iringa?

Jenerali Kiwelu: Kwanza mimi nikiwa kule nilijua Mbeya ambako nilikuwa napita pale, Iringa na Ruvuma ndio iliyokuwa mikoa mitatu mikubwa na mashuhuri kwa kilimo, ikiitwa “The Big Three”. Nikasema hawa hawawezi kuwa Big Three na mimi napita mikoa yao, changamoto yangu ya kwanza nikasema lazima niingie pale kwenye orodha ya Big Three ili tuwe Big Four.

Raia Mwema: Baadaye ulipelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera, hali ilikuwaje kule?

Jenerali Kiwelu: Unajua ule Mkoa wa Kagera unafafana hali ya hewa na mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro na Arusha, mimi sehemu ya asili ni Kilimanjaro ambako mazao ni pamoja na kahawa na migomba kule nako mazao ni hayo hayo, tofauti iliyokuwapo ni kwamba kule Kilimanjaro tulikuwa tunalima kahawa aina ya Arabika sasa Kagera ilikuwa nafasi yangu ya kujifunza kilimo cha kahawa aina ya Robusta, ikawa lazima niwainue wale wakulima tuone tunafanya vizuri zaidi. Sasa kule kwa sababu wengi ni wabishi kweli kweli wanataka lazima waone vitendo kwa mfano, ikabidi niwe na shamba la mfano na hata sasa baada ya kustaafu bado naendelea na kilimo kwenye shamba langu.

Chanzo Raia Mwema.

Maoni Yangu

Tumeeona jinsi Generala Kiwelu alimvyomnyima Sokoine taarifa za vita kwa kumwambia ni siri ya kijeshi na Sokoine pamoja na wadhifa aliokuwa nao aliheshimu hilo hakutaka zaidi ya jibu alilojibiwa.

Hivyo basi wanasiasa wetu wa kizazi hiki waige mfano wa Sokoine kwa kuheshimu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kutotaka kila kitu kuwa wazi ikiwemo eti kwa kuwa wao ni wabunge au wanasiasa wapo kwa niaba ya wananchi hapo watakuwa hawavitendei haki vyombo vyetu hivyo kwani vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha tuna kuwa na amani pamoja na uturuvu.

Hata huko Marekani na ulaya huwezi kukuta wanasiasa wanataka mambo ya jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuwekwa hadharani kama wa hapa kwetu wanavyotaka.
 
kumbe tanzania ilishirikiana na museven kumpindua idd amin dada nduli.

pia nimevutiwa jinsi vyombo vya ulinz na usalama vilivyopewa mawazir wenye ujuz na shughuli yao
 
Mjomba, mimi nilikuwa front katika vita vya mtukula na nilienda pia msumbiji kupambana na remamo baada ya kagera. Nalijua jeshi na vyombo ya usalama navijua na naviheshimu. Lakini uisasahau kwamba Jenerali hajasema yote kwa sababu tumefundikshwa diplomasia ya mawasiliano. Sawa kile kilwapata watu kama ..., n.k wakati mapambao yakaendelea na wengine wakapigwa marufuku kuonekana uwanja wa vita. Hawezi kusema na mimi siwezi kusema haya hapa.

Tambua kwamba jeshi ni kazi lakini kama ilyvomfanya kazi yeyote ana ofisi na maisha yake bianfsi. Na ndiyo sababu tunasisitiza Magufuli akama anataka kuliweka taifa mahala pema, atengeneze mfumo utakaomlazimisha kila mtu kutii hata kama hataki na bila kujali ana cheo gani. Tunaktaa taifa kuendelea kuendeshwa kwa mihemuko, sanaa na utashi wa mtu binafsi kwamba akiota hiki anafanya akija mwingine hataki kile anaacha kiwe chema aam kibaya na hakuna mfumo unaomlazimisha.

Nimekusoma sanakatika hitima yako ya kutaka watu waache kuingilia masuwala ya jeshi, naim naungana na wewe. Lakini tambua kwamba "LUGUMI SIYO SUALA LA KIJESHI, NA LUGUMI SI MWAJIRIWA WA JESHI ILA NI MBIA KATIKA FUSADI ULIOVUKA MIPAKA NA KUINGIA KATIKA JESHI LA POLISI". "KUWAZUIA WATANZANIA KUZUNGUMZIA LUGUMI NA UFISADI KATIKA JIESH LA POLISI, NI KULINGIA JESHI KWENYE KARANTINI PAMOJA NA JOKA AMBALO MWISHO WA SIKU UNAKUWA NA JESHI LISILO NA WAPIGANAJI, MAANA JOKA LINAKULA UASIKARI WAO NA KUACHA WATU WASIO WAPIGANAJI KAMBINI KITU AMBACHO NI KINUME NA MALENGO YA UWEPO WA MAJESHI".

Ungemalizia vizuri kama ungetoa wito kwa majeshi yetu kuzingatia uzalendo na uadilifu ulikuwepo siku zile badala ya kujiingiza katika matendo ya kifisadi halafu unataka yalindwe kwa ngao ya maadili. Maadadili yalivunjwa ndani ya jeshi. Tunataka jeshi letu liwe pure na lenye hadhi inayotamaniwa. Cha kwanza ni usafi wa jeshi badala ya kuwazuia wananchi wasifuatilie adui aliyeingia kule. Kumbuka jeshi ni letu sote na hivyo tunahitaji jeshi halisi lisilo na lugumi wala harufu ya vile.

Kinyume cha pale, TUTAENDELEA KUJENGA JESHI LILILO IMARA NA LENYE HADHI YA JUU KWA KULISAFISHA NA KUYATOA MAJOKA KAMA LUGUMI NA MILANGO YAKE KUIFUNGA KWA USALAMA WETU SOTE!. USISHANGAE SIKU MOJA HAPA TUNAKUJA NA HOJA YA UNUNUZI WA CHOPA.....KITU AMBACHO KWA SASA MUDA WAKE HAUJAFIKA, NINAKIACHA.

"LUGUMI SIYO SIRI YA JESHI, NA SIYO SUALA LA KIJESHI". Acha kumahribia Kiwelu kwa kumpindishia maelezo yake. Vinginevyo hata ulikuwa humwelewi na ndiyo sababu katika makalayako umekosa taarifa nyingi muhimu kwa kushindwa kuhoji maswali mengi muafaka.

"TUTAPAMBANANA MAFISADI KAMA LUGUMI, HATA KAMA UTAWAFICHA NDANI YA JESHI KWA KISINGIZIO CHA SIRI ZA JESHI AMBAZO KIWELU WALA HAKUMAANISHA SIRI ZA UFIRAUNI!. lOL!. Nenda kaanze upya!.
 
  • Asema katika Vita ya Kegara udhibiti wa mawasiliano na taarifa ulikuwa wa kiwango cha
Raia Mwema: Hali ilikuwaje kule eneo la mapambano wakati wa vita ya Kagera?
Jenerali Kikwelu: Kazi ilikuwa ngumu sana. Maana vijana wangu waliokuwa kule mbele, wale askari wa JWTZ walikuwa katika nusu morali, maana ukishatoka kwenye mstari wa mbele ukarudi nyuma morali ya vita inapungua.

Kwa hiyo kazi ya kwanza ilikuwa kuwajenga kisaikolojia. Kazi ya pili ilikuwa ni kupata reinforcement (kuongeza nguvu) kazi ambayo niliyomwachia Ernest Mwita Kiaro, hata CDF naye alikuja akakaa mahala fulani pale Bukoba (jirani), kwa hiyo Dar es Salaam tulimpa kazi Mwakalindile ndiye aliyekuwa anakaimu kama Chief of Staff, halafu Kiaro, chifu wa mgambo kazi yake ilikuwa kukusanya mgambo wote nchini, akina Mwakalindile ni kukusanya JKT, Polisi na Magareza, wote walikuja kule.

Ninaposema kulikuwa na changamoto kubwa sana ni kwamba hawa askari hata siku moja hawakuwahi kuwa eneo la vita ama eneo la mafunzo ya kivita kwa pamoja. Kwa hiyo, ilikuwa kazi kubwa, ndiyo maana ikatuchukua muda pale kabla hatujaruka daraja, ilikuwa ni lazima nifanye mafunzo ya pamoja ili kuwaweka watu (askari kutoka Magereza, Polisi, Mgambo na JKT) waweze kufanya kazi pamoja.

Lengo ilikuwa kuondoa fikra za kitabaka vitani, kuachana na mambo ya huyu mgambo au JKT. Kwa hiyo nilianzisha range ya kupiga silaha, mtu unampa risasi kumi anapiga zote wash out (anakosa kulenga shabaha), maana sisi (jeshini) tuna kitu kinaitwa bull, inner, outer n.k… sasa huyu unampa risasi zote anapiga wash out, tunampa nyingine, akipiga ile target namwambia umepiga bega (target hasa ni kifuani kwenye moyo au kichwani) sasa wakati mwingine ukimpa risasi tano… mbili anapiga ndani, nikasema sasa wameiva.

Kwa hiyo ilikuwa ni mafunzo ya msingi. Kwa mfano, ukiwa porini na ndege ya adui inakuja ufanye nini.

Unaulizwa ukiona ndege ya adui inatoka kule wewe unakwenda wapi? Namna gani mnaweza kusonga mbele, mnajihami vipi na namna gani mnaweza kupumzika kwa sababu askari hawezi kupumzika chini ya kivuli cha mti. Sasa baada ya mafunzo hayo ya pamoja, tukaridhika askari wetu wameiva, tukaanza kusonga mbele kutoka Katoro hadi tukafika karibu na mpakani, tukaweka kambi ambayo mpaka leo ipo pale, nyuma ya Mtukula.

Raia Mwema: Labda ungeeleza kuhusu Daraja la Kagera kushambuliwa na adui?

Jenerali Kiwelu: Daraja hili wakati nimefika tu, kutoka kupewa ile amri (ya kwenda vitani)… nimefika Kaboya, siku hiyo hiyo jioni nikatoka kwenda kutazama daraja. Nikafika darajani upande wa kulia kama unakwenda Mtukula umbali wa kilomita moja, nikaliona daraja ambalo baada ya dakika 15 nikiwa pale likalipuka, kwa hiyo sikuweza kuwahi kuweka askari pale darajani.

Wakati nafika pale na mtu mmoja anaitwa Kanali Kitete tunatazama…nataka sasa kufanya mbinu namna gani nitavuka daraja ili majeshi yangu yakae upande mwingine.

Basi nikarudi zangu Kaboya kwa ajili ya kuanza kufanya mkakati mwingine maana pale daraja limekwishavunjwa, nikaripoti daraja limevunjwa…hakuna daraja kuanzia sasa. Ndipo tukaanza mipango mingine kuhusu daraja, tukaleta madaraja ya muda na mtu mmoja anaitwa Brigedia Rajabu ndiye aliyekuja na vifaa hivyo kutoka kikosi chetu cha uhandishi na tukamweka sehemu ya umbali wa kama kilomita tano kutoka kwenye daraja, ndipo alipofanya mafunzo yake ili baadaye kufunga daraja la muda.

Raia Mwema: Ilichukua muda gani hadi kufanikisha daraja hilo la muda?

Jenerali Kiwelu: Unajua kuna wanazungumza kwa ushabiki mambo ya vita tu wakati hawajui chochote kuhusu vita, watu hawa mimi nawaita majitu, hawajui maana ya vita. Wapo wengine wanafikiri jeshi hii la Tanzania lilikuwa tayari kwamba unakwenda tu kwenye vita, sasa ukiwaambia kwamba jeshi hili tulipokwenda kwenye vita tulikuwa na mchanganiyo wa watu wote hawa, halafu pia kuleta vifaa vya kuvuka daraja, kuwafundisha namna ya kuweka daraja, kuleta vifaru, ndipo wataona ugumu wa kazi iliyokuwapo.

Pale ni lazima uwe na nguvu ya kutosha kuhakikisha kwamba mkiruka (daraja) hakuna kurudishwa nyuma. Kama nilivyotangulia kusema wale askari wetu waliokuwa kule awali, walikuwa wachache na walivurumishwa na adui kiasi cha morali yao kuwa chini kivita, kwa hiyo ilikuwa ni lazima nihakikishe sasa watu wangu ni imara, vifaa viko.

Tulikuwa tunafanya mipango na ukaguzi pamoja na makamanda wangu, akina Jenerali Marwa, Jenerali Luhanga, Mayunga, Walden… tunakwenda hadi tunafika pale kwenye daraja kwa sababu Idi Amin alirudisha majeshi yake (Uganda) akiamini kazi imekwisha. Sasa tulikuwa na makamanda wangu hao tunakwenda pale kupanga mikakati, lakini, swali kwamba wapi tupite (kuvuka daraja) na lini sikuwaambia.

Hakuna mtu aliyejua hata Edward Sokoine (aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Mwalimu Nyerere) alikuja akaniuliza …. sasa General nafikiri tumechelewa sana kuruka (daraja), sasa unaruka lini na unapitia wapi?

Nikamwambia hiyo ni siri ya kijeshi… akasema hata mimi? Nikamwambia ndiyo mzee. Kwa hiyo mimi nilikuwa napita kando ya ule mto kwa gari hadi Murongo, halafu watu wanapiga mabomu kila sehemu lakini hawajui tunaruka wapi kupitia wapi.. .tuliweka watu (askari) hadi eneo la Kakunyu huku Bukoba Vijijini, kwa hiyo kuna ambao walijua tunaruka kupitia huko. Hatimaye nikaona sehemu ya kuruka ni pale pale walipovunja (daraja), lakini sikuwaambia wapiganaji wetu.

Sasa imefika siku ya kuruka, ndani ya saa 24. Nikawaita makamanda wangu nikawaambia sasa inabidi turuke kwenda kumshambulia adui, vifaa na kila kitu tayari, na askari kama tulivyofanya mafunzo wako tayari. Makamanda wakasema tunangoja tu amri yako, nikasema amri itatoka, wakauliza na kutaka niwaambie tunaruka kupitia eneo gapi, nikasema nitawaambia.

Ilipofika saa tano usiku nikawaambia makamanda… Marwa utakuwa katikati, Mayunga ukiruka tu unakwenda kushoto kuelekea eneo la Mbarara, Walden ukiruka tu unaelekea eneo la Minziro, Luhanga ukiruka tu unafuata njia ya Marwa halafu makamanda wengine watakuwa tayari kusubiri lolote (reserve). Baada ya maelekezo hayo nikawataka waende kuwaambia askari wao kwamba tunaruka leo (usiku huo), nikamwita Mhandisi Mkuu Rajabu na kumwambia utatandaza daraja lako (juu ya mto) saa nane usiku…akafanya kazi hiyo.

Saa nane usiku mpaka kufika saa tisa kuelekea saa 10 (takriban saa mbili hivi mfululizo) vikosi vikaanza kuruka kwa mujibu wa amri ya operesheni (operation order) ilivyotamkwa. Ilikuwa bahati mbaya nilipoteza askari mmoja tu pale wakati wa kuvuka daraja.

Baada ya hapo tulifanya mashambulizi, kazi ya kwanza ilikuwa ni kukamata eneo. Nimeeleza kazi niliyopewa nilitakiwa kurudisha heshima ya nchi hii na heshima ya nchi ni kurudisha mipaka yetu pale ilipokuwa awali na hivyo tukahakikisha tumefika Mtukula, wengine wamefika Minziro na wengine mpakani na Uganda kule.

Sasa jukumu la msingi la kurejesha mipaka ya nchi likawa limekamilika na Rais Julius Nyerere akaja kule na akasimama eneo lenye kilima pale na tukamweleza kwamba sasa mzee kazi ya kwanza uliyotutuma tumeimaliza, mipaka yetu sasa iko salama, akasema vizuri lakini huyu “mshenzi” huyu ametuharibia mambo mengi sana si bado yuko kule (nchini mwake), basi kazi bado haijakwisha.

Ndipo tukaingia hatua ya pili, maana sehemu ya kwanza ya ukombozi wa nchi yetu ikawa imekwisha ikafuata hatua hiyo ya pili ambayo ni kumwadhibu adui.

Raia Mwema: Je, baada ya kazi hiyo ya kwanza kukamilika ulirejeshwa kwenye nafasi ya Mnadhimu Mkuu (Chief of Staff)?

Jenerali Kiwelu: Pale kilichofanyika ni kwamba baada ya kumaliza ile kazi ya awali, tukaingia sasa kazi ya kuandaa na kutekeleza operesheni ya kuvuka mpaka ambayo ni tofauti na opereshani ya kumwondoa adui nyumbani kwako.

Sasa unakwenda nyumbani kwake lazima uwe na mkakati, sambamba na nguvu ya kutosha kwenda kwake, kwa hiyo rais ikabidi afanye utaratibu wa kumtafuta kamanda wa kuingia Uganda, mimi si ndiye niliyekuwa Chief of Staff na mkuu wa majeshi akiwa Twalipo ambaye naye hayuko makao makuu, kwa maana hiyo akiwa huku mbele (vitani) kule makao makuu hakuna maandalizi yoyote, nani anaanda nini… nani anafanya nini.

Kwa hiyo ilibidi nirudi Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam na pale (vitani kuelekea ndani ya Uganda) nikamkabidhi Msuguri, mimi nakamwambia nakwenda (makao makuu) kukufanyia kazi ya kuandaa vifaa, wewe kazi yako ni kwenda ndani kumwadhibu Idi Amin. Nikarudi makao makuu nilikuwa na mtu mmoja alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi, Kanali Bakari, basi tukafanya kazi na Bakari, tunkaenda hadi nchi za nje kutafuta nguvu…. zana za kivita.
Wako marafiki walitusaidia, sina sababu ya kuwataja sana lakini kati ya nchi rafiki tulizokwenda ni pamoja na Urusi, China, Korea na Bulgaria. Ikabidi tukusanye vifaa na ndipo hapo wananchi walichangia mambo mengi sana, wapo waliojitolea magari yao, vyakula, mifugo kama ng’ombe ili kuwawezesha wapiganaji wetu kule mstari na hatimaye Msuguri akuvuka mpaka akiwa na uhakika wa nguvu za kutosha na uangalizi huku nyuma anakotoka.
Raia Mwema: Kwa wakati huo wewe ndiye uliyekuwa makao makuu Dar, sasa uliwezaje kudhibiti link (viunganishi vya taarifa) za silaha mlizopata kutoka nje ya nchi?
Jenerali Kiwelu: Kwanza wakati nikiwa pale Kagera tulikuwa tumedhibiti sana uvujaji wa taarifa. Unajua kuna mkutano mmoja mkubwa wa kimataifa ulikuwa unaendelea pale Arusha uliokuwa umehusisha nchi nyingi huku vita pia ikiendelea na hao washiriki wa mkutano hawakujua chochote kilichokuwa kikiendelea nilidhibiti uvujaji wa taarifa, viongozi wengine tuliwapa amri maalumu hakuna kufika kwenye eneo la vita na wala kupewa taarifa yoyote, ni kama tulivyokuwa tunapambana kuwasaidia kule Msumbiji siku moja tukakuta mzee mmoja wa kizungu kule Tunduru anayo redio ameijichimbia ndani, kumbe alikuwa anawasiliana kwa maana ya kupeleka taarifa, tukamkamata.

Hata pale Karagwe, tulikuwa na watu fulani pale ambao ni kanisa fulani sitaki kuwataja nao pia walikuwa na redio ya mawasiliano, ukiona utafikiri mtu anapiga kinanda kumbe anapeleka taarifa, kwa hiyo tukafunga njia zote za mawasiliano, nikasema hakuna mawasiliano ya aina yoyote na taarifa zozote kwenda Ikulu nitapeleka, tulihakikisha taarifa hazivuji vinginevyo tusingeweza kuvuka pale.

Raia Mwema: Vipi kuhusu Yoweri Museven (Rais wa sasa wa Uganda), alikuwa sehemu ya mapambano?

Jenerali Kiwelu: Museven yeye alitokea huku nyuma kapitia Karagwe kalala kijijini pale wakati Mayunga amekwishavuka mpaka, akaungana na Mayunga, ukweli ni kwamba Jeshi la Tanzania na chini ya Luteni Jenerali Mayunga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kupita Mbarara na kutoka hapo kuelekea Kampala, na wengine wakapita Minziro kwenda kuungana kule. Museven hakuwa na jukumu la kuongoza ni kama alisaidia mambo kadhaa yakiwamo masuala ya taarifa.

Raia Mwema: Vipi kuhusu uteuzi wako kuwa mkuu wa mkoa?

Jenerali Kiwelu: Baada ya vita, tukawapokea vijana kutoka Uganda pale Bunazi, nikafanya kazi ya kuwasambaza na kuwarudisha kule walikotoka, wengine Ruvuma, Kigoma na maeneo mengine ya nchi. Tukahakikisha wamerudi na kupewa haki zao.

Baada ya kumaliza pale Bunazi, nikarudi Dar es Salaam kwenye kitengo changu cha Mnadhimu Mkuu, sasa makamanda wote wakawa wamerejea kutoka vitani. Ikabidi sasa jeshi lipangwe upya….unajua watu walikwishaonja kutoa roho za watu huwezi kucheza nao hivi hivi, ikabidi sasa tupangane upya.

Namna gani jeshi litakavyoendeshwa na kwa hiyo, Amiri Jeshi Mkuu akapanga upya…akasema sasa wewe bwana umemaliza kazi hii nakushukuru…sasa nataka kukupa kazi nyingine…nikamwambia sawa, nipo tayari kwa kazi yoyote, akaniambia utakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nikamwambia naenda lakini hii kazi sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na mimi nikiona kuna tatizo nitakuja. Kwa hiyo nikaenda zangu Tanga ndipo wakati huo yakafanyika mabadiliko, Twalipo akatoka pale akawa Waziri wa Ulinzi, Msuguri akawa Mkuu wa Majeshi halafu na Jenerali Kombe akawa Mnadhimu Mkuu, tukaendelea.

Raia Mwema: Nini hasa unachojivunia katika wadhifa wako wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga?

Jenerali Kiwelu: Tanga kuna mambo mengi. Lakini moja kubwa ni kwamba pale Tanga wale Waswahili wangu wa Tanga ni wavivu, hawakuwa watu wa maendeleo. Sasa walikuwa wanakaa pale kwenye nyumba zao za nyasi mjini, nikawaambia sikilizeni hatuwezi kuishi hivi…mtu lazima afanye kazi na mjiwekee kipato na mtengeneze nyumba.

Wakauliza tunatengenezaje na hatuna mashamba kwa ajili ya kutupatia kipato? Nikafanya uamuzi, nikaenda barabara ya kuelekea Muheza kuna mashamba ya mkonge pale na hapakuwa na mtu anayelima, nikasema nitachukua haya mashamba na wala sikuuliza ni ya nani.

Nikawaambia nyie mtakwenda kulima pale na kutakuwa na mabasi asubuhi na jioni ya kwenda na kurudi shambani, na kwamba wakishavuna watapata chakula lakini nikataka watengeneze nyumba zao na watoto wasome kwa kipato watakachopata.

Nikamwambia ofisa husika apime viwanja, lakini nikawaambia nyumba zao wasizivunje isipokuwa wajenge kuta kwa kuzizunguka na baada ya kufika hatua ya kupaua, wanaweza kuvunja nyumba za ndani yake za nyasi, ndivyo nyumba nyingi za Tanga zilivyojengwa kwa wakati huo.

Nilikaa pale kwa miaka nadhani mitatu tangu mwaka 1980 kisha nikahamishiwa Rukwa ambako nako pia kuna mambo mengi niliyofanya. Uzuri wa Rukwa watu wa kule ni wachapa kazi lakini tatizo lao walikuwa wanachapa kazi bila utaratibu. Nikawaambia msilime tu mahindi ya kutosha nyumba yako tu bali limeni kwa malengo ya kupata kipato. Nikawataka walime kwa utaratibu, wajue masuala ya mbegu, maandalizi ya shamba.

Lakini haikuwa kazi rahisi kwa sababu ilibidi tutengeneze kitu kama shule kijijini kwa ajili ya kumfundisha mtu kulima, kuandaa shamba, kupanda, kupalilia hadi kuvuna, ni miezi minne…watano amevuna ameweka kwenye kihenge, anakuwa amefaulu. Sasa mtu anapokuwa anajifunza kulima alikuwa akijifunza kilimo cha kisasa, kupanda kwa mistari, kutumia mbolea, kutumia dawa za kudhibiti wadudu na baada ya kuvuna, ajue namna ya kutunza mazao.

Sasa katika kuandaa mashamba wengine walikuwa wanatumia majembe madogo ya kukokotwa kwa ng’ombe na wengine majembe ya mkono, uongozi ngazi ya mkoa ilibidi tufanye utaratibu na tulifanikwa kwenda kununua majembe kutoka Zimbabwe ya kukokota kwa ng’ombe na ya kupandia. Niliomba fedha nikapewa za mbegu ambazo kule hakuna, nikaagiza mbegu kutoka Kenya lakini hazikuwa zinatosha, nikaenda kwenye wizara (ya kilimo) natafuta mbegu nako hakuna.

Lakini nikaona sio siku zote kwenda kutafuta mbegu, nikaanzisha shamba la mbegu eneo la Mlundikwa, mwaka wa pili tukawa sasa tunaweza kupata mbegu zetu na tukajua namna ya kuziweka katika madaraja ya ubora.

Sasa baada ya kuwa na uhakika wa mbegu tukaingia hatua ya matumizi ya majembe ya ng’ombe, tulipomaliza mwaka wa kwanza na wa pili, ule mwaka wa tatu tukafaulu na kupata mazao mengi, maana nia yangu pale ilikuwa ni kupata mavuno mengi ili kushindana na wenzangu wa mikoa mingine ya kilimo, na ikibidi hata kuwazidi lakini kwa manufaa ya watu wangu hasa katika kuongeza kipato chao mara dufu au zaidi.

Raia Mwema: Kwa hiyo kuwapo kwako Rukwa kulisababisha mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa mingine mikubwa ya kilimo kama Mbeya, Ruvuma na Iringa?

Jenerali Kiwelu: Kwanza mimi nikiwa kule nilijua Mbeya ambako nilikuwa napita pale, Iringa na Ruvuma ndio iliyokuwa mikoa mitatu mikubwa na mashuhuri kwa kilimo, ikiitwa “The Big Three”. Nikasema hawa hawawezi kuwa Big Three na mimi napita mikoa yao, changamoto yangu ya kwanza nikasema lazima niingie pale kwenye orodha ya Big Three ili tuwe Big Four.

Raia Mwema: Baadaye ulipelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera, hali ilikuwaje kule?

Jenerali Kiwelu: Unajua ule Mkoa wa Kagera unafafana hali ya hewa na mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro na Arusha, mimi sehemu ya asili ni Kilimanjaro ambako mazao ni pamoja na kahawa na migomba kule nako mazao ni hayo hayo, tofauti iliyokuwapo ni kwamba kule Kilimanjaro tulikuwa tunalima kahawa aina ya Arabika sasa Kagera ilikuwa nafasi yangu ya kujifunza kilimo cha kahawa aina ya Robusta, ikawa lazima niwainue wale wakulima tuone tunafanya vizuri zaidi. Sasa kule kwa sababu wengi ni wabishi kweli kweli wanataka lazima waone vitendo kwa mfano, ikabidi niwe na shamba la mfano na hata sasa baada ya kustaafu bado naendelea na kilimo kwenye shamba langu.

Chanzo Raia Mwema.

Maoni Yangu

Tumeeona jinsi Generala Kiwelu alimvyomnyima Sokoine taarifa za vita kwa kumwambia ni siri ya kijeshi na Sokoine pamoja na wadhifa aliokuwa nao aliheshimu hilo hakutaka zaidi ya jibu alilojibiwa.

Hivyo basi wanasiasa wetu wa kizazi hiki waige mfano wa Sokoine kwa kuheshimu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kutotaka kila kitu kuwa wazi ikiwemo eti kwa kuwa wao ni wabunge au wanasiasa wapo kwa niaba ya wananchi hapo watakuwa hawavitendei haki vyombo vyetu hivyo kwani vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha tuna kuwa na amani pamoja na uturuvu.

Hata huko Marekani na ulaya huwezi kukuta wanasiasa wanataka mambo ya jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuwekwa hadharani kama wa hapa kwetu wanavyotaka.

Lugumi sio
 
MNADHIMU Mkuu wa Majeshi (mstaafu), Jenerali Tumainieli Kiwelu, amesema Rais Dk. John Magufuli ni kiongozi wa uhakika, kwa kuwa hana ahadi alizoziita za “blaa blaa” na kwamba, ni mtu wa kusimamia anachokiamini.

Jenerali Kiwelu ambaye katika vita vya Uganda dhidi ya Idi Amini alikuwa na jukumu nyeti la kuratibu majeshi ya Tanzania na kuongoza vita hivyo hadi kufikia ushindi, ametoa kauli yake hiyo katika mahojiano maalumu na gazeti hili hivi karibuni nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, mahojiano ambayo sehemu yake ya kwanza imechapishwa kwenye gazeti hili na sehemu ya pili itaendelea wiki ijayo.

Katika mahojiano hayo ambapo amezungumzia masuala mbalimbali ya utumishi wake jeshini na hata nje ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambako amewahi kuwa mkuu wa mikoa ya Kagera, Shinyanga, Rukwa na Tanga, aliweka bayana kwamba Rais Magufuli ni kiongozi bora.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa Rais Magufuli alisema; “Mheshimiwa Magufuli ana sifa nyingi sana hana blaa blaa ni mtendaji, akiamua jambo anaamua on principle (kwa misingi) na atalisimamia hivyo, huwezi kumwondoa hapo. Kama anasema hili ni uchafu ni uchafu tu na anazo sababu za kusema hivyo.”

Kuhusu anavyomfahamu Magufuli alijibu; “Mimi namfahamu kiasi kwa kipindi cha miaka kama tisa, nimekuwa Kagera kwa miaka yote kama Mkuu wa Mkoa naye akiwa mbunge na mjumbe wa RCC (Kamati ya Maendeleo ya Mkoa) na pia nimekuwa nikifanya ziara kwenye wilaya yake, tunaendesha miradi mbalimbali. Kwa hiyo yule kwa kweli akiamua jambo …akisema ujue hawezi kurudi nyuma, hana ahadi za blaa blaa.”

Akaongeza kusema; “…ni mwanasayansi anafanya utafiti kwanza ili kujua hili jambo linatekelezeka na kisha anasimama hapo hapo kuhakikisha linatekelezeka.”

Kuhusu wanaoamini Magufuli ni nguvu ya soda akajibu; “Hawa watu wengine, unajua mimi bahati mbaya sijui namna ya kutukana sana nasema watu wengine hawa wanaosema kwamba mwendo wake huu si wa kudumu, mimi siwezi kuwaita wajinga, nasema tu ni watu wasiojua kutazama mambo.

Magufuli hawezi kurudi nyuma amefanya kazi kwa miaka 20 someni historia yake, wewe ukimweka kwenye samaki atashughulika na samaki, atashughulika mpaka aone lengo liliowekwa linatekelezwa.”

Raia Mwema
 
Hii ni sehemu ya pili ya mahojiano kati ya Jenerali Kiwelu na mwandishi Livingstone Luhere wa gazeti la Raia mwema.

Nimependa namna Kiwelu alivyofunguka. Nafikiri ni vyema makamanda wetu wakawa wanaandika vitabu kuhusu matukio muhimu kuhusu harakati za jeshi letu angalau za miaka 30 iliyopita.

Habari hii hapa chini:

------------------------

  • Asema katika Vita ya Kegara udhibiti wa mawasiliano na taarifa ulikuwa wa kiwango cha juu
  • Akumbuka namna alivyoteuliwa kuwa balozi na kisha uteuzi ukaishia ‘hewani’, sasa ni mkulima

Ifuatayo ni sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano kati ya Mwandishi wa Habari, Livingstone Ruehere na Jenerali (mstaafu) wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Tumainieli Kiwelu.
………………

Raia Mwema: Hali ilikuwaje kule eneo la mapambano wakati wa vita ya Kagera?

Jenerali Kikwelu: Kazi ilikuwa ngumu sana. Maana vijana wangu waliokuwa kule mbele, wale askari wa JWTZ walikuwa katika nusu morali, maana ukishatoka kwenye mstari wa mbele ukarudi nyuma morali ya vita inapungua. Kwa hiyo kazi ya kwanza ilikuwa kuwajenga kisaikolojia. Kazi ya pili ilikuwa ni kupata reinforcement (kuongeza nguvu) kazi ambayo niliyomwachia Ernest Mwita Kiaro, hata CDF naye alikuja akakaa mahala fulani pale Bukoba (jirani), kwa hiyo Dar es Salaam tulimpa kazi Mwakalindile ndiye aliyekuwa anakaimu kama Chief of Staff, halafu Kiaro, chifu wa mgambo kazi yake ilikuwa kukusanya mgambo wote nchini, akina Mwakalindile ni kukusanya JKT, Polisi na Magareza, wote walikuja kule.

Ninaposema kulikuwa na changamoto kubwa sana ni kwamba hawa askari hata siku moja hawakuwahi kuwa eneo la vita ama eneo la mafunzo ya kivita kwa pamoja. Kwa hiyo, ilikuwa kazi kubwa, ndiyo maana ikatuchukua muda pale kabla hatujaruka daraja, ilikuwa ni lazima nifanye mafunzo ya pamoja ili kuwaweka watu (askari kutoka Magereza, Polisi, Mgambo na JKT) waweze kufanya kazi pamoja.

Lengo ilikuwa kuondoa fikra za kitabaka vitani, kuachana na mambo ya huyu mgambo au JKT. Kwa hiyo nilianzisha range ya kupiga silaha, mtu unampa risasi kumi anapiga zote wash out (anakosa kulenga shabaha), maana sisi (jeshini) tuna kitu kinaitwa bull, inner, outer n.k… sasa huyu unampa risasi zote anapiga wash out, tunampa nyingine, akipiga ile target namwambia umepiga bega (target hasa ni kifuani kwenye moyo au kichwani) sasa wakati mwingine ukimpa risasi tano… mbili anapiga ndani, nikasema sasa wameiva.

Kwa hiyo ilikuwa ni mafunzo ya msingi. Kwa mfano, ukiwa porini na ndege ya adui inakuja ufanye nini. Unaulizwa ukiona ndege ya adui inatoka kule wewe unakwenda wapi? Namna gani mnaweza kusonga mbele, mnajihami vipi na namna gani mnaweza kupumzika kwa sababu askari hawezi kupumzika chini ya kivuli cha mti. Sasa baada ya mafunzo hayo ya pamoja, tukaridhika askari wetu wameiva, tukaanza kusonga mbele kutoka Katoro hadi tukafika karibu na mpakani, tukaweka kambi ambayo mpaka leo ipo pale, nyuma ya Mtukula.

Raia Mwema: Labda ungeeleza kuhusu Daraja la Kagera kushambuliwa na adui?

Jenerali Kiwelu: Daraja hili wakati nimefika tu, kutoka kupewa ile amri (ya kwenda vitani)… nimefika Kaboya, siku hiyo hiyo jioni nikatoka kwenda kutazama daraja. Nikafika darajani upande wa kulia kama unakwenda Mtukula umbali wa kilomita moja, nikaliona daraja ambalo baada ya dakika 15 nikiwa pale likalipuka, kwa hiyo sikuweza kuwahi kuweka askari pale darajani.

Wakati nafika pale na mtu mmoja anaitwa Kanali Kitete tunatazama…nataka sasa kufanya mbinu namna gani nitavuka daraja ili majeshi yangu yakae upande mwingine.
Basi nikarudi zangu Kaboya kwa ajili ya kuanza kufanya mkakati mwingine maana pale daraja limekwishavunjwa, nikaripoti daraja limevunjwa…hakuna daraja kuanzia sasa. Ndipo tukaanza mipango mingine kuhusu daraja, tukaleta madaraja ya muda na mtu mmoja anaitwa Brigedia Rajabu ndiye aliyekuja na vifaa hivyo kutoka kikosi chetu cha uhandishi na tukamweka sehemu ya umbali wa kama kilomita tano kutoka kwenye daraja, ndipo alipofanya mafunzo yake ili baadaye kufunga daraja la muda.

Raia Mwema: Ilichukua muda gani hadi kufanikisha daraja hilo la muda?

Jenerali Kiwelu: Unajua kuna wanazungumza kwa ushabiki mambo ya vita tu wakati hawajui chochote kuhusu vita, watu hawa mimi nawaita majitu, hawajui maana ya vita. Wapo wengine wanafikiri jeshi hii la Tanzania lilikuwa tayari kwamba unakwenda tu kwenye vita, sasa ukiwaambia kwamba jeshi hili tulipokwenda kwenye vita tulikuwa na mchanganiyo wa watu wote hawa, halafu pia kuleta vifaa vya kuvuka daraja, kuwafundisha namna ya kuweka daraja, kuleta vifaru, ndipo wataona ugumu wa kazi iliyokuwapo.

Pale ni lazima uwe na nguvu ya kutosha kuhakikisha kwamba mkiruka (daraja) hakuna kurudishwa nyuma. Kama nilivyotangulia kusema wale askari wetu waliokuwa kule awali, walikuwa wachache na walivurumishwa na adui kiasi cha morali yao kuwa chini kivita, kwa hiyo ilikuwa ni lazima nihakikishe sasa watu wangu ni imara, vifaa viko.

Tulikuwa tunafanya mipango na ukaguzi pamoja na makamanda wangu, akina Jenerali Marwa, Jenerali Luhanga, Mayunga, Walden… tunakwenda hadi tunafika pale kwenye daraja kwa sababu Idi Amin alirudisha majeshi yake (Uganda) akiamini kazi imekwisha. Sasa tulikuwa na makamanda wangu hao tunakwenda pale kupanga mikakati, lakini, swali kwamba wapi tupite (kuvuka daraja) na lini sikuwaambia. Hakuna mtu aliyejua hata Edward Sokoine (aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Mwalimu Nyerere) alikuja akaniuliza …. sasa General nafikiri tumechelewa sana kuruka (daraja), sasa unaruka lini na unapitia wapi?

Nikamwambia hiyo ni siri ya kijeshi… akasema hata mimi? Nikamwambia ndiyo mzee. Kwa hiyo mimi nilikuwa napita kando ya ule mto kwa gari hadi Murongo, halafu watu wanapiga mabomu kila sehemu lakini hawajui tunaruka wapi kupitia wapi.. .tuliweka watu (askari) hadi eneo la Kakunyu huku Bukoba Vijijini, kwa hiyo kuna ambao walijua tunaruka kupitia huko. Hatimaye nikaona sehemu ya kuruka ni pale pale walipovunja (daraja), lakini sikuwaambia wapiganaji wetu.

Sasa imefika siku ya kuruka, ndani ya saa 24. Nikawaita makamanda wangu nikawaambia sasa inabidi turuke kwenda kumshambulia adui, vifaa na kila kitu tayari, na askari kama tulivyofanya mafunzo wako tayari. Makamanda wakasema tunangoja tu amri yako, nikasema amri itatoka, wakauliza na kutaka niwaambie tunaruka kupitia eneo gapi, nikasema nitawaambia.

Ilipofika saa tano usiku nikawaambia makamanda… Marwa utakuwa katikati, Mayunga ukiruka tu unakwenda kushoto kuelekea eneo la Mbarara, Walden ukiruka tu unaelekea eneo la Minziro, Luhanga ukiruka tu unafuata njia ya Marwa halafu makamanda wengine watakuwa tayari kusubiri lolote (reserve). Baada ya maelekezo hayo nikawataka waende kuwaambia askari wao kwamba tunaruka leo (usiku huo), nikamwita Mhandisi Mkuu Rajabu na kumwambia utatandaza daraja lako (juu ya mto) saa nane usiku…akafanya kazi hiyo.

Saa nane usiku mpaka kufika saa tisa kuelekea saa 10 (takriban saa mbili hivi mfululizo) vikosi vikaanza kuruka kwa mujibu wa amri ya operesheni (operation order) ilivyotamkwa. Ilikuwa bahati mbaya nilipoteza askari mmoja tu pale wakati wa kuvuka daraja.

Baada ya hapo tulifanya mashambulizi, kazi ya kwanza ilikuwa ni kukamata eneo. Nimeeleza kazi niliyopewa nilitakiwa kurudisha heshima ya nchi hii na heshima ya nchi ni kurudisha mipaka yetu pale ilipokuwa awali na hivyo tukahakikisha tumefika Mtukula, wengine wamefika Minziro na wengine mpakani na Uganda kule.

Sasa jukumu la msingi la kurejesha mipaka ya nchi likawa limekamilika na Rais Julius Nyerere akaja kule na akasimama eneo lenye kilima pale na tukamweleza kwamba sasa mzee kazi ya kwanza uliyotutuma tumeimaliza, mipaka yetu sasa iko salama, akasema vizuri lakini huyu “mshenzi” huyu ametuharibia mambo mengi sana si bado yuko kule (nchini mwake), basi kazi bado haijakwisha.

Ndipo tukaingia hatua ya pili, maana sehemu ya kwanza ya ukombozi wa nchi yetu ikawa imekwisha ikafuata hatua hiyo ya pili ambayo ni kumwadhibu adui.

Raia Mwema: Je, baada ya kazi hiyo ya kwanza kukamilika ulirejeshwa kwenye nafasi ya Mnadhimu Mkuu (Chief of Staff)?

Jenerali Kiwelu: Pale kilichofanyika ni kwamba baada ya kumaliza ile kazi ya awali, tukaingia sasa kazi ya kuandaa na kutekeleza operesheni ya kuvuka mpaka ambayo ni tofauti na opereshani ya kumwondoa adui nyumbani kwako. Sasa unakwenda nyumbani kwake lazima uwe na mkakati, sambamba na nguvu ya kutosha kwenda kwake, kwa hiyo rais ikabidi afanye utaratibu wa kumtafuta kamanda wa kuingia Uganda, mimi si ndiye niliyekuwa Chief of Staff na mkuu wa majeshi akiwa Twalipo ambaye naye hayuko makao makuu, kwa maana hiyo akiwa huku mbele (vitani) kule makao makuu hakuna maandalizi yoyote, nani anaanda nini… nani anafanya nini.

Kwa hiyo ilibidi nirudi Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam na pale (vitani kuelekea ndani ya Uganda) nikamkabidhi Msuguri, mimi nakamwambia nakwenda (makao makuu) kukufanyia kazi ya kuandaa vifaa, wewe kazi yako ni kwenda ndani kumwadhibu Idi Amin. Nikarudi makao makuu nilikuwa na mtu mmoja alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi, Kanali Bakari, basi tukafanya kazi na Bakari, tunkaenda hadi nchi za nje kutafuta nguvu…. zana za kivita.

Wako marafiki walitusaidia, sina sababu ya kuwataja sana lakini kati ya nchi rafiki tulizokwenda ni pamoja na Urusi, China, Korea na Bulgaria. Ikabidi tukusanye vifaa na ndipo hapo wananchi walichangia mambo mengi sana, wapo waliojitolea magari yao, vyakula, mifugo kama ng’ombe ili kuwawezesha wapiganaji wetu kule mstari na hatimaye Msuguri akuvuka mpaka akiwa na uhakika wa nguvu za kutosha na uangalizi huku nyuma anakotoka.

Raia Mwema: Kwa wakati huo wewe ndiye uliyekuwa makao makuu Dar, sasa uliwezaje kudhibiti link (viunganishi vya taarifa) za silaha mlizopata kutoka nje ya nchi?

Jenerali Kiwelu: Kwanza wakati nikiwa pale Kagera tulikuwa tumedhibiti sana uvujaji wa taarifa. Unajua kuna mkutano mmoja mkubwa wa kimataifa ulikuwa unaendelea pale Arusha uliokuwa umehusisha nchi nyingi huku vita pia ikiendelea na hao washiriki wa mkutano hawakujua chochote kilichokuwa kikiendelea nilidhibiti uvujaji wa taarifa, viongozi wengine tuliwapa amri maalumu hakuna kufika kwenye eneo la vita na wala kupewa taarifa yoyote, ni kama tulivyokuwa tunapambana kuwasaidia kule Msumbiji siku moja tukakuta mzee mmoja wa kizungu kule Tunduru anayo redio ameijichimbia ndani, kumbe alikuwa anawasiliana kwa maana ya kupeleka taarifa, tukamkamata. Hata pale Karagwe, tulikuwa na watu fulani pale ambao ni kanisa fulani sitaki kuwataja nao pia walikuwa na redio ya mawasiliano, ukiona utafikiri mtu anapiga kinanda kumbe anapeleka taarifa, kwa hiyo tukafunga njia zote za mawasiliano, nikasema hakuna mawasiliano ya aina yoyote na taarifa zozote kwenda Ikulu nitapeleka, tulihakikisha taarifa hazivuji vinginevyo tusingeweza kuvuka pale.

Raia Mwema: Vipi kuhusu Yoweri Museven (Rais wa sasa wa Uganda), alikuwa sehemu ya mapambano?

Jenerali Kiwelu: Museven yeye alitokea huku nyuma kapitia Karagwe kalala kijijini pale wakati Mayunga amekwishavuka mpaka, akaungana na Mayunga, ukweli ni kwamba Jeshi la Tanzania na chini ya Luteni Jenerali Mayunga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kupita Mbarara na kutoka hapo kuelekea Kampala, na wengine wakapita Minziro kwenda kuungana kule. Museven hakuwa na jukumu la kuongoza ni kama alisaidia mambo kadhaa yakiwamo masuala ya taarifa.

Raia Mwema: Vipi kuhusu uteuzi wako kuwa mkuu wa mkoa?

Jenerali Kiwelu: Baada ya vita, tukawapokea vijana kutoka Uganda pale Bunazi, nikafanya kazi ya kuwasambaza na kuwarudisha kule walikotoka, wengine Ruvuma, Kigoma na maeneo mengine ya nchi. Tukahakikisha wamerudi na kupewa haki zao.

Baada ya kumaliza pale Bunazi, nikarudi Dar es Salaam kwenye kitengo changu cha Mnadhimu Mkuu, sasa makamanda wote wakawa wamerejea kutoka vitani. Ikabidi sasa jeshi lipangwe upya….unajua watu walikwishaonja kutoa roho za watu huwezi kucheza nao hivi hivi, ikabidi sasa tupangane upya.

Namna gani jeshi litakavyoendeshwa na kwa hiyo, Amiri Jeshi Mkuu akapanga upya…akasema sasa wewe bwana umemaliza kazi hii nakushukuru…sasa nataka kukupa kazi nyingine…nikamwambia sawa, nipo tayari kwa kazi yoyote, akaniambia utakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nikamwambia naenda lakini hii kazi sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na mimi nikiona kuna tatizo nitakuja. Kwa hiyo nikaenda zangu Tanga ndipo wakati huo yakafanyika mabadiliko, Twalipo akatoka pale akawa Waziri wa Ulinzi, Msuguri akawa Mkuu wa Majeshi halafu na Jenerali Kombe akawa Mnadhimu Mkuu, tukaendelea.

Raia Mwema: Nini hasa unachojivunia katika wadhifa wako wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga?

Jenerali Kiwelu: Tanga kuna mambo mengi. Lakini moja kubwa ni kwamba pale Tanga wale Waswahili wangu wa Tanga ni wavivu, hawakuwa watu wa maendeleo. Sasa walikuwa wanakaa pale kwenye nyumba zao za nyasi mjini, nikawaambia sikilizeni hatuwezi kuishi hivi…mtu lazima afanye kazi na mjiwekee kipato na mtengeneze nyumba.

Wakauliza tunatengenezaje na hatuna mashamba kwa ajili ya kutupatia kipato? Nikafanya uamuzi, nikaenda barabara ya kuelekea Muheza kuna mashamba ya mkonge pale na hapakuwa na mtu anayelima, nikasema nitachukua haya mashamba na wala sikuuliza ni ya nani. Nikawaambia nyie mtakwenda kulima pale na kutakuwa na mabasi asubuhi na jioni ya kwenda na kurudi shambani, na kwamba wakishavuna watapata chakula lakini nikataka watengeneze nyumba zao na watoto wasome kwa kipato watakachopata.

Nikamwambia ofisa husika apime viwanja, lakini nikawaambia nyumba zao wasizivunje isipokuwa wajenge kuta kwa kuzizunguka na baada ya kufika hatua ya kupaua, wanaweza kuvunja nyumba za ndani yake za nyasi, ndivyo nyumba nyingi za Tanga zilivyojengwa kwa wakati huo.

Nilikaa pale kwa miaka nadhani mitatu tangu mwaka 1980 kisha nikahamishiwa Rukwa ambako nako pia kuna mambo mengi niliyofanya. Uzuri wa Rukwa watu wa kule ni wachapa kazi lakini tatizo lao walikuwa wanachapa kazi bila utaratibu. Nikawaambia msilime tu mahindi ya kutosha nyumba yako tu bali limeni kwa malengo ya kupata kipato. Nikawataka walime kwa utaratibu, wajue masuala ya mbegu, maandalizi ya shamba. Lakini haikuwa kazi rahisi kwa sababu ilibidi tutengeneze kitu kama shule kijijini kwa ajili ya kumfundisha mtu kulima, kuandaa shamba, kupanda, kupalilia hadi kuvuna, ni miezi minne…watano amevuna ameweka kwenye kihenge, anakuwa amefaulu. Sasa mtu anapokuwa anajifunza kulima alikuwa akijifunza kilimo cha kisasa, kupanda kwa mistari, kutumia mbolea, kutumia dawa za kudhibiti wadudu na baada ya kuvuna, ajue namna ya kutunza mazao.

Sasa katika kuandaa mashamba wengine walikuwa wanatumia majembe madogo ya kukokotwa kwa ng’ombe na wengine majembe ya mkono, uongozi ngazi ya mkoa ilibidi tufanye utaratibu na tulifanikwa kwenda kununua majembe kutoka Zimbabwe ya kukokota kwa ng’ombe na ya kupandia. Niliomba fedha nikapewa za mbegu ambazo kule hakuna, nikaagiza mbegu kutoka Kenya lakini hazikuwa zinatosha, nikaenda kwenye wizara (ya kilimo) natafuta mbegu nako hakuna. Lakini nikaona sio siku zote kwenda kutafuta mbegu, nikaanzisha shamba la mbegu eneo la Mlundikwa, mwaka wa pili tukawa sasa tunaweza kupata mbegu zetu na tukajua namna ya kuziweka katika madaraja ya ubora.

Sasa baada ya kuwa na uhakika wa mbegu tukaingia hatua ya matumizi ya majembe ya ng’ombe, tulipomaliza mwaka wa kwanza na wa pili, ule mwaka wa tatu tukafaulu na kupata mazao mengi, maana nia yangu pale ilikuwa ni kupata mavuno mengi ili kushindana na wenzangu wa mikoa mingine ya kilimo, na ikibidi hata kuwazidi lakini kwa manufaa ya watu wangu hasa katika kuongeza kipato chao mara dufu au zaidi.

Raia Mwema: Kwa hiyo kuwapo kwako Rukwa kulisababisha mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa mingine mikubwa ya kilimo kama Mbeya, Ruvuma na Iringa?

Jenerali Kiwelu: Kwanza mimi nikiwa kule nilijua Mbeya ambako nilikuwa napita pale, Iringa na Ruvuma ndio iliyokuwa mikoa mitatu mikubwa na mashuhuri kwa kilimo, ikiitwa “The Big Three”. Nikasema hawa hawawezi kuwa Big Three na mimi napita mikoa yao, changamoto yangu ya kwanza nikasema lazima niingie pale kwenye orodha ya Big Three ili tuwe Big Four.

Raia Mwema: Baadaye ulipelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera, hali ilikuwaje kule?

Jenerali Kiwelu: Unajua ule Mkoa wa Kagera unafafana hali ya hewa na mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro na Arusha, mimi sehemu ya asili ni Kilimanjaro ambako mazao ni pamoja na kahawa na migomba kule nako mazao ni hayo hayo, tofauti iliyokuwapo ni kwamba kule Kilimanjaro tulikuwa tunalima kahawa aina ya Arabika sasa Kagera ilikuwa nafasi yangu ya kujifunza kilimo cha kahawa aina ya Robusta, ikawa lazima niwainue wale wakulima tuone tunafanya vizuri zaidi. Sasa kule kwa sababu wengi ni wabishi kweli kweli wanataka lazima waone vitendo kwa mfano, ikabidi niwe na shamba la mfano na hata sasa baada ya kustaafu bado naendelea na kilimo kwenye shamba langu.

Raia Mwema: Kuna wakati uliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania katika moja ya nchi za nje. Hali ilikuwaje?

Jenerali Kiwelu: Sikwenda, na nafasi hiyo haikufutwa. Pengine nieleze niliteuliwaje. Nilipoteuliwa kwenda ubalozi na Rais Mwinyi nikaenda kusoma chuo hapo cha diplomasia, nikajiandaa kabisa kuondoka lakini nadhani kuna taratibu nyingine hazikuwa zimekamilika, hiyo ndio njia ninayoweza kuiweka kwamba taratibu hazikukamilika.

Nakumbuka nilikuwa Rukwa (Mkuu wa Mkoa). Niliitwa kutoka Rukwa nikarudishwa Makao Makuu ya Jeshi kuwa Mnadhimu Mkuu kwa mara ya pili, nikakaa pale …. katikati bwana mkubwa (Rais) akasema sasa uende ukanisaidie kazi ya ubalozi huko Italia na wakati huo nikawa nimestaafu jeshini. Kwa hiyo sikwenda ubalozini na Rais Mwinyi akaniteua kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Raia Mwema: Kuna mizengwe imefanyika hadi ukashindwa kwenda ubalozini?

Jenerali Kiwelu: Hakuna mizengwe, maana Rais hawezi kufanya mizengwe. Kwa hiyo nilikwenda Tabora kisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na baadaye Kagera, ambako nikastaafu rasmi nikawa nalima kahawa, miwa na kufuga ng’ombe pale.

Raia Mwema: Lakini hili la kutokwenda kuwa balozi lilikusononesha kidogo?

Jenerali Kiwelu: Unajua mambo haya yanatokea kama ilivyotokea juzi kwa waziri mmoja ambaye alimteua mtu kuwa mkurugenzi wa shirika fulani na baada ya saa tatu hivi uteuzi ule ukatenguliwa kwa sababu taratibu hazikuwa zimekamilika.

Raia Mwema: Je, ni kweli kwamba umaarufu katika jeshi unaweza kuwakwaza viongozi pia? Mfano wewe, Jenerali Mayunga na wengine wengi.

Jenerali Kiwelu: Yaani wewe askari unakuwa maarufu? Unajua kwenye jeshi askari ama maofisa wanaweza kuonyesha ukaribu kwa mtu fulani kwa sababu fulani, kwamba huyu anaweza kutufikisha mahala fulani, hiyo haina maana kwamba yeye ndiye amefanya vitendo vya kujipa umaarufu, hapana. Hao ndio wameona wanamtaka huyu anaweza kwenda nao, kwa mfano huwezi kumpeleka askari kwenye mapambano wakati akiwa na njaa, lakini wewe kamanda kama unahakikisha askari huyu anakula na anapata mahitaji yake, hiyo si kwamba umejipendekeza kwao bali unatekeleza wajibu wako ili nao watekeleze wajibu wao, ni lazima wataonyesha kukuhitaji tu.

Ni tofauti na mtu kujipendekeza eti kwamba huyu ni rafiki yangu … hakuna rafiki. Askari ni askari, amefundishwa namna ya kutii amri na wewe umefundishwa namna ya kuongoza, ni suala la kutimiza wajibu. Ukitaka kufanya vitendo ambavyo ni kwa kujionyesha, kwamba unapendelea watu fulani ujue kuna wengine wanakutazama kwa umakini, haiwezekani.

Raia Mwema: Unazungumziaje utendaji wa Rais Magufuli?

Jenerali Kiwelu: Mheshimiwa Magufuli ana sifa nyingi sana hana blaa blaa ni mtendaji, akiamua jambo anaamua on principle (kwa misingi) na atalisimamia hivyo, huwezi kumwondoa hapo. Kama anasema hili ni uchafu ni uchafu tu na anazo sababu za kusema hivyo.”
“Mimi namfahamu kiasi kwa kipindi cha miaka kama tisa, nimekuwa Kagera kwa miaka yote kama Mkuu wa Mkoa naye akiwa mbunge na mjumbe wa RCC (Kamati ya Maendeleo ya Mkoa) na pia nimekuwa nikifanya ziara kwenye wilaya yake, tunaendesha miradi mbalimbali. Kwa hiyo yule kwa kweli akiamua jambo …akisema ujue hawezi kurudi nyuma, hana ahadi za blaa blaa.”
“…ni mwanasayansi anafanya utafiti kwanza ili kujua hili jambo linatekelezeka na kisha anasimama hapo hapo kuhakikisha linatekelezeka.”

“Hawa watu wengine, unajua mimi bahati mbaya sijui namna ya kutukana sana nasema watu wengine hawa wanaosema kwamba mwendo wake huu si wa kudumu, mimi siwezi kuwaita wajinga, nasema tu ni watu wasiojua kutazama mambo. Magufuli hawezi kurudi nyuma amefanya kazi kwa miaka 20 someni historia yake, wewe ukimweka kwenye samaki atashughulika na samaki, atashughulika mpaka aone lengo liliowekwa linatekelezwa.”

Raia Mwema: Unadhani inastahili pia katika vyombo vya usalama akaingilia kurekebisha mambo kidogo?

Jenerali Kiwelu: Mimi sijui kama vyombo vya usalama ambavyo haviendi vizuri, lakini ninachojua ni kwamba katika nchi hii tuna vyombo vya usalama vilivyowekwa kumsaidia kiongozi mkuu wa nchi kuendesha shughuli zake na hivi vyombo ni macho na masikio ya huyu kiongozi, kwamba anapewa ushauri, sasa ukikaa na kutafakari sasa hivi hii hali ya kutumbua majipu yote haya (mengi) unajiuliza, hawa watu walikuwa wapi? Wale waliokuwa macho na masikio ya rais walikuwa wapi? Mimi siwezi kutoa jibu ila ninyi tazameni tu.

Raia Mwema: Nini wito wako kwa Watanzania?

Jenerali Kiwelu: Watanzania wa mwaka huu tunaosema ni mwaka wa mabadiliko tufanye kazi tu. Watanzania wote popote walipo ni lazima kuisaidia serikali iliyopo madarakani, wana wajibu huo, mtu akishakuwa rais anakuwa rais wa wote, hakuna CUF, CCM, Chadema au nini. Wote hawa sasa njia yao ni moja ya kumsaidia huyu rais atekeleze wajibu wake kwa miaka mitano, ili kuhakikisha nchi hii inasonga kutoka hatua moja kwenda nyingine.
 
  • Asema katika Vita ya Kegara udhibiti wa mawasiliano na taarifa ulikuwa wa kiwango cha
Raia Mwema: Hali ilikuwaje kule eneo la mapambano wakati wa vita ya Kagera?
Jenerali Kikwelu: Kazi ilikuwa ngumu sana. Maana vijana wangu waliokuwa kule mbele, wale askari wa JWTZ walikuwa katika nusu morali, maana ukishatoka kwenye mstari wa mbele ukarudi nyuma morali ya vita inapungua.

Kwa hiyo kazi ya kwanza ilikuwa kuwajenga kisaikolojia. Kazi ya pili ilikuwa ni kupata reinforcement (kuongeza nguvu) kazi ambayo niliyomwachia Ernest Mwita Kiaro, hata CDF naye alikuja akakaa mahala fulani pale Bukoba (jirani), kwa hiyo Dar es Salaam tulimpa kazi Mwakalindile ndiye aliyekuwa anakaimu kama Chief of Staff, halafu Kiaro, chifu wa mgambo kazi yake ilikuwa kukusanya mgambo wote nchini, akina Mwakalindile ni kukusanya JKT, Polisi na Magareza, wote walikuja kule.

Ninaposema kulikuwa na changamoto kubwa sana ni kwamba hawa askari hata siku moja hawakuwahi kuwa eneo la vita ama eneo la mafunzo ya kivita kwa pamoja. Kwa hiyo, ilikuwa kazi kubwa, ndiyo maana ikatuchukua muda pale kabla hatujaruka daraja, ilikuwa ni lazima nifanye mafunzo ya pamoja ili kuwaweka watu (askari kutoka Magereza, Polisi, Mgambo na JKT) waweze kufanya kazi pamoja.

Lengo ilikuwa kuondoa fikra za kitabaka vitani, kuachana na mambo ya huyu mgambo au JKT. Kwa hiyo nilianzisha range ya kupiga silaha, mtu unampa risasi kumi anapiga zote wash out (anakosa kulenga shabaha), maana sisi (jeshini) tuna kitu kinaitwa bull, inner, outer n.k… sasa huyu unampa risasi zote anapiga wash out, tunampa nyingine, akipiga ile target namwambia umepiga bega (target hasa ni kifuani kwenye moyo au kichwani) sasa wakati mwingine ukimpa risasi tano… mbili anapiga ndani, nikasema sasa wameiva.

Kwa hiyo ilikuwa ni mafunzo ya msingi. Kwa mfano, ukiwa porini na ndege ya adui inakuja ufanye nini.

Unaulizwa ukiona ndege ya adui inatoka kule wewe unakwenda wapi? Namna gani mnaweza kusonga mbele, mnajihami vipi na namna gani mnaweza kupumzika kwa sababu askari hawezi kupumzika chini ya kivuli cha mti. Sasa baada ya mafunzo hayo ya pamoja, tukaridhika askari wetu wameiva, tukaanza kusonga mbele kutoka Katoro hadi tukafika karibu na mpakani, tukaweka kambi ambayo mpaka leo ipo pale, nyuma ya Mtukula.

Raia Mwema: Labda ungeeleza kuhusu Daraja la Kagera kushambuliwa na adui?

Jenerali Kiwelu: Daraja hili wakati nimefika tu, kutoka kupewa ile amri (ya kwenda vitani)… nimefika Kaboya, siku hiyo hiyo jioni nikatoka kwenda kutazama daraja. Nikafika darajani upande wa kulia kama unakwenda Mtukula umbali wa kilomita moja, nikaliona daraja ambalo baada ya dakika 15 nikiwa pale likalipuka, kwa hiyo sikuweza kuwahi kuweka askari pale darajani.

Wakati nafika pale na mtu mmoja anaitwa Kanali Kitete tunatazama…nataka sasa kufanya mbinu namna gani nitavuka daraja ili majeshi yangu yakae upande mwingine.

Basi nikarudi zangu Kaboya kwa ajili ya kuanza kufanya mkakati mwingine maana pale daraja limekwishavunjwa, nikaripoti daraja limevunjwa…hakuna daraja kuanzia sasa. Ndipo tukaanza mipango mingine kuhusu daraja, tukaleta madaraja ya muda na mtu mmoja anaitwa Brigedia Rajabu ndiye aliyekuja na vifaa hivyo kutoka kikosi chetu cha uhandishi na tukamweka sehemu ya umbali wa kama kilomita tano kutoka kwenye daraja, ndipo alipofanya mafunzo yake ili baadaye kufunga daraja la muda.

Raia Mwema: Ilichukua muda gani hadi kufanikisha daraja hilo la muda?

Jenerali Kiwelu: Unajua kuna wanazungumza kwa ushabiki mambo ya vita tu wakati hawajui chochote kuhusu vita, watu hawa mimi nawaita majitu, hawajui maana ya vita. Wapo wengine wanafikiri jeshi hii la Tanzania lilikuwa tayari kwamba unakwenda tu kwenye vita, sasa ukiwaambia kwamba jeshi hili tulipokwenda kwenye vita tulikuwa na mchanganiyo wa watu wote hawa, halafu pia kuleta vifaa vya kuvuka daraja, kuwafundisha namna ya kuweka daraja, kuleta vifaru, ndipo wataona ugumu wa kazi iliyokuwapo.

Pale ni lazima uwe na nguvu ya kutosha kuhakikisha kwamba mkiruka (daraja) hakuna kurudishwa nyuma. Kama nilivyotangulia kusema wale askari wetu waliokuwa kule awali, walikuwa wachache na walivurumishwa na adui kiasi cha morali yao kuwa chini kivita, kwa hiyo ilikuwa ni lazima nihakikishe sasa watu wangu ni imara, vifaa viko.

Tulikuwa tunafanya mipango na ukaguzi pamoja na makamanda wangu, akina Jenerali Marwa, Jenerali Luhanga, Mayunga, Walden… tunakwenda hadi tunafika pale kwenye daraja kwa sababu Idi Amin alirudisha majeshi yake (Uganda) akiamini kazi imekwisha. Sasa tulikuwa na makamanda wangu hao tunakwenda pale kupanga mikakati, lakini, swali kwamba wapi tupite (kuvuka daraja) na lini sikuwaambia.

Hakuna mtu aliyejua hata Edward Sokoine (aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Mwalimu Nyerere) alikuja akaniuliza …. sasa General nafikiri tumechelewa sana kuruka (daraja), sasa unaruka lini na unapitia wapi?

Nikamwambia hiyo ni siri ya kijeshi… akasema hata mimi? Nikamwambia ndiyo mzee. Kwa hiyo mimi nilikuwa napita kando ya ule mto kwa gari hadi Murongo, halafu watu wanapiga mabomu kila sehemu lakini hawajui tunaruka wapi kupitia wapi.. .tuliweka watu (askari) hadi eneo la Kakunyu huku Bukoba Vijijini, kwa hiyo kuna ambao walijua tunaruka kupitia huko. Hatimaye nikaona sehemu ya kuruka ni pale pale walipovunja (daraja), lakini sikuwaambia wapiganaji wetu.

Sasa imefika siku ya kuruka, ndani ya saa 24. Nikawaita makamanda wangu nikawaambia sasa inabidi turuke kwenda kumshambulia adui, vifaa na kila kitu tayari, na askari kama tulivyofanya mafunzo wako tayari. Makamanda wakasema tunangoja tu amri yako, nikasema amri itatoka, wakauliza na kutaka niwaambie tunaruka kupitia eneo gapi, nikasema nitawaambia.

Ilipofika saa tano usiku nikawaambia makamanda… Marwa utakuwa katikati, Mayunga ukiruka tu unakwenda kushoto kuelekea eneo la Mbarara, Walden ukiruka tu unaelekea eneo la Minziro, Luhanga ukiruka tu unafuata njia ya Marwa halafu makamanda wengine watakuwa tayari kusubiri lolote (reserve). Baada ya maelekezo hayo nikawataka waende kuwaambia askari wao kwamba tunaruka leo (usiku huo), nikamwita Mhandisi Mkuu Rajabu na kumwambia utatandaza daraja lako (juu ya mto) saa nane usiku…akafanya kazi hiyo.

Saa nane usiku mpaka kufika saa tisa kuelekea saa 10 (takriban saa mbili hivi mfululizo) vikosi vikaanza kuruka kwa mujibu wa amri ya operesheni (operation order) ilivyotamkwa. Ilikuwa bahati mbaya nilipoteza askari mmoja tu pale wakati wa kuvuka daraja.

Baada ya hapo tulifanya mashambulizi, kazi ya kwanza ilikuwa ni kukamata eneo. Nimeeleza kazi niliyopewa nilitakiwa kurudisha heshima ya nchi hii na heshima ya nchi ni kurudisha mipaka yetu pale ilipokuwa awali na hivyo tukahakikisha tumefika Mtukula, wengine wamefika Minziro na wengine mpakani na Uganda kule.

Sasa jukumu la msingi la kurejesha mipaka ya nchi likawa limekamilika na Rais Julius Nyerere akaja kule na akasimama eneo lenye kilima pale na tukamweleza kwamba sasa mzee kazi ya kwanza uliyotutuma tumeimaliza, mipaka yetu sasa iko salama, akasema vizuri lakini huyu “mshenzi” huyu ametuharibia mambo mengi sana si bado yuko kule (nchini mwake), basi kazi bado haijakwisha.

Ndipo tukaingia hatua ya pili, maana sehemu ya kwanza ya ukombozi wa nchi yetu ikawa imekwisha ikafuata hatua hiyo ya pili ambayo ni kumwadhibu adui.

Raia Mwema: Je, baada ya kazi hiyo ya kwanza kukamilika ulirejeshwa kwenye nafasi ya Mnadhimu Mkuu (Chief of Staff)?

Jenerali Kiwelu: Pale kilichofanyika ni kwamba baada ya kumaliza ile kazi ya awali, tukaingia sasa kazi ya kuandaa na kutekeleza operesheni ya kuvuka mpaka ambayo ni tofauti na opereshani ya kumwondoa adui nyumbani kwako.

Sasa unakwenda nyumbani kwake lazima uwe na mkakati, sambamba na nguvu ya kutosha kwenda kwake, kwa hiyo rais ikabidi afanye utaratibu wa kumtafuta kamanda wa kuingia Uganda, mimi si ndiye niliyekuwa Chief of Staff na mkuu wa majeshi akiwa Twalipo ambaye naye hayuko makao makuu, kwa maana hiyo akiwa huku mbele (vitani) kule makao makuu hakuna maandalizi yoyote, nani anaanda nini… nani anafanya nini.

Kwa hiyo ilibidi nirudi Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam na pale (vitani kuelekea ndani ya Uganda) nikamkabidhi Msuguri, mimi nakamwambia nakwenda (makao makuu) kukufanyia kazi ya kuandaa vifaa, wewe kazi yako ni kwenda ndani kumwadhibu Idi Amin. Nikarudi makao makuu nilikuwa na mtu mmoja alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi, Kanali Bakari, basi tukafanya kazi na Bakari, tunkaenda hadi nchi za nje kutafuta nguvu…. zana za kivita.
Wako marafiki walitusaidia, sina sababu ya kuwataja sana lakini kati ya nchi rafiki tulizokwenda ni pamoja na Urusi, China, Korea na Bulgaria. Ikabidi tukusanye vifaa na ndipo hapo wananchi walichangia mambo mengi sana, wapo waliojitolea magari yao, vyakula, mifugo kama ng’ombe ili kuwawezesha wapiganaji wetu kule mstari na hatimaye Msuguri akuvuka mpaka akiwa na uhakika wa nguvu za kutosha na uangalizi huku nyuma anakotoka.
Raia Mwema: Kwa wakati huo wewe ndiye uliyekuwa makao makuu Dar, sasa uliwezaje kudhibiti link (viunganishi vya taarifa) za silaha mlizopata kutoka nje ya nchi?
Jenerali Kiwelu: Kwanza wakati nikiwa pale Kagera tulikuwa tumedhibiti sana uvujaji wa taarifa. Unajua kuna mkutano mmoja mkubwa wa kimataifa ulikuwa unaendelea pale Arusha uliokuwa umehusisha nchi nyingi huku vita pia ikiendelea na hao washiriki wa mkutano hawakujua chochote kilichokuwa kikiendelea nilidhibiti uvujaji wa taarifa, viongozi wengine tuliwapa amri maalumu hakuna kufika kwenye eneo la vita na wala kupewa taarifa yoyote, ni kama tulivyokuwa tunapambana kuwasaidia kule Msumbiji siku moja tukakuta mzee mmoja wa kizungu kule Tunduru anayo redio ameijichimbia ndani, kumbe alikuwa anawasiliana kwa maana ya kupeleka taarifa, tukamkamata.

Hata pale Karagwe, tulikuwa na watu fulani pale ambao ni kanisa fulani sitaki kuwataja nao pia walikuwa na redio ya mawasiliano, ukiona utafikiri mtu anapiga kinanda kumbe anapeleka taarifa, kwa hiyo tukafunga njia zote za mawasiliano, nikasema hakuna mawasiliano ya aina yoyote na taarifa zozote kwenda Ikulu nitapeleka, tulihakikisha taarifa hazivuji vinginevyo tusingeweza kuvuka pale.

Raia Mwema: Vipi kuhusu Yoweri Museven (Rais wa sasa wa Uganda), alikuwa sehemu ya mapambano?

Jenerali Kiwelu: Museven yeye alitokea huku nyuma kapitia Karagwe kalala kijijini pale wakati Mayunga amekwishavuka mpaka, akaungana na Mayunga, ukweli ni kwamba Jeshi la Tanzania na chini ya Luteni Jenerali Mayunga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kupita Mbarara na kutoka hapo kuelekea Kampala, na wengine wakapita Minziro kwenda kuungana kule. Museven hakuwa na jukumu la kuongoza ni kama alisaidia mambo kadhaa yakiwamo masuala ya taarifa.

Raia Mwema: Vipi kuhusu uteuzi wako kuwa mkuu wa mkoa?

Jenerali Kiwelu: Baada ya vita, tukawapokea vijana kutoka Uganda pale Bunazi, nikafanya kazi ya kuwasambaza na kuwarudisha kule walikotoka, wengine Ruvuma, Kigoma na maeneo mengine ya nchi. Tukahakikisha wamerudi na kupewa haki zao.

Baada ya kumaliza pale Bunazi, nikarudi Dar es Salaam kwenye kitengo changu cha Mnadhimu Mkuu, sasa makamanda wote wakawa wamerejea kutoka vitani. Ikabidi sasa jeshi lipangwe upya….unajua watu walikwishaonja kutoa roho za watu huwezi kucheza nao hivi hivi, ikabidi sasa tupangane upya.

Namna gani jeshi litakavyoendeshwa na kwa hiyo, Amiri Jeshi Mkuu akapanga upya…akasema sasa wewe bwana umemaliza kazi hii nakushukuru…sasa nataka kukupa kazi nyingine…nikamwambia sawa, nipo tayari kwa kazi yoyote, akaniambia utakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nikamwambia naenda lakini hii kazi sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na mimi nikiona kuna tatizo nitakuja. Kwa hiyo nikaenda zangu Tanga ndipo wakati huo yakafanyika mabadiliko, Twalipo akatoka pale akawa Waziri wa Ulinzi, Msuguri akawa Mkuu wa Majeshi halafu na Jenerali Kombe akawa Mnadhimu Mkuu, tukaendelea.

Raia Mwema: Nini hasa unachojivunia katika wadhifa wako wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga?

Jenerali Kiwelu: Tanga kuna mambo mengi. Lakini moja kubwa ni kwamba pale Tanga wale Waswahili wangu wa Tanga ni wavivu, hawakuwa watu wa maendeleo. Sasa walikuwa wanakaa pale kwenye nyumba zao za nyasi mjini, nikawaambia sikilizeni hatuwezi kuishi hivi…mtu lazima afanye kazi na mjiwekee kipato na mtengeneze nyumba.

Wakauliza tunatengenezaje na hatuna mashamba kwa ajili ya kutupatia kipato? Nikafanya uamuzi, nikaenda barabara ya kuelekea Muheza kuna mashamba ya mkonge pale na hapakuwa na mtu anayelima, nikasema nitachukua haya mashamba na wala sikuuliza ni ya nani.

Nikawaambia nyie mtakwenda kulima pale na kutakuwa na mabasi asubuhi na jioni ya kwenda na kurudi shambani, na kwamba wakishavuna watapata chakula lakini nikataka watengeneze nyumba zao na watoto wasome kwa kipato watakachopata.

Nikamwambia ofisa husika apime viwanja, lakini nikawaambia nyumba zao wasizivunje isipokuwa wajenge kuta kwa kuzizunguka na baada ya kufika hatua ya kupaua, wanaweza kuvunja nyumba za ndani yake za nyasi, ndivyo nyumba nyingi za Tanga zilivyojengwa kwa wakati huo.

Nilikaa pale kwa miaka nadhani mitatu tangu mwaka 1980 kisha nikahamishiwa Rukwa ambako nako pia kuna mambo mengi niliyofanya. Uzuri wa Rukwa watu wa kule ni wachapa kazi lakini tatizo lao walikuwa wanachapa kazi bila utaratibu. Nikawaambia msilime tu mahindi ya kutosha nyumba yako tu bali limeni kwa malengo ya kupata kipato. Nikawataka walime kwa utaratibu, wajue masuala ya mbegu, maandalizi ya shamba.

Lakini haikuwa kazi rahisi kwa sababu ilibidi tutengeneze kitu kama shule kijijini kwa ajili ya kumfundisha mtu kulima, kuandaa shamba, kupanda, kupalilia hadi kuvuna, ni miezi minne…watano amevuna ameweka kwenye kihenge, anakuwa amefaulu. Sasa mtu anapokuwa anajifunza kulima alikuwa akijifunza kilimo cha kisasa, kupanda kwa mistari, kutumia mbolea, kutumia dawa za kudhibiti wadudu na baada ya kuvuna, ajue namna ya kutunza mazao.

Sasa katika kuandaa mashamba wengine walikuwa wanatumia majembe madogo ya kukokotwa kwa ng’ombe na wengine majembe ya mkono, uongozi ngazi ya mkoa ilibidi tufanye utaratibu na tulifanikwa kwenda kununua majembe kutoka Zimbabwe ya kukokota kwa ng’ombe na ya kupandia. Niliomba fedha nikapewa za mbegu ambazo kule hakuna, nikaagiza mbegu kutoka Kenya lakini hazikuwa zinatosha, nikaenda kwenye wizara (ya kilimo) natafuta mbegu nako hakuna.

Lakini nikaona sio siku zote kwenda kutafuta mbegu, nikaanzisha shamba la mbegu eneo la Mlundikwa, mwaka wa pili tukawa sasa tunaweza kupata mbegu zetu na tukajua namna ya kuziweka katika madaraja ya ubora.

Sasa baada ya kuwa na uhakika wa mbegu tukaingia hatua ya matumizi ya majembe ya ng’ombe, tulipomaliza mwaka wa kwanza na wa pili, ule mwaka wa tatu tukafaulu na kupata mazao mengi, maana nia yangu pale ilikuwa ni kupata mavuno mengi ili kushindana na wenzangu wa mikoa mingine ya kilimo, na ikibidi hata kuwazidi lakini kwa manufaa ya watu wangu hasa katika kuongeza kipato chao mara dufu au zaidi.

Raia Mwema: Kwa hiyo kuwapo kwako Rukwa kulisababisha mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa mingine mikubwa ya kilimo kama Mbeya, Ruvuma na Iringa?

Jenerali Kiwelu: Kwanza mimi nikiwa kule nilijua Mbeya ambako nilikuwa napita pale, Iringa na Ruvuma ndio iliyokuwa mikoa mitatu mikubwa na mashuhuri kwa kilimo, ikiitwa “The Big Three”. Nikasema hawa hawawezi kuwa Big Three na mimi napita mikoa yao, changamoto yangu ya kwanza nikasema lazima niingie pale kwenye orodha ya Big Three ili tuwe Big Four.

Raia Mwema: Baadaye ulipelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera, hali ilikuwaje kule?

Jenerali Kiwelu: Unajua ule Mkoa wa Kagera unafafana hali ya hewa na mikoa kama Mbeya, Kilimanjaro na Arusha, mimi sehemu ya asili ni Kilimanjaro ambako mazao ni pamoja na kahawa na migomba kule nako mazao ni hayo hayo, tofauti iliyokuwapo ni kwamba kule Kilimanjaro tulikuwa tunalima kahawa aina ya Arabika sasa Kagera ilikuwa nafasi yangu ya kujifunza kilimo cha kahawa aina ya Robusta, ikawa lazima niwainue wale wakulima tuone tunafanya vizuri zaidi. Sasa kule kwa sababu wengi ni wabishi kweli kweli wanataka lazima waone vitendo kwa mfano, ikabidi niwe na shamba la mfano na hata sasa baada ya kustaafu bado naendelea na kilimo kwenye shamba langu.

Chanzo Raia Mwema.

Maoni Yangu

Tumeeona jinsi Generala Kiwelu alimvyomnyima Sokoine taarifa za vita kwa kumwambia ni siri ya kijeshi na Sokoine pamoja na wadhifa aliokuwa nao aliheshimu hilo hakutaka zaidi ya jibu alilojibiwa.

Hivyo basi wanasiasa wetu wa kizazi hiki waige mfano wa Sokoine kwa kuheshimu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kutotaka kila kitu kuwa wazi ikiwemo eti kwa kuwa wao ni wabunge au wanasiasa wapo kwa niaba ya wananchi hapo watakuwa hawavitendei haki vyombo vyetu hivyo kwani vinafanya kazi kubwa ya kuhakikisha tuna kuwa na amani pamoja na uturuvu.

Hata huko Marekani na ulaya huwezi kukuta wanasiasa wanataka mambo ya jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuwekwa hadharani kama wa hapa kwetu wanavyotaka.
Kwanza nimshukuru mleta mada. Ila ametoa fundisho moja tuwakati kuna mafundisho mengi mno ya maana.
1. Uzalendo/ Utanzania- kuweza kuwafikiria watanzania wengine ili wapige hatua kadhaa za maendeleo tena kwa ubunifu.
2. Ubunifu- kusaka mbegu mpakanchi za nje, kuwaambia watu wa Tanga wajenge nyumba zao wakiwa ndani as ingekuwa vigumu kuwaambia watu wabomoe nyumba zao waanze jenga upya wangekaa wapi.
3. uchapakazi
4. Utayari wakijifunza - alipoenda mara ya kwanzakwenda kuwa Mkuu waMkoa alimwambia aliyemteua nikikoseaniambie
5. ushindani wa maendeleo.
6.Ujasiri- Alichukua mashamba ya Mikonge kwa faida ya wanannchi- ingekuwa leo tayari wanaharakati na vyama kadhaavingeanza ooh amekiuka sheria what what ili mradi utumbomtupu
7. Uthubutu- Kwenda mpaka nchi za nje kwenda kutafuta mbegu wkt viongozi wengine nje ni kuula- kwenda kufanya shopping etc.
8. Utayari- kutoka kuongoza jeshi kuwa Mkuu wa mkoa kuna utofauti lakini alikuwa tayari. Binadamu wakati mwingine tukibadilishwa wadfa tunanyongonyea etc- kumbe chapa kazi. huyu bwana ana historia nzuri hata akiifikiria inamuongezea maisha zaidi. Kumbe furaha ya moyoni sio kuwa na mali tu hata kuwa na mchango Fulani katika kufanikisha kitu Fulani inaleta furaha.
Wito: Hebu wazee kama hawa waandike vitabu kuhusu mambo mbalimbali ikiwa pamoja na mafanikio ya vita vya Kagera etc. halafu vitabu hivyo vitumike mashuleni ili kujua historia lakini kuiga utayari, uchapakazi etc wa hawa wazee wetu wa zamani waliokuwa na moyo wa kijamaa na kujituma.
Na kadhalika na kadhallika.
 
kumbe tanzania ilishirikiana na museven kumpindua idd amin dada nduli.

pia nimevutiwa jinsi vyombo vya ulinz na usalama vilivyopewa mawazir wenye ujuz na shughuli yao

..museveni just hitched a ride kwenye vita ya kumtimua amini.

..kazi kubwa na nzito ilifanywa na wa-Tz.

..tafuta habari za jinsi gani Jwtz ilivyobadilisha uongozi( regime change)wa Uganda toka kwa Iddi Amini kwenda kwa Prof.Yussuf Lule.

.halafu baadaye toka kwa Yussuf Lule kwenda kwa Lukongwa Godfrey Binaisa.
 
Story km hizi kwangu hata uandike kitabu chenye kurasa ndefu dar es saalam hadi Mafinga nitasoma kurasa zoote, kituo kwa kituo, neno kwa neno....leo nimejiuliza why napendeleaga story za aina hii?? Nimekoswa jibu.
Nakumbuka nikiwa drs la 4 niliwah kupata kitabu cha picha picha za vita hii ya Uganda na maelezo yake....Kilipewa jina la AMINI ANAKULA NYAMA ZA WATU...Had leo nakumbuka content nyinhi zilizokuwemo hasa picha za kiwanda cha sukari kagera kulipuliwa....picha za mizoga ya watanzania wazakendo waliouawa na nduli Amin kuliwa na fisi misituni...askari wakivuka mito ya tope,...nyererere rais akiwa juu ya ujenzi wa daraja.....wanajeshi wa Tz wakiwa uwanja wa vita kampala, wameteka maduka, wameteka uwanja wa jinja kama sikosei....wanajeshi wa Tz wakikaribishwa kampala na wanachi wenyeji wakishangiliwa na vingine vingi vingi vingi.......tatzo daah ukihitaj kujua zaidi unanyimwa.....unaambiwa hiyo inatosha....haya bna
 
Tanzania ya Wazalendo wetu hawa inazidi kwisha. Generation yetu inatia aibu mno. Kila nikiangalia kizazi hiki najisikia aibu sana. Nina hakika Watanzania wa sasa wangekuwa kama hawa tungekuwa mbali pengine katika level ya South Africa au zaidi.

Angalia kizazi kilichofuatia kilichofanya. Na sasa tuna kizazi kinachoinukia ambacho wanachojua ni siasa, matusi, starehe na uvivu.

Oh my poor Nation, where is your future? Your youth are wasteful and directionless. Oh! Oh! Is it the end of Era?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom