GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,422
- 120,747
Huko nyuma nilikuwa nikipenda sana ujengaji wake wa hoja hasa katika masuala mazima ya Sheria na Katiba nchini Tanzania ila kwa bahati mbaya mno matukio mawili ya hivi karibuni tu yamenifanya nianze kuwa na wasiwasi na Shahada ya Uzamivu ( PhD ) aliyonayo Waziri wa Sheria na Katiba nchini Mheshimiwa Harrison Mwakyembe.
Ni huyu huyu mwezi mmoja uliopita alijitokeza tena huku akijigamba kabisa kuwa Chama cha Wanasheria nchini TLS ( Tanzania Law Society ) hakipaswi kugombewa na Mtu ambaye tayari ni Mwanasisa hoja ambayo mbele ya Mahakama na Mahakimu waliokwenda shule ilitupiliwa mbali na Mwakyembe akaangukia pua.
Kuonyesha kuwa hana mshipa wa aibu ni juzi tu huyu huyu Waziri Mwakyembe kakurupuka tena kwa kusema kuwa kuanzia tarehe 1 mwezi May wale wote ambao wanatarajia kufunga Ndoa basi sharti wawe na Vyeti vya Kuzaliwa uamuzi ambao tunashukuru Bosi wake Rais Dkt. Magufuli aliutengua kwa hoja zenye mashiko mbele ya Great Thinkers tuliotukuka kabisa.
Kutokana na matukio haya kutoka kwa Daktari wa Falsafa Mwakyembe je kwa utaalam na uchambuzi wenu wana JF mnadhani huyu Mtu ni Kielelezo tosha cha PhD makini au anawakilisha wenye PhD za hovyo hovyo nchini Tanzania?
Karibuni na naomba kuwasilisha.