Jehanamu ipo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jehanamu ipo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamaka, Jul 30, 2010.

 1. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NAOMBENI MAJIBU WADAU KWELI JEHANAMU IPO?KAMA UPO INTERESTED ,THANK YOU.Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa, sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu. Tunasoma katika WAEBRANIA 9:27, ”Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu.“ Watu wanaofundisha kinyume na kweli ya Neno la Mungu, hufundisha kwamba mtu anapokufa, analalatu, na hakuna lolote la hukumu mara moja wakitumia maandiko yafuatayo na kuyatafsiri visivyo: MATHAYO 27:52; 1WAKORINTHO 15:20: YOHANA 11:11-14 n.k.; na pia wanasema wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama MHUBIRI 9:5. Ilivyo ni kwamba, kinachobaki kaburini ni mwili tu. Roho ya mtu huondoka na kuingia katika mwili mwingine, unaoitwa mwili wa roho Miili tuliyo nayo wanadamu kabla ya kufa, inaitwa miili ya asili. Tunasoma katika 1WAKORINTHO 15:40, 44, ”Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani, …Ikiwa uko mwili wa asili, na wa r oho pia uko.“ Mwili wa asili, ndio unabaki kaburini, lakini roho ya mtu huondoka kama tunavyosoma katika MHUBIRI 12:7, Nayo mavumbi ya nchi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.“Mwili wa asili, ndio unaobaki kaburini, na huo ndio unaotajwa kwamba umelala, haujui lolote, na hauna kumbukumbu; lakini pasipo mwili huo, mtu atamwona Mungu na kukabiliana na hukumu yake dakika ileile baada ya kufa (AYUBU 19:26). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu, mara tu baada ya kufa huchukuliwa mbinguni (LUKA 23:43; 16:22). Ikiwa ameishi na kufa katika dhambi, bila kutubu dhambi zake na kuokoka, hukumu yake mtu huyo, huwa ni kutupwa katika Jehanamu ya moto, mara tu baada ya kufa, kama yule tajiri anayetajwa katika Biblia (LUKA 16:19-24). Mbinguni ni juu (Mbingu ya tatu), lakini kuzimu au Jehanamu ya moto, ni pande za chini zanchi (2 WAKORINTHO 12:1-4; MITHALI 15:1-4; MITHALI 15:24; ZABURI 63:9; EZEKIELI 31:14. Mara mtu anapokufa, hufika kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni kuzuri, hata hivyo ikiwa jina lake haliko katika kitabu cha uzima cha mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda motoni, huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni. Hali hii wakati mwingine inaweza kuonekana katika mwili wa asili kwa kumwangalia mtu anavyotapatapa na kuhangaika sana katika kufa kwake. Kutokana na mtu asivyopenda kwenda motoni na kutaka kwenda mbinguni asikotakiwa, mtu hulazimika kukamatwa kwa nguvu na malaika wa kutisha, na kutupwa katika Jehanum ya moto; inayojulikana pia kwa jina jingine, giza la nje; kama tutakavyoona baadaye kidogo (UFUNUO 19:20; 20;10; MATHAYO 25:30). Huko motoni Jehanum kukoje? Kunatisha, nashindwa hata nikueleze vipi unielewe. Moto wa milele, hatukuwekewa wanadamu bali shetani na malaika zake (MATHAYO 25:41). Kama utakwenda huko baada ya kusoma ujumbe huu, itakuwa ni kwa sababu ya kiburi chako tu, na kushupaza shingo yako na kukataa kulitendea kazi Neno hili (MITHALI 29:1). Moto wa Jehanum siyo mahali pa mchezo kama walimu wa uongo wanavyofundisha. Waalimu hawa huwafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na kutoweshwa na kuangamizwa kabisa na ndiyo mwisho wake. Wanatumia maandiko kama MATHAYO 10:28 (kuangamizwa) na YOHANA 3:16 (kupotea). Kuangamia katika maandiko hayo haimaanishi kumalizika kabisa, bali kukabiliwa na mauti (ESTA 4:16). Mauti ya watu walioko motoni, ni mauti ya milele, kama tutakavyoona hivi punde. Kondoo akipotea, haimaanishi hayupo kabisa ila ametengwa na mchungaji (ISAYA 57:1-3). Vilevile, neno ”Kuharibu“ linapotumika kuhusiana na adhabu ya milele, halina maana ya kufanya kitu kisiwepo, bali ni kuadhibu vikali (1WAKORINTHO 3:16-17. Waalimu hawa wa uongo, pia hufundisha pia kwamba, eti watu watatoweshwa kama moshi baada ya kuunguzwa kwa kutumia andiko la ZABURI 37:20. Kutoweshwa hapa ni kutenganishwa na Mungu, kama Adamu na Hawa walivyotoweshwa na kutolewa katika bustani ya Edeni, na hivyo kutengwa na Mungu, Kwa ujumla, mafundisho yote haya yanayotokana na Shetani, yanalenga kuwafanya watu waendelee kutenda dhambi, huku wakipuuza ukweli juu ya Jehanum, kwa kuwaza kwamba watateseka dakika chache na kupotea kabisa na ndiyo mwisho. Hiyo siyo kweli.Ukweli kuhusu Jehanum ya moto ni upi basi? Sikiliza nikuambie! Jehanum ya moto, au Kuzimu, ni shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Wengi tunafahamu jinsi wanawake wanavyouchochea moto wa kuni au mkaa, kwa kuupulizia hewa kwa mdomo, au kipepeo. Sasa basi, moto wa Jehanum nao huchochewa mfululizo, ili usizimike; lakini huchochewa na pumzi ya Bwana, yaani pumzi maalum ya Mungu mwenyewe (ISAYA 14:15; 30:33). Moto wa Jehanum ni mkali sana kuliko moto wowote tunaoufahamu duniani. Moto wa gesi wa kuunganishia vyuma, unaotokana na kuwashwa mchanganyiko wa gesi ya ”Oxygen“ na ”Acetylene“, moto huu unaonekana kwa hapa duniani kwamba ni mkali. Moto huu, siyo chochote, ukilinganishwa na moto wa Jehanum. Katika karakana au viwanda vinavyotengeneza vifaa vya chuma, chuma huyeyushwa na kuwa ujiuji katika matanuru ya moto mkali unaofikia nyuzi joto 2,000 hadi 3,000 na zaidi. Moto huu unaoyeyusha vyuma na ukali wake, huo si chochote! (Kumbuka kwamba maji yaliyochemka sana hufikia nyuzi joto 100 tu!). Moto ulio katikati ya jua linalotuangaza, unafikia nyuzi joto milioni kumi . Moto wa jua nao, si chochote ukilinganishwa na moto wa Jehanum! Ukali wa moto wa Jehanum, unatisha (WAEBRANIA 10:26-27). Siyo hilo tu, moto wa duniani una rangi mbalimbali, njano, bluu, nyekundu n.k. Moto wa Jehanumu ni tofauti kabisa; Ni moto wa rangi nyeusi, unaosababisha giza na kumfanya mtu aliye motoni, awaone wenzake wachache tu wa karibu naye, hivyo hamna faraja ya kusema ”tuko wengi!“ Moto huu mweusi, ndiyo maana unaitwa ”giza la nje“ Mathayo 8:11-12, 22:13; 25:30; YUDA 1:6). Siyo hilo tu. Moto huu wa Jehanum, una meno! Hivyo una uwezo wa kuwala na kuwatafuna walioko motoni (KUMBUKUMBU 32:22; WAEBRANIA 10:26-27). Hata hivyo, pamoja na moto huu kumtafuna mtu, bado una sifa ya kumhifadhi mtu huyo na kumfanya asimalizike, kama jinsi chumvi ilivyo na uwezo wa kuizuia nyama kuharibika. Hivyo moto unamtafuna mtu wakati wote, lakini haishi na wala moto wenyewe hauzimiki. Ndiyo maana unaitwa moto wa milele (MARKO 9:43-49; MATHAYO 25:41).Moto huu wa Jehanum, huambatana na madini yanayoitwa kiberiti au kwa lugha ya kitaaluma, Sulphur.“ Kwa wale wanaofahamu kidogo somo la shule la ”Kemia,“ au ”Chemistry,“ wanafahamu kwamba madini ya ”sulphur“ yakiwashwa moto, huwa kama mpira, na hutoa harufu mbaya kama ya mayai yaliyooza. Harufu ya namna hii inafunika kuzimu yote, na watu walioko huko wanahangaika kushika pua zao, lakini hakuna jinsi! Hebu jaribu kuwaza maisha haya, ndiyo yawe ya milele, mpendwa msomaji! Siyo hilo tu! Katika moto huu, wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na kufanya matundu mengi makubwa katika miili yao, wakiingia na kutoka, kutoka ubavu hadi ubavu mwingine, kutoka kwenye tumbo hadi mgongoni n.k. Hii hufanya sura za wale walioko motoni, kuwa mbaya mno kama madude tu! (ISAYA 14:11; MARKO 9:43-49; ISAYA 66:24). Hata kama mtu alikuwa mweupe duniani, huko motoni, huwa ni mweusi tii!Moto wa milele, huitwa pia mauti ya pili (UFUNUO 21:8). Kwa nini huitwa mauti ya pili?
   
 2. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndio ipo na ukitaka kuiepuka mwamini Yesu na umfanye Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Yaani kwa kifupi OKOKA.
   
 3. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeshindwa kusoma hayo maelezo ila najibu swali tu mkuu Jehanamu ipo na mbinguni kupo hivyo ni uamuzi wako kuchagua, jaribu kuedit hiyo post yako isomeke fresh umebananisha sana maneno.
  hakuna hata HAYA(paragraph) wajameni. :director:
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Jehanamu ipo ndugu yangu!
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Jehanamu ipo, waulize Wayahudi ndugu zao waliochomwa moto na Hitler, au Warusi waliouawa na Stalin (Soma "The Gulag Achipelago" cha Alexander J. Solzhenitsyn anaelezea Jehanam ya Siberia huko)

  Zaidi ya hapo hizi stories za afterlife ni mythologies ambazo haziwezi kuwa proved. Kama unataka kuamini, amini, unaweza kuamini chochote.Kama unataka kujua huwezi kuniambia kuna mtu anaweza kuthibitisha kwamba anajua jehanam ipo.
   
 6. minda

  minda JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  1. "Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu " (matayo 5:22)
  2. hayo juu ni maneno ya yesu mwenyewe na mungu anatuambia pale mlimani yesu alipogeuka sura, "msikieni yeye"
  3. hivyo, kwa kuzingatia hoja zote 1 na 2 hapo juu, natangaza rasmi kwamba jehanamu ipo
  4. gonga hapa   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Biblia hiyo hiyo unayo i quote inatuambia kwamba jua linazunguka dunia, je unaamini pia kwamba jua linazunguka dunia ?
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kama mbingu ipo kwa nini jehanamu isiwepo? Maana mbinguni ni makao ya wema na jehanamu makao ya waovu. Kama jehanamu isingekuwepo unafikiri waovu wangekwenda wapi? Hawawezi kuchanganyikana na wema hata siku moja. Lazima wawe na mahali pao wakiongozwa na Ibilisi: wakilia na kusaga meno.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Mbingu iko wapi? Umesikia wapi wamba mbingu ipo? Ulishawahi kwenda? Ulishawahi kukutana na mtu yeyote aliyefika mbinguni huko ? Hao wema wenye makao mbinguni ushawahi kuwasiliana nao wakakueleza mbingu ikoje?
   
 10. minda

  minda JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  bilblia ni historical narative khs physical reality ambayo inatupa maana khs maisha yetu kiroho. bila shaka ni sababu hiyo ndiyo iliyomfanya joshua kuamuru jua lisimame kuizunguka dunia hadi kieleweke na kanaani; nchi ya ahadi.

  ningekuwa naishi wakati huo, ningeamini kwamba ni kweli jua linalizunguka dunia na kusimama kwa amri ya mungu kupitia kwa mtumishi wake yoshua.

  yaliyofuatia ya akina corpenicus, descartes ni matokeo tu.
   
 11. minda

  minda JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  usisumbuke. kuna sehemu katika biblia imeandikwa:

  mimi ndimi njia ukweli na uzima. mtu haji kwa baba (mbinguni) ila kwa njia ya mimi...(my words).
  mwenye hiyo nukuu atupatie manake naona huyu kiranga (sijui mjukuu wa mpagani kingunge?) ni too demanding
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Nimeuliza hapo juu, biblia hii hii imesema jua linazunguka dunia, je mnaamini na hilo pia?

  Mpaka sasa naona jiii. Biblia haina credibility kwenye haya, ni kitabu cha watu, kimetungwa na kuandikwa na watu. Kwa hiyo unless una empirical evidence za kuwepo kwa Jehanam, kama source yako ya info ni biblia, you might as well claim that there is a restaurant at the end of the universe based on a Douglas Adams Sci-Fi novel.

  It is all fiction, largely.
  [​IMG]
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jul 30, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Biblia ni fiction tu.....
   
 14. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Kaka usiumie kichwa sana kwani Dini ni sumu ya fikira zetu. Dini zote zililetwa kwa madhumuni ya hawa jamaa watutawale kwa urahisi zaidi

  Kama dini ni utaratibu wa maisha tunayoishi kila siku basi dini za mababu zetu zilikuwa nzuri kabla ya ukristo na uislam Kiranga utakuwa unanipata vizuri kwa kuwa unajua dini za mababu zetu zilivyokuwa zinasaidia ilikuwa ni mwiko wengine kufa njaa wakati wengine wanakula kama sasa jirani wako analala njaa wakati asubuhi unatupa chakula. Walileta dini zao ili kuweza kuua dini zetu na utamaduni wetu na dini zetu ili wapate kututawala kiurahisi

  uwepo au kutokuwepo kwa jehanamu hakutatusaidia kitu kwani matokeo yake watu tunapoteza muda mwingi kwa nchi zetu za kiafrikakuongelea dini badala ya kuwa na maendeleo. sehemu itatakiwa kupita barabara watu watakuambia kuna kanisa au msikiti usipitishe hapo au ukitaka kufanya hiki watakuambia dini haitaki. kwa mfano wenzetu wanatumia mpaka kinyesi cha binadamu kutengeneza biogesi lkn sisi tutasema hiyo dini haitaki ni najisi

  Matokeo yake sasa hakuna mafisadi kama viongozi wa dini walioanzisha makanisa na misikiti wakati yatima wanakufa na kuhangaika mitaani
   
 15. T

  Tiger JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  I love challenges.
   
 16. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  unafanya kazi gazeti gani? , hivi keyboard yako haina space bar ? (kwa wale walevi ,hii space bar hii haihusiani kabisa na bar ya kuuzia ulevi)
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Kwanza hii post haina paragraph wala nini hadi yatia uvivu kuisoma anyways nimejaribu, ni hivi katka kila kitu kuna opposide reaction yake, kama unakimbia elewa kuwa kuna hali ikusukumayo urudi utokako, ukisema ukweli kunauwezekano wa mwingine kijibu kwa kusema uongo. Kama una njaa basi elewa kuwa kuna uwezekano wa kushiba in short ni kuwa everything has its opposite side. Kama wamwamini Mungu basi elewa kuwa kuna mpinga Mungu na kama Mungu yuko Mbinguni basi kinyume chake wako Jehanam so IPO!
   
 18. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kiranga,
  pole sana kwanza elewa kuwa unapoishia wewe kuelewa ndipo mwingine huanzia
  na anapoishia mwingine ndipo unapoanzia wewe, sasa usipende kutaka kila
  mtu alazimike kuifanya akili yake ifanye kazi samba mba na akili yako,

  kwani wewe unaelewa nini kuhusu mbingu? unaelewa nini kuhusu nyota?
  si kila tunachoamini kuwepo ni lazima mwamini awahi kuenda wewe jamaa
  mwalimu wako nani hasa?
   
 19. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wewe ni atheist? Mbona haya maswali yamejaa jazba ya atheism?
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  I'm very tired my dears Jf friends, don't know where to start.
  Let me sleep by tomorrow, God willing we shall see each other.
  By the way if heven is there, why not hell. And if God is really why not devil?
   
Loading...