Nilishajitoa kujadili haya maswala lakini nimegundua halikuwa jambo la busara. Ni ushauri wangu kwa wanaJF tusipoteze muda na hawa watu...mi nawaona wote wahuni tu. Gembe hujatumia busara kuwataja watu fulani kuwa wako kwenye payroll wakati huna hata salary slip zao, suala la kutoa maoni limegawanyika katika makundi tofauti, kwa mfano:
1. Kuna watu wako tayari kutia pamba masikioni ili kumuunga mkono au kumtetea mtu yeyote hata kama hawamjui kiundani ili mradi wanatoka kumoja, kabila moja, dini moja au ni mapenzi binafsi tu na jina au wasifu.
2. Kuna watu hawako tayari yaani piga ua, kumsema mtu ambaye kwa namna moja au nyingine jina lake linatamkika vizuri masikioni pake, anamapenzi binafsi na rangi ya mtu huyo, au alishawahi kupokea fadhila muhimu hapo nyuma.
3. Wengine wanaweza kukuunga mkono mtu ni kwasababu hawezi kukaa kimya penye mjadala kama huu wetu, ni sawa na kuangalia mpira ukasema mi timu yangu fulani hata kama unayo timu yako ambayo kwa muda ule haichezi. Kwa mfano: ilipocheza Man na Arsenal kuna wapenzi wa Chelsea na Livepool waliamua kuishangilia Arsenal si kwa kuipenda timu hiyo ila kwa maslahi yao binafsi.
Sasa wandugu tukirejea kwenye jukwaa letu. Ishu ya Mengi na RA haina mwisho....wapo wanaomuunga mkono RA kwa rangi yake na sura yake ya kimanga pengine hata kwa kuwa amesemwa sana na wameanza kusympathisize nae au kama wanavyosema wadau...wamenufaika na uwepo wake. Pia kuna wanamuunga mkono Mengi kwa rangi yake nyeusi na pengine wamemsikia mara nyingi akichangia vijisenti kwa wanyonge japo hawajui kama moyo huo upo pia kwa wafanyakazi wake.
Mimi binafsi nilikuwa upande wa RA na kundi lake kwa kuwa naamini hawakutendewa haki katika MTAJO wa Mengi...interest yangu ilikuwa ni misingi ya sheria inapofikia kuwataja watuhumiwa. Baadae nilibadilika na kuwaona wote WAHUNI kwani nao wakatumia njia ile ile ya Mengi ambayo kwangu si njia sahihi katika kutatua matatizo makubwa kama haya. Hivyo nawahisi ndugu zangu tuweke kando ubinafsi, chuki, fitina na hata mapenzi binafsi na tusimame katika taratibu za sheria....tuwahamasishe watanzania wafuate misingi hii na ikiwezekana twende mtaani kuwaambia watu HAWA wakabidhi malalamiko yao mbele ya vyombo vya sheria na sisi tuhakikishe haki inatendeka. TUKIFANYE HAYO TUTATENDA JAMBO LA MAANA KWA NCHI BADALA YA KUONYESHANA UMWAMBA WA KUJENGA HOJA VICHAKANI.