Je, watoto ni mbolea ya penzi?

Je, watoto ni mbolea ya penzi?

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
6,250
Reaction score
11,924
Ni vyema mkulima anapopanda mbegu kutegemea mavuno.Japo Mbegu zingine huotea juu ya mwamba,nyingine zinasongwa na miiba,nyingine kuliwa na ndege na nyingine huota kwenye udongo mzuri.

Mke wangu aliponizalia mtoto nampenda kwa kasi zaidi na nafurahi mana mtoto kafanana na mimi kama vile genetic ili cut na kupaste.Je kuna ukweli kwamba wapendwa wanapojaliwa mtoto upendo huongezeka ama ni kawaida tu?

Nawatakia upigaji kura mwema.
 
Yapo mahusiano yanayoimarika baada ya kupata mtoto/watoto, yapo yatakayotetereka, na yapo yatakayovunjika kabisa. Inategemea.

Nishawahi kusikia mwanamama akilalamika kuwa mumewe anampenda mtoto wao zaidi ya anavyompenda yeye, noma ikaanzia hapo.

Nishasikia situations pia ambazo wapenzi walikuwa poa tu, super excited for the coming of a new member in the family. Kazaliwa mtoto yuko challenged, matatizo yakaanzia hapo. Jamaa anamlaumu mkewe kuwa hiyo imetoka upande wake wa familia.
 
Mwanamke kukuzalia ni kuweka rehani roho yake kati ya kufa ama kupona... so ukilifkria hilo upendo utaongezeka kama yeye alivyouongeza kwako.
 
Back
Top Bottom