Je, yawezekana kuanzisha polisi jamii isiyo na mahusiano na serikali?

akilimtindi

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
421
83
Nimetatizika sana kuhusu mamlaka ya polisi wetu n uwajibikaji wao, naomba wanasheria watushauri kidogo sehemu hii. Je, kuna uwezekano wowote wa kuanzisha kitengo cha polisi jamii kitachofanya kazi huenda kama ya kuwahoji watuhumiwa na kuleta habari zisizokinzana kwa umma kuhusu matukio?

Je, inawezekana kuanzisha NGO itayohusika kupitia labda kazi waliyofanya polisi na kuchambua ukweli na pumba ili kuwafunulia wananchi kile ambacho hawakijui?

Je, inawezekana kuanzisha kampuni ya ku-audit kazi za polisi kama vile Sirkali inavyoita kampuni kama Ernest & Young kukagua mahesabu ya BOT? naombeni msaada hapo
 
Nimetatizika sana kuhusu mamlaka ya polisi wetu n uwajibikaji wao, naomba wanasheria watushauri kidogo sehemu hii. Je, kuna uwezekano wowote wa kuanzisha kitengo cha polisi jamii kitachofanya kazi huenda kama ya kuwahoji watuhumiwa na kuleta habari zisizokinzana kwa umma kuhusu matukio?

Je, inawezekana kuanzisha NGO itayohusika kupitia labda kazi waliyofanya polisi na kuchambua ukweli na pumba ili kuwafunulia wananchi kile ambacho hawakijui?

Je, inawezekana kuanzisha kampuni ya ku-audit kazi za polisi kama vile Sirkali inavyoita kampuni kama Ernest & Young kukagua mahesabu ya BOT? naombeni msaada hapo
Inawezekana kabisa. Wales- Katika Uingereza wanalo hiuo jambo na linafanmkiwa sana tu. Jamii inafurahi na Serikali inafurahi. It is possible.
 
Inawezekana kabisa. Wales- Katika Uingereza wanalo hiuo jambo na linafanmkiwa sana tu. Jamii inafurahi na Serikali inafurahi. It is possible.
Nakushukuru sana mkuu maana swali lingine nililotaka kuuliza ni kama kuna nchi iliyowahi kujaribu hili na mambo yalikuwaje, umenipatia mfano mzuri mkuu. Je, kwa hapa Tanzania inawezekana hii kweli...???

Polisi wetu hawafanyi lolote kuhusu chochote cha maana...!
 
kichwa cha swali lako hakihusiani na swali lako la ndani; so ni nini hasa unataka kujua?
Tumia tu kichwa cha habari kama swali lenyewe mkuu, hizo zilizomo ndani ni alternative nilizofikiria labda zaweza kusaidia kama ya kwanza haitofaa. Hata hivyo nimeambiwa kuwa inawezekana, kwahiyo fuata kichwa cha habari mkuu.
 
Basi kama swali ni kuanzisha Polisi Jamii isiyohusiana na serikali, jibu ni hapana. As a matter of fact nimekuwa na feelings kuwa his security firms tulizonazo haziruhusiwi kisheria na Kikatiba.
 
Mrema alianzisha sungusungu, Hili lilikuwa ni jeshi ambalo halikuwa la kisheria, hawa wameanzisha polisi jamii sasa kila mmoja kili kukicha anakuja na jambo lake hata kama wamelijadili bar ama pengine, kifupi hatufuati sheria ila tunafuata matakwa ya anayeongoza ama mwenye dhamana na mamlaka.
 
Mimi naungana na Mwanakijiji kwamba haiwezekani kuanzisha jeshi la polisi lisilo na mahusiano na serikali.

Hii maana yake ni private police na itakuwa ni kichekesho.

Kama nimeelewa swali lako ni kwamba umekerwa na mwenendo wa sasa ambapo jeshi la polisi limeshindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusiana na ajali ya gari ilomhusu marahemu Chacha Wangwe.

Pia ukichambuachambua humu JF kuna thread ambayo nime-suggest kuundwa upya kwa jeshi la polisi ili liendane na wakati.

Unajua mimi nimeona mambo mengi ya maana ambayo majeshi ya polisi katika nchi za wenzetu pamoja na wananchi wanafanya tena kwa ufanisi.

Katika nchi zilizoendelea nao wana vituo vya polisi hata vile vya mobile au katika kila wilaya. Pia wameongeza polisi wa jamii au police community support officers ambao wamewekwa kutokana na marekebisho (reforms) ambayo yanapitishwa na bunge.

Kwa hio ni suala la ku-lobby na wabunge ili wamshauri raisi ili nae amteue mtu mwenye ujuzi na mambo ya polisi ili atengeneze reform proposal ambayo baada ya kuonwa na waziri Masha ataipeleka bungeni kwa kujadiliwa kabla ya kupitishwa na kuwa sheria.

Unajua wenzetu wapo mbali mno. Inapotokea ajali yoyote ile ndogo kama hio ya marehemu Wangwe, wananchi wananchi wa eneo hilo kitu cha kwanza kinakuwa ni kuwatafuta polisi ambao nao watawajulisha watu wa "ambulance".

Katika eneo la ajali wananchi wakajaribu kutoa msaada unaohitajika na kama kuna first aider yoyote atamshughulikia majeruhi huku akiwasiliana na watu wa ambulance ambao nao wakiwa njiani wanakuwa wanaandaa kila kitu kwa ajili ya kushughulikia majeruhi na wakifika eneo hilo ambalo linakuwa tayari "cordoned" na polisi ambao walifika muda si zaidi ya dakika 20.

Umuhimu wa polisi kuzuia kwa utepe au "cordon" eneo la tukio lolote lile ni kuzuia watu wasiingie au wasivuruge uchunguzi ambao unakuwa unaanza mara polisi wanapofika eneo hilo.

Sasa kama hayo bado hayawezi kufanyika kwa sasa mpaka mtu pengine anafariki kwa kukosa msaada, ni hali ambayo inasikitisha sana.

Ninaloliona hapo ni kwamba Tanzania bado tuna safari ndefu kiasi cha kufikia kutoona watu wa kawaida wanaingia eneo la ajali na kuiba mali au hata kummmalizia au kuwamalizia majeruhi.
 
Nathani Hiyo Itakuwa Jeshi La Kimfya Ambapo Si Siku Nyingi Tutayaona Hapo Kwetu, Nigeria Au Niseme West Africa Jamaa Wana Vijeshi Vyao,huko Colombia Kila Family Yenye Visent Haa Ianayo Jeshi,sasa Kwa Nini Usiwe Na Jeshi Lako Pale Tulionao Ni Staily Ya Zombe, I Can Not Trust Dem
 
mawazo mazuri kabisa ,ni kweli jeshi la polisi linahitaji oversight ya wananchi,it just make sense,lakini mafisadi wetu ambao bado wanasisitiza serikali isaini contracts kwa siri ukiwambia hilo jambo wataona unataka Tanzania tupeleke mtu Mars
 
shida ya jeshi letu la police linataka ku divert shughuli zao kwa wananchi.
Sawa ni kweli wananchi ndiyo walio na clue za baadhi ya wakola na watenda uovu. Lakini tangu zamani jeshi la police kupitia makachero wao walikuwa na ushirika na wananchi katika kupata datas za wanaovunja sheria.
Hata hivyo ni hawa hawa police wanaotoa siri kwa waharifu kwa kuwataja wanaotoa taarifa za uharifu. Kwani ni ukweli usio na shaka kwamba police wetu wengi sana kama 70% wako kwenye payroll ya waharifu. Got me?
 
Hatuwezi kuanzisha "polisi jamii" let alone "polisi jamii isiyo na mahusiano ya serikali"

Ni kama kulitaka sanamu la Michelini lifanye some high wire acrobats!
 
Inawezekana sana!... Ikiwa kwanza wabunge wetu wasipokuwa viongozi wa serikali (Mawaziri).
Pili ni lazima wakuu wa vyombo vya Usalama wawe na mamlaka kamili ya kuendesha shughuli zao bila kuwepo kamati za wanasiasa zinazopitia tuhuma ili kutoa uamuzi wa uchunguzi.
Jeshi la Usalama wakitaka kuchunguza kifo, Ufisadi ama kashfa fulani sio lazima wapewe kibali na mkuu fulani mfano wa swala la EPA ambalo kwanza limeenda bungeni kisha likamfikia rais na kurudi ktk vyombo vya usalama kufanya yalitoamriwa na wanasiasa...
Kilichotakiwa ni vyombo vyetu kufanya uchunguzi wao wenyewe na kama watahitaji ushirika wa nje mfano wa EPA wale Ernst & Young kisha baada ya kukusanya ushahidi ndipo chombo hicho kinaweza kuepelka mashtaka mahakamani, au kuwakilisha bungeni kwa kamati teule, ama kwa kuiwakilisha kwa rais kulingana na uzito wa swala lenyewe.
Tatizo la Tanzania kila swala huanzia kwa wanasiasa ambao kwa kura za maoni hupitisha ama kutopitisha uchunguzi hali wao hawana ushahidi mkononi wala mamlaka ya kuamua kuendesha mashtaka. Sidhani kaa katiba yetu inasema lazima madai yoyote ya Ufisadi yapitie bungeni kwanza ama kwa wanasiasa kuchambua ukweli wa madia hayo kabla vyombo vya usalama havijahusishwa.
Ni jambo la kushangaza sana Bunge letu leo hii linasikiliza kesi mbalimbali kama vile wao ndio mahakama...hukumu zote tunaziona bungeni siku hizi hata zile za hujuma ya uchumi wetu.

Kifupi Wanasiasa ni - Above the Law, bado tunaendelea na mfumo wa Kijamaa (communist) ambao Wanasiasa viongozi are Untouchables na wanamwogopa Mwenyekiti wao (rais) tu sio jeshi wala mahakama.
 
Nimetatizika sana kuhusu mamlaka ya polisi wetu n uwajibikaji wao, naomba wanasheria watushauri kidogo sehemu hii. Je, kuna uwezekano wowote wa kuanzisha kitengo cha polisi jamii kitachofanya kazi huenda kama ya kuwahoji watuhumiwa na kuleta habari zisizokinzana kwa umma kuhusu matukio?

Je, inawezekana kuanzisha NGO itayohusika kupitia labda kazi waliyofanya polisi na kuchambua ukweli na pumba ili kuwafunulia wananchi kile ambacho hawakijui?

Je, inawezekana kuanzisha kampuni ya ku-audit kazi za polisi kama vile Sirkali inavyoita kampuni kama Ernest & Young kukagua mahesabu ya BOT? naombeni msaada hapo



Basi kama swali ni kuanzisha Polisi Jamii isiyohusiana na serikali, jibu ni hapana. As a matter of fact nimekuwa na feelings kuwa his security firms tulizonazo haziruhusiwi kisheria na Kikatiba.


I would like to rephrase that to read "XYZ Jamii isiyohusiana na serikali"

Tumeshuhudia chombo vya habari hasa television vikiiwajibisha na kuipeleka Serikali mchaka mchaka, hata kupelekea tuanze kuamini nchi inaongozwa na TV. Ukiangalia kwa upande mwingine utaona si TV bali wananchi wanaiwajibisha Serikali indirectly.

Internet ni nyenzo muhimu sana, we just need to exploit it.

Akilimtindi idea yako safi sana, inahitaji kufanyiwa kazi. Ila kwanini utumie jina akili-mtindi?




.
 
Nimesoma post kadhaa kwa swali langu naona kuna wanaoniunga mkono na mmoja ametoa mfano wa Wales, Uingereza kuwa kuna jambo kama hilo.

Pia kuna wazo kuwa bunge letu lisiwe na mawaziri, bunge lenyewe na mawaziri pengine kwa maana ya kwamba bunge litakuwa likifanya kuikagua serikali tofauti na sasa ambapo serikali inajikagua yenyewe (ndoto za mchana).

Nadhani yote ni sawa na yote yanatakiwa tukianzia na hili la bunge kuwa peke yake, yaani mawaziri watoke kwingine. Tena jambo zuri sana ni kwamba Waziri akipoteza kiti chake ndio imetoka, sio anakuja kuegesha masikio tena bungeni, NO...! Nadhani pia itaondoa dhana ya majibwa kung'ang'ana kupata ubunge kwa style zote maana inatumika kama ngazi ya kuingia serikalini. "Wewe fanya bidii ukipata ubunge nakuingiza kwenye supu moja kwa moja, nakupa Uwaziri" Mbunge aking'ang'ana basi iwe amekomaa kuwakilisha wananchi na sio vinginevyo. Waziri akiteuliwa ama akichaguliwa basi ni kama ajira na bunge limwangalie vyema, akichemsha anang'olewa on the sport. Kwanza wabunge watakuwa wakali maana hawapo serikalini na mawaziri watakuwa makini maana watawajibishwa kirahisi kwasababu huo mchanganyiko uliopo sasa utakuwa umepotea, Waziri akienda Dodoma ni kuwakilisha ama kuulizwa juu ya uzembe fulani, sio kwenda kukaa tu kusikiliza wabunge wanaongea nini...

Nadhani hapo ni pazuri pa kuanzia tukifikiria jinsi ya kuwaweka polisi sawa ama kuwa na kitengo kingine ambacho kinaweza kumulika ndani ya polisi maana akina manumba na wenzake wanacheza tu sindimba hakuna lolote.

Nimeshangazwa sana na Polisi unafiki wa polisi kumpeleka Deus Mallya mahakamani siku ya kumzika Wangwe, ni wapumbavu wakubwa wanaotaka sisi tuamini wanafanya kazi. Nasema ni wapumbavu kwasababu hawajui walifanyalo na hawajui kwamba hawajui maana wangeshabadilika muda uendavyo ukibadilisha mambo.
 
Back
Top Bottom