Je, Wema Sepetu atakubali kuwa mke wa Nabii Tito?

Huyo wala si Nabii fake tu, bali ni mwehu . Amri ya saba inasema Usizini yeye anahimiza watu wazini na wasichana wa kazi huku wakiwa na rundo wake. Mchawi huyu.
Anatumia kitabu hicho hicho. Jambo la msingi ni kuwaelimisha waumini juu ya ukweli wa ndani ya Injili.

Anaweza kula huyo binti kama pochi lake litakuwa fresh.
 
Mi namshauri afungue branch na huku kwetu bukoba, wafuasi wake tuko wengi
 
Makanisa yana kibali kufanya ibada asubuhi na kama huo mvinyo wanaunywa kama eako bar ni kosa kisheria
Na yeye anafanya hivyo wanakunywa siku za ibada ambapo ibada hazijatajwa zinatakiwa ziwe asbh tu bali ni siku nzima,siku za kazi anafanya maombi yake jioni na wanakula vyombo,sasa baa gani inafunguliwa kabla ya saa za kazi ambapo atatakiwa kufanya ibada?
 
Kimusingi hapa duniani kuna dini za aina mbili tu dini zilizoletwa na wageni na dini za wenyeji dini zilizoletwa na wageni ni Islamic na Christianity hizi dini tofauti zake ni tatu tu lakini pia zinavitu vikubwa viwili vinafanana kwa hiyo hoja hapa huyo nabii ni wa dini gani ili mutafakari je dini zilizoletwa na wageni na zile za wanyeji zipi sahihi
Duniani kuna dini zaidi ya hizo mbili mkuu
 
Umeoa, una michepuko, unakunywa pombe baa tena mpka unakesha, kanisani au msikitini huendi alafu upo kwenye uzi huu unamponda Nabii Tito wakati yeye ķakurahisishia kwa kukuongezea neno wakati uñikata maji
Mbona mfalme Solomon alikuwa na mahawara si alizini na bible imemtaja je wewe nani mpaka ubishe.
 
Huyu niborasana kwanza nimkweli na nisahihi anao wafuasi wengi tu ,wanaume wangapi niwalevi na wazinifu?? Huonikuwa niwafuasiwake hao??wapo mashehe na mapadri weengi wazinzi na walezi ila huyu sio mnafiki kabisa.pia niuhuru wakuabudu huo muacheni jamani maadam havunji sheria.
 
Sipati picha nyimbo za walevi wanazoimba ahaaa pambio, ninachojua walevi wana sauti mzuri wanaimba bila stress
 
Kimusingi hapa duniani kuna dini za aina mbili tu dini zilizoletwa na wageni na dini za wenyeji dini zilizoletwa na wageni ni Islamic na Christianity hizi dini tofauti zake ni tatu tu lakini pia zinavitu vikubwa viwili vinafanana kwa hiyo hoja hapa huyo nabii ni wa dini gani ili mutafakari je dini zilizoletwa na wageni na zile za wanyeji zipi sahihi
yamewakuta pambaneni nae tu kama mna maandiko ya kumpinga kama hayapo ukiristu ndio uko hivyo dini mbili unatafuta msaada kutoka kwa waislamu ha ha ha,pole sana.
 
Huyu niborasana kwanza nimkweli na nisahihi anao wafuasi wengi tu ,wanaume wangapi niwalevi na wazinifu?? Huonikuwa niwafuasiwake hao??wapo mashehe na mapadri weengi wazinzi na walezi ila huyu sio mnafiki kabisa.pia niuhuru wakuabudu huo muacheni jamani maadam havunji sheria.
ha ha ha yamewakuta wakina fulani pambaneni nae tu bila kuwahusisha mashehe kama mna hoja lakin kama hamna hoja ndio hivyo chungu lakini dawa.
 
*NABII WA KANISA LA POMBE SASA ATAKA KUMUOA WEMA SEPETU*

By Elizabeth
Mwandishi gazeti la Mwananchi online
___________________________
Dar es Salaam. Mkazi mmoja wa Dodoma anayejitangaza kama nabii, Tito Machija amesema watu wasimuone kuwa hana akili kutokana na mahubiri yake ambayo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na imani za waumini wa dini nyingine, hasa Wakristo.
Machija, ambaye anajulikana kama ‘Nabii Tito’ anahamasisha kuoa mke zaidi ya mmoja, ikiwa ni pamoja na kutembea na wafanyakazi wa ndani; anatumia pombe kunasa waumini na anadai hataki nyimbo za injili kwenye ‘ibada’ zake, ambazo nyingi hufanyikia baa. ‘Nabii’ huyo anaonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa amevalia kanzu nyeupe yenye misalaba miwili, chupa ya bia na kitabu kitakatifu aina ya Biblia. “Nawashangaa wanaoniona mimi sina akili, niko timamu kabisa na ninaelewa ninachokifanya,” alisema alipozungumza na MCL Digital. “Narudia tena kusisitiza kuwa walevi ndio watakaoingia ‘mbinguni’ na mafundisho ninayoyatoa ni sahihi,”
Tito amekuwa akionekana kwenye mitandao ya kijamii, hususani kwenye video fupifupi za Instagram, akiwa amevalia mavazi kama ya kichungaji na kucheza muziki huku akinywa bia na akiwa ameshika biblia. ‘Nabii’ huyo, mwenye wake watano na watoto 12, amedai kuwa kwa sasa hitaji lake kubwa ni kumuoa mwigizaji Wema Sepetu ili aungane naye katika huduma zake. “Wema ni msichana mzuri wa sura na umbo nataka nimuoe awe sehemu ya kanisa langu na nina imani watu wengi wataongezeka kwenye ibada ili kuja kumuona yeye na wake zangu hawana tatizo na hilo hata mmoja wao ananisaidia kumshawishi ili tuungane naye,” alisema Tito.
Tito anakiri kuwa ‘kanisa’ lake halijasajiliwa ila anadai kwamba anapata ufadhili kutoka kwa walevi mbalimbali. Tito amedai kuwa ‘kanisa’ lake lipo karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma na mara nyingi ibada zake huwa anazifanya kwenye baa na ana wafuasi wengi kiasi cha kutojua idadi yao.
Amesema kabla ya ibada kufanyika kwenye baa husika, huanza kwa kupeleka vipeperushi kwa mmiliki ili kuwapa taarifa waumini wake siku hasa ya ibada kufanyika katika baa hiyo. “Siku ya ibada ikifika naenda pale nikiwa na bia zangu za (anaitaja aina ya bia) ambazo nimeshaziombea. Zina ‘upako’. Kila anayetaka kuingia kwenye ibada analipa kiingilio cha Sh12,500. Ukilipa pesa hiyo unapata bia zako tano ndiyo huduma inaendelea usipotoa unafukuzwa,” alisema. Tito anajinasibu kuwa ana waumini wengi ambao hujitokeza kusikiliza mafundisho yake ambayo kwa kiasi kikubwa yanahamasisha ulevi na mapenzi kwa wasichana wa kazi wa majumbani.
Amesema kwenye huduma zake nyimbo za injili hazina nafasi kwa kuwa huwaburudisha waumini wake kwa nyimbo za kisasa. “Mtu akishaweza safari zake kichwani ukimuwekea bongofleva anacheza na kufurahi huku ibada inaendelea,” alisema. Nabii huyo amedai kuwa hakuna anachokizungumza kutoka kichwani mwake bali anasimamia mistari ya vitabu vitakatifu. “Wapo wengi wanaopinga huduma zangu ila nawaambia sijakurupuka nafanya kitu ambacho kipo na wala sioni kama ninakosea,” alisema.
Kwanini ‘ibada’ kwenye baa? Tito amedai kuwa anaingia makubaliano na wenye baa kwa kuwa ndiyo sehemu ambayo walevi hukutana na kwake ni mahali sahihi pa kutoa huduma. “Pale nakwenda na bia zangu kadhaa kwa ajili ya waumini watakaoingia kwenye ‘ibada’. Zikiisha naondoka zangu, nawaacha wanaendelea kununua za baa hapo ndipo mwenye baa anaponufaika,” alisema.
Watu wengi wamekuwa wakilaumu mafundisho ya Tito kuwa yanapotosha na wameiomba Serikali kuchukua hatua.
***MWISHO WA KUNUKUU***
Hakika kadri tunapoelekea kufungwa kwa historia ya ulimwengu huu, dunia itashuhudia matukio na vituko vya kustaajabisha zaidi.
 
Back
Top Bottom