Je, Zitto kumsifia Kikwete ni ....?

Kisoda2

JF-Expert Member
May 30, 2008
2,475
745
Magazeti mengi leo yameandika kuwa mbunge wa Kigoma kaskazini amusifu utendaji wa muungwana na hasa jinsi alivyo shughulikia miradi ya maendeleo huko Kigoma.
Wachambuzi wa siasa za nchi yetu naombeni kujuzwa hapa:-
1.Je huyu bwana mdogo ndo kaishiwa cha kuwaambia ndugu zake kwamba five yrs yeye amelifanyia nini jimbo lake?
2.Ama ndo mambo yale yale ya Tambwe Hiza?
 
acha uzushi ndo mana amekuwa specific, praised the achievement of JK in Kigoma and not the whole Tanzania! siasa si mchezi mchafu unavyojiaminisha wewe
 
Zitto hajafikia hatua ya kuwa Mnafiki kiasi hicho.......ameongelea baadhi ya maeneo machache kati ya lukuki ambayo Serikali imeyafanyia kazi Kigoma.Mleta mada usitupoteze
 
Sifa za Zitto kwa Kikwete na Serikali yake ni sawa na kumsikia Mbunge wa chama cha Conservative cha Uingereza anamsifia hadharani Waziri Mkuu kutoka chama cha Labour na serikali yake kwamba wamefanya mambo makubwa hapa na pale. Vile vile ni sawa na kusikia kiongozi kutoka chama cha Republican anasimama hadharani kusifia kazi nzuri ya kiongozi wa chama cha Democrat. Demokrasia hii ya Zitto nzuri sana!

CHADEMA wakitaka kuingia Ikulu watawezaje kupata kura za wananchi hususan wale wa Kigoma ambako tayari mbunge wao keshawadhihirishia na kuwahakikishia kwamba Kikwete na Serikali ya CCM imefanya makubwa mazuri jimboni humo? Wananchi wa Kigoma watakuwa na sababu gani za kuchagua mgombea kutoka CHADEMA wakati CCM inawatekelezea yale wanayotaka na mbunge wao kasifia juhudi hizo?
 
Zitto yuko right kabisa, kama kuna kisima kimejengwa lazima aseme kimejengwa na nani zaidi ya hapo ni unafiki, ulitegemea aseme barabara imejengwa na serikali ya Burundi, kuna mambo yaliyo wazi ambayo ni vigumu kuyapindisha au kusema uongo, vile vile asingeweza kusema miradi imetekelezwa na serikali ya Chadema.

Tofauti inakuja ni nani kasimamia utekelezaji wa hiyo miradi, maana si kwamba hilo jimbo lilikuwa halina mbunge lakini miradi mingi imetekelezwa wakati wa kipindi chake 2005-2010 hicho ndicho cha kujivunia na alikuwa na maana hiyo.
 
Ikiwa JK amefanya kazi kigoma specific mimi sina shida. Hata siku akiweza kuweka lami kuja kijijini huku niliko, japo mimi si m-ccm nitamsifu. sioni tatizo hapo.
 
Ni wakati wa kujua kusema ukweli hata kama ukweli huo utakugharimu. Zitto anayohaki ya kusema kweli anachoamini ni sawa na kweli.
 
Back
Top Bottom