Je, wewe ni Mzaliwa wa Kigoma? Fanya haya ili uraia wako usitiliwe shaka yoyote na wabaya wako

Nchi jirani na maeneo hayo zipo stable na raia wake hata kama ataingia wengi wao wanarudi walipotoka na wana mahusiano ya kindugu mfano Wakurya wa Tz/Wakurya wa Kenya, Wajaluo wa Tz/Wajaluo wa Kenya, Wamasai wa Tz/Wamasai, Wanyambo wa Karagwe / Wanyankore wa Uganda huwa Kuna vi-favor visivyo rasmi kutokana na mahusiano ya moja Kwa moja ya kiutamaduni kabla na baada ya Uhuru hasa ukizingatia tulikuwa chini ya koloni la Uingereza lakini Kuna watu wanakuwa Wana vinasaba vya karibu tangu enzi na enzi
Ok
 
Wamejazana Mno Mishamo Huko, Nambuka Jiwe Aliwakataa Kuwapa Uraia Akawaambia Wazi Mnamiliki Mpaka Silaha Tutawanyoosha Hakuna Uraia View attachment 2881102View attachment 2881104
Mbona wale wa Katumba Katavi wamepewa Uraia wakati hawana tofauti na wa Mishamo,tena hawa wa Katumba ni Magufuli mwenyewe ndio aliwapa uraia. Mwaka jana Uhamiaji ilipitisha fagio kwa wale Waha wauza maziwa na wakopesha bidhaa mitaani kuanzia Tegeta mpaka Temeke wengi walitokea Mishamo katavi ambapo kiukweli si RAIA wa Tanzania.
 
Baba yangu ni mtusi walihamia Kagera miaka kenda. Akaoa mama yangu muikizu (kabila kutoka Mara).
Sina hisia ya unyarwanda najiona ni mhaya. Najiona mtanzania japo kuna nyakati nakerwa na yanayoendelea nchini, lakini nikiwaza mkono wa chuma wa Kagame sitamani kuishi huko.
Rudi kwenu mkapambane nae,haiwezekani mtu mmoja awasumbue maelfu tena wasomi.
 
Cha kushangaza katika kasumba hii ya uraia huwakuti Wajaluo, Wamasai, na watu wa Kusini. Kwanini muda wote Kigoma na marachache Kagera. Kwanini wahamiaji haramu wa mkoa wa Kigoma na Kagera wanaogopwa sana, tofauti na Mara, Arusha, Ruvuma na Mtwara?.
Sababu iko wazi: wahaamiaji kutoka Burundi na Rwanda walioko katika mikoa ya jirani na nchi zao waliacha maadui kule walikotoka. Uadui wao unaendelea kwa kufanyiana kampeni chafu duniani kote. Baadhi ya kamepeni chafu dhidi yao hufanywa na viongozi wa nchi walikotoka na matajiri wakubwa. Mmasai wa Tz na Kny ni ndugu, mkulya wa Tz na Kny ni ndugu vile vile wajaruo
 
Ati wamepewa uraia watu zaidi ya 200,000? Huo ni uraia hewa ndugu yangu kutengwa kupo pale pale miaka ya 70's watusi waliokuwepo kagera hasa kambi ya kimuli walipewa uraia na nyerere basi wakaishi mpaka wakazeeka na kufia hapo kagera sasa mwaka 2006 vizazi vyao vilivyobaki vikasombwa na kupelekwa Rwanda kwamba ni wahamiaji haramu wanarudishwa kwao, wengi wao hajui hata lugha ya kinyarwanda hawana ndugu huko ila ikabidi wapekwe tu bila kujali lolote.

Utajiri wa kwanza ni watu sasa inakuwaje nchi inakataa watu? Tutapataje maendeleo bila watu? Na hii kasumba ya ukitaka kumdhoofisha mtu unamuita mkimbizi itaisha lini? Hayo tumeyaona na yanazidi kuongezeka ilikuwaga kigoma na kagera sasa hata geita na shinyanga ukizaliwa huko unaonekana ni raia wa mashaka, mwisho wa haya mambo lini? Yanafaida kwa nani?

Ni kutokana na watanzania walichokishuhudia kipindi cha uhai wao!

Kama hujui ubaguzi huunganishwa na matukio fulani hauji tu kama kwamba wanabaguliwa no!

Watusi/wahutu ——mauji ya kimbari/M23/Machafuko
Wasomali—-ugaidi
waarabu——ubaguzi/ugaidi

Usihangaike kulalamika jua kila kitu kinachanzo!! Ubaya unaishi
 
Mbeya, Songwe, Mara na Kilimanjaro nazo zimepakana na nchi jirani na kuoa na kuolewa ni jambo la kawaida sn, mbona hakuna usumbufu wowote?

we netanyahu jina au kiazi??

Uwe unasoma comment zangu utoe uvundo kichwani.

Ubaya unaishi!! Yaliyotokea kwene hizo nchi ndio yanayosababishwa watu wawe na hofu au kinachoendelea Kongo!! Ni hilo lililoganda kichwan mwa watanzania si kua wanahangaika na mipaka yote ushaona wanasumbua mipaka ya kenya ,zambia au malawi??
 
Unasahau Rwanda Burundi na Tanganyika zilikuwa nchi moja koloni la mjerumani?

[mention]jay-millions [/mention] wewe n mrundi au mtusi??
Huwezi ng’ang’ania hawa watu wakat intelligencia ya nchi imeona kuna shida ya usalama!!

Kama wana kwao warudi
mbona sisi tulipokea wasomali wabantu walioishi miaka zaidi ya 200 somalia??
 
Ndugu watu wameishi vizazi na vizazi hawajafanya baya lolote leo unawafananisha na hamasi? Hii chuki imepitiliza sasa
Nimeona comments za mtu somewhere nikafumbuka macho: anasema kuwa huenda kuna agenda ambayo serikali inataka kutusahaulisha, anasema kuwa haoni sababu kwanini hili lisemwe sasa na lisemwe na mamlaka makubwa kwenye forum kubwa kama ile. Nimeona pia mtu akitoa orodha ndefu ya watu waliotajwa kuwa wanaasili ya nchi jirani. mtoa maoni kataja Julius Nyerere, KInana, Moses Mnauye, Iddi Simba , apson Mwangonda etc
 
Baba yangu ni mtusi walihamia Kagera miaka kenda. Akaoa mama yangu muikizu (kabila kutoka Mara).
Sina hisia ya unyarwanda najiona ni mhaya. Najiona mtanzania japo kuna nyakati nakerwa na yanayoendelea nchini, lakini nikiwaza mkono wa chuma wa Kagame sitamani kuishi huko.

kwaiyo we ni chotara??
 
Unafikiri kujaza nchi ubaguzi na chuki ndo kutaleta nafuu ya maisha? Tukimaliza kubagua hao who next? Waarabu, wahindi, wasomali au wazenji? Ubaguzi ukiulea hautaishia hapo bali mwishowe utabagua hata watoto wako mwenyewe wa kuwazaa

we bana rudi kwenu!!

Kongo had sasa watu milion 12 wamekufa!!

Kosa ni kupokea wageni?? bora kufa kwa ubaguzi kuliko siku mgeni akuue
 
Mm ni mtanzania.Lakin pale Uganda kuna, kabira yetu wengi sana. Haya Mambo Nyerere, aliyakataa. Nyerere mwenyewe alitokea Rwanda na kuja Musoma. Wajita wakawaita vijanaki. Yaan waliokuja na nn. Leo tunaanzisha debate za Kipumbavu.

we nchi yako yenyewe inatwaliwa na nyankole watusi wa uganda.

Tangu waingie madarakani hawajatoka hadi leo
 
we netanyahu jina au kiazi??

Uwe unasoma comment zangu utoe uvundo kichwani.

Ubaya unaishi!! Yaliyotokea kwene hizo nchi ndio yanayosababishwa watu wawe na hofu au kinachoendelea Kongo!! Ni hilo lililoganda kichwan mwa watanzania si kua wanahangaika na mipaka yote ushaona wanasumbua mipaka ya kenya ,zambia au malawi??
Sikiliza dada angu unatakiwa usome historia, hawajaanza kusumbuliwa leo ni muda mrefu tangu enzi ya Mwl, nadhani kuna shida zaidi tunatakiwa kufanya utafiti mkuu.
 
View attachment 2881093

Ukishazaliwa Kigoma au ukiwa na asili ya Kigoma jambo la kwanza unalotakiwa kuwa nalo (kichwani) kabla ya yote unatakiwa kuwa na uelewa mzuri wa maswala ya elimu ya uraia na utaifa. Kwasababu hiyo ndio fitina ya kwanza utakutana nayo pindi tu ukihitaji kujitanua kihimaya. Uraia ndio fimbo ya kwanza utayocharazwa nayo.

Mambo muhimu ni kuhakikisha kwamba makaburi ya wazee wako yanahifadhika kwa pande zote (ubabani na umamani). Hakikisha kwamba nyumba za wazee wako zinahifadhika haziuzwi wala kuvunjwa. Hakikisha kwamba ardhi yenu mnaitunza vyema, kumbukumbu za picha na mabaki ya historia muyahifadhi ipasavyo.

Watoto zenu anzeni kuwafundisha mapema namna ya kukabiliana na kasumba hii ya uraia inayotumiwa kama silaha kuwadhoofisha watu wa Kigoma.

Kwanini tunashauri mambo haya? Ni kwasababu nchi yetu pendwa bado haina njia sahihi ya kufanya verification ya uraia hususan kwa watu walio mipakani. Usumbufu umekithiri mno, na sasa imekua kasumba endelevu.

Sio ajabu tena muhamiaji haramu kuingia nchini, kupata haki zote kinyemela ikiwemo kuajiriwa na kuteuliwa katika nafasi za maamuzi.

Hawa watu wanapataje nguvu hiyo?
...........
Hivyo ni muhimu kwa Serikali kuweka mifumo mizuri kwa watu wa mipakani, hususan huku kwetu Kigoma na watu wenye asili ya Kigoma.

Cha kushangaza katika kasumba hii ya uraia huwakuti Wajaluo, Wamasai, na watu wa Kusini. Kwanini muda wote Kigoma na marachache Kagera. Kwanini wahamiaji haramu wa mkoa wa Kigoma na Kagera wanaogopwa sana, tofauti na Mara, Arusha, Ruvuma na Mtwara?.

Mwaka 2014 Tanzania ilitangazwa kuwapa uraia wakimbizi 162,000 wa Burundi kwa mkupuo.

Idadi ya watu waliopewa uraia ilifikia 200,000, rekodi ambayo haijawahi kutokea mpaka muda huu kwa mujibu wa shirika la wakimbizi wa Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kama tunawapa watu uraia kwanini hakuna mifumo mizuri ya utambuzi kwa watu hawa? Kwanini bado wenyeji wenye asili ya Kigoma wanapitia madhila na kasumba ya uraia hadi sasa?

Kasumba hii imepelekea hofu kwa watu wa Kigoma, leo mtu wa Kigoma hawezi kuthubutu kusema kwamba ana ndugu Congo au Burundi.

Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi wamesoma hadi shule za Kenya, wana ndugu zao Kenya na Tanzania na wala hawapati usumbufu au ukakasi wowote.

Ukienda Mtwara, Wamakonde na Wayao wapo pande zote mbili za Msumbiji na Tanzania, wala hakuna shida.

Ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na Wazambia na Wamalawi, wameoleana mno, wafanyabiashara wengi wa Lusaka ni Wakinga na Wanyakyusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule Zambia.

Leo hapa mwanakigoma apite mpakani aseme naenda kusalimu ndugu zangu Burundi au naenda kwa ndugu zangu Congo. Basi na yeye atajumuishwa kuwa ni Mrundi au Mkongo.

Ukienda Moshi kwa Wachagga, na Wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili Tanzania na Kenya, nchi ya Kenya kuna eneo na kabila la Wameru.

Ni kawaida sana kumkuta mtu wa Tanga au Zanzibar ana ukoo wa mashangazi na wajomba huko Mombasa Kenya.

Mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote kwasababu watu wanaoleana, wanafanya biashara pamoja, wanazaliana na wengine wanahamia kabisa. Lakini huku kwetu Kigoma mambo yanakua ni tofauti. Dhiki na manyanyaso ya uraia yanazidi.

Je! serikali inasubiri nini kutatua fumbo hili la muda mrefu kwa wakazi wa asili ya Kigoma?

Ukijitambulisha wewe ni mtu wa Kigoma chakwanza kabisa mtu anakufikiria kunako uraia. Kanakwamba watu wa Kigoma ni raia daraja la pili. (Inaumiza sana kihisia na kiakili pindi unapowekewa mashaka).

Kigoma Region Tanzania
Kagera wanachukiwa kwa sababu ya nguvu zao kiuchumi, elimu, nk, pia kwa vile kuna propaganda kuwa Rwanda(ya, Kagame) ni adui yetu, na wana kagera/karagwe/ngara, wana fanana Sana na watu wa huko Rwanda, Burundi, Uganda,
Ukiwa jamii ya mpkani, huwezi kuzuia kuwa na ndugu upande wa pili, hii mipaka aliyeiweka, hakuangslia jamii, akatenga jamii moja pande mbili,
Nina binamu zangu tumesoma shule za msingi Zambia, tunaongea kiwemba, chuo mi nikarudi bongo, wenzangu, wakazamia Zambia, wameoa huko, wanamiriki ma kampuni huko, wanapiga mpaka kura huko, harafu wakija bongo, kuna kenge uhamiaji, aliyepata ajira kwa kubebwa na D zake,anasema sio raia.
 
Rudini makwenu tu Nchi za Watu ni Za watu Na kwanin mlazimishe Urai kwenye Nchi za Watu apo mlipo utakuta Mnalima kwenye Ardhi yetu bure kabisa kana kwamba iyo Ardhi ni ya Mababu zenu Wakati Ardhi Yenu ipo ila Mnaogopa Kurudi
 
View attachment 2881093

Ukishazaliwa Kigoma au ukiwa na asili ya Kigoma jambo la kwanza unalotakiwa kuwa nalo (kichwani) kabla ya yote unatakiwa kuwa na uelewa mzuri wa maswala ya elimu ya uraia na utaifa. Kwasababu hiyo ndio fitina ya kwanza utakutana nayo pindi tu ukihitaji kujitanua kihimaya. Uraia ndio fimbo ya kwanza utayocharazwa nayo.

Mambo muhimu ni kuhakikisha kwamba makaburi ya wazee wako yanahifadhika kwa pande zote (ubabani na umamani). Hakikisha kwamba nyumba za wazee wako zinahifadhika haziuzwi wala kuvunjwa. Hakikisha kwamba ardhi yenu mnaitunza vyema, kumbukumbu za picha na mabaki ya historia muyahifadhi ipasavyo.

Watoto zenu anzeni kuwafundisha mapema namna ya kukabiliana na kasumba hii ya uraia inayotumiwa kama silaha kuwadhoofisha watu wa Kigoma.

Kwanini tunashauri mambo haya? Ni kwasababu nchi yetu pendwa bado haina njia sahihi ya kufanya verification ya uraia hususan kwa watu walio mipakani. Usumbufu umekithiri mno, na sasa imekua kasumba endelevu.

Sio ajabu tena muhamiaji haramu kuingia nchini, kupata haki zote kinyemela ikiwemo kuajiriwa na kuteuliwa katika nafasi za maamuzi.

Hawa watu wanapataje nguvu hiyo?
...........
Hivyo ni muhimu kwa Serikali kuweka mifumo mizuri kwa watu wa mipakani, hususan huku kwetu Kigoma na watu wenye asili ya Kigoma.

Cha kushangaza katika kasumba hii ya uraia huwakuti Wajaluo, Wamasai, na watu wa Kusini. Kwanini muda wote Kigoma na marachache Kagera. Kwanini wahamiaji haramu wa mkoa wa Kigoma na Kagera wanaogopwa sana, tofauti na Mara, Arusha, Ruvuma na Mtwara?.

Mwaka 2014 Tanzania ilitangazwa kuwapa uraia wakimbizi 162,000 wa Burundi kwa mkupuo.

Idadi ya watu waliopewa uraia ilifikia 200,000, rekodi ambayo haijawahi kutokea mpaka muda huu kwa mujibu wa shirika la wakimbizi wa Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kama tunawapa watu uraia kwanini hakuna mifumo mizuri ya utambuzi kwa watu hawa? Kwanini bado wenyeji wenye asili ya Kigoma wanapitia madhila na kasumba ya uraia hadi sasa?

Kasumba hii imepelekea hofu kwa watu wa Kigoma, leo mtu wa Kigoma hawezi kuthubutu kusema kwamba ana ndugu Congo au Burundi.

Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi wamesoma hadi shule za Kenya, wana ndugu zao Kenya na Tanzania na wala hawapati usumbufu au ukakasi wowote.

Ukienda Mtwara, Wamakonde na Wayao wapo pande zote mbili za Msumbiji na Tanzania, wala hakuna shida.

Ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na Wazambia na Wamalawi, wameoleana mno, wafanyabiashara wengi wa Lusaka ni Wakinga na Wanyakyusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule Zambia.

Leo hapa mwanakigoma apite mpakani aseme naenda kusalimu ndugu zangu Burundi au naenda kwa ndugu zangu Congo. Basi na yeye atajumuishwa kuwa ni Mrundi au Mkongo.

Ukienda Moshi kwa Wachagga, na Wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili Tanzania na Kenya, nchi ya Kenya kuna eneo na kabila la Wameru.

Ni kawaida sana kumkuta mtu wa Tanga au Zanzibar ana ukoo wa mashangazi na wajomba huko Mombasa Kenya.

Mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote kwasababu watu wanaoleana, wanafanya biashara pamoja, wanazaliana na wengine wanahamia kabisa. Lakini huku kwetu Kigoma mambo yanakua ni tofauti. Dhiki na manyanyaso ya uraia yanazidi.

Je! serikali inasubiri nini kutatua fumbo hili la muda mrefu kwa wakazi wa asili ya Kigoma?

Ukijitambulisha wewe ni mtu wa Kigoma chakwanza kabisa mtu anakufikiria kunako uraia. Kanakwamba watu wa Kigoma ni raia daraja la pili. (Inaumiza sana kihisia na kiakili pindi unapowekewa mashaka).

Kigoma Region Tanzania
Me mw hata sikuwazaga ilo sana mpk rafiki yangu aliyezaliwa Kagera akasumbuliwa kupata passport ndo akaniambia watu wa ukanda la ziwa wanafanyiwaga ivi coz wapo kw boda nkaona ajabu coz mw nimezaliwa Mbeya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom