Je, wewe ungekuwa yule kijana,ungefanyaje?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,406
40,358
Kutokana na kuimarika kwa teknolojia na ubora wa elimu duniani,vijana wengi wadogo au wenye umri wa kati wamekuwa wabobezi au mabingwa katika fani walizosomea, mfano udaktari wa kutibu binadamu.

Sasa ilitokea mji mmoja mmama mtu mzima alikuwa na tatizo la uzazi, baada ya kwenda hospitali husika.

Wakamfanyia vipimo na ikaonekana anatakiwa aje afanyiwe upasuaji siku fulani ambapo daktari bingwa atakuwepo. Ile siku ilipofika, yule mmama akaenda hospitali na kupelekwa kwenye chumba cha upasuaji.

Baada ya dakika chache daktari bingwa akawa amefika chumba cha upasuaji; yule mmama alishtuka kwa kumuona ni kijana mdogo na kuanza kuropoka huyu kijana ni mdogo sana hatakiwi kuuona utupu wangu.

Yule kijana akawa anacheka tu; baada ya kufanyiwa counselling ilibidi akubali kwa shingo upande. Je wewe ungekuwa yule kijana,ungefanyaje?
 
Kazi ya daktari bingwa sio kuhangaika na ridhaa ya mgonjwa (mteja) juu ya nani auone utupu wake na nani asiuone.
Ningekua 'yule kijana' ningetekeleza wajibu wa daktari bingwa.
 
Back
Top Bottom