Je, Zanzibar wamechangia pesa za maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya Muungano?

Tanganyika ichangie nini na tumeambiwa haipo.

Tanganyika ipo hata ile Hati kule UN imeandikwa jina la Tanganyika japo sasa inaitwa BARA lakini ndio Baba wa muungano Pesa yote inatoka Tanganyika a.k.a Bara , Zanzibar walikwisha kataa kitambo na sasa wamevunja katiba wao ni Nchi Hakuna wa kuwalazimisha Kutoa pesa.
 
Zanzibar si nchi? Au nimekosea?

Nani kakudanganya kwamba ZNZ ni nchi? Achana na maneno ya wanasiasa, watakupotosha. Kwa mujibu wa katiba yetu chombo chenye mamlaka ya KUTAFASIRI SHERIA ZETU NI MAHAKAMA period. Mahakama kuu ya rufani ya JMT walishasema (read rule out) kwamba Zanzibar sio NCHI, hivyo UHAINI hauwezi kufanywa Zanzibar. Ni sawa na Jamhuri imushitaki mtu kwa kosa la uhaini kwa kujaribu kuipindua serikali ya mkoa wa Tanga. Hiyo case it is null and void before the court of law.
 
Ni kama ndoa ambyo inayumba. Mmoja anayetaka kuachana htakubali kulipia matumizi ya pamoja, huyo mwingine anambembeleza abaki atalipia kila kitu hata kama mwenzake anastahili kulipia. Serikali 2 ni kupunguza gharama kwa zbar sio kwa bara ambayo iwe 2 au 3 italipia jmt.
Ni kweli Zanzibar hawaitaki ndoa na Tanganyika ,lakini Tanganyika a.k.a Bara ndiye anailazimisha ndoa ndio Maana analazimika kutumia Pesa nyingi kuilea Zanzibar na kutumia Mabilioni kuubembeleza muungano,Zanzibar wao wanakuja kusherekea na kula tu, mambo ya michango si kazi Yao ni kazi ya Tanganyika.
 
Hadhi gani apate Dr. Shein? Katiba ya JMT inasema kwamba rais wa Zanzibar ni WAZIRI ASIYE NA WIZARA MAALUMU. Dr. Shein ni sawa na Prof Mark Mwandosya akiwa Tanganyika. Halafu eti mnataka ZNZ wachangie sherehe za muungano, give me a break dude. Kama VIFARU tu vya kufanyia exhibition katika sherehe zao za MAPINDUZI "MATUKUFU" tunawaazimisha watapata wapi uwezo wa kuchangia sherehe za MUUNGANO?

Zanzibar wanayajua hayo yote ndio Maana hawajachangia chochote juu ya muungano kwa mda wa Miaka 47, wanajua Tanganyika anawahitaji Zanzibar kuliko Zanzibar anavyomhitaji Tanganyika, wao wanataka waje wale wanywe washerekee tu mambo ya michango hakuna kila kitu ni Tanganyika tu.
 
Zanzibar kuna watu wachache na tanganyika kuna watu wengi lakini cha ajabu wachache wanagawana nusu kwa nusu na wengi huku wachache wakati mwingine wakipata kingi .
 
Nani kakudanganya kwamba ZNZ ni nchi? Achana na maneno ya wanasiasa, watakupotosha. Kwa mujibu wa katiba yetu chombo chenye mamlaka ya KUTAFASIRI SHERIA ZETU NI MAHAKAMA period. Mahakama kuu ya rufani ya JMT walishasema (read rule out) kwamba Zanzibar sio NCHI, hivyo UHAINI hauwezi kufanywa Zanzibar. Ni sawa na Jamhuri imushitaki mtu kwa kosa la uhaini kwa kujaribu kuipindua serikali ya mkoa wa Tanga. Hiyo case it is null and void before the court of law.

Kama sio nchi, kwanini ina rais na wimbo wa taifa?
 
Znz hana sababu ya kuchangia muungano LUKUVI amesha sema bayana bila kutafuna maneno muungano sio wahiyari ni walazima kwa maslahi ya UKIRISTO sasa znz wachangie nini wakati wakijua ukiristo utafanya kila liwezekanalo ili dunia iyone muungano upo na wananchi wanaukubaki.
 
Tufunngueni account ya fedha ya pamoja kwanza...ikesha itakua rahisi kuandika cheki na kuwalipa suppliers wote!
 
Wana jamvi huko bungeni ili tajwa kuwa tangu mwaka 1968 zanzibar haijawahi kuchangia katika kapu la muungano,je katika gharama za maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya muungano zanzibar wamechangia?

Riziki Magembe;
Lukuvi sasa hivi atakuja hapa na kusema unauvunja Muungano huu mtukufu. Kwa nini uulizie gharama ilichangiwa na nani? Hapo hapo ulipo lazima uelewe kimoyomoyo kuwa, kachangia mwenye koti la kuungana. Kama hutaki Zenj (Mwali) anaweza amua kuishia zake.
Njemba lazima ibembeleze. Asikudanganye Lukuvi wala Sendeka. Tanganyika imetoa kiila senti.
 
Back
Top Bottom