Je, Watanzania tuna chochote cha kujifunza katika uchaguzi unaoendelea nchini Marekani?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Zilikuwa ni kampeni zilizogubikwa na hamasa kubwa lakini hatimaye siku imefika na kura ndizo zitaamua kama Wamarekani kwa ujumla wao wanaunga mkono taifa hilo linakoelekea chini ya utawala wa Rais wao Donald Trump. Kwa sasa nchi hiyo inakabiliwa na mgawanyiko mkubwa kufuatia hatua alizoamua kuchukua Rais huyo na mengi akiungwa na chama chake cha Republicans.

Katika kipindi amekuwa madarakani tofauti za kiitikadi, kidini, kirangi, kijinsia na hata kindugu zimejitokeza kiasi kwamba umoja wa taifa umetikiswa kwa kiwango fulani. Wapo ndugu hawatembeleani, wako majirani hawasalimiani, ziko familia zimegawanyika hata simu hawapigiani, wako marafiki hawaongei kama zamani na taifa limegawanyika pande mbili...wanaompenda Trump na wasiotaka hata kumuona.

Ni katika hali kama hiyo ya hewa uchaguzi wa leo unafanyika. Cha ajabu ambacho kimetuacha wengine tukikuna vichwa na kujiuliza, je nchi hiyo inao polisi? Kwa kweli tumebaki tunashangaa kwani hakuna sura, kivuli wala hata harufu ya polisi kwenye vituo vya kupigia kura, je vipi kama hali hiyo ingetokea hapa kwetu? Nadhani hapa kwetu idadi ya polisi labda ingekuwa sawa ama kuzidi idadi ya wapiga kura.

Hilo moja lakini la muhimu zaidi ni namna siku kama hiyo ya leo, kila mwananchi anayejitokeza kupiga kura ni lazima aruhusiwe kutumia haki hiyo ya kikatiba bila kikwazo hata kama kuna pingamizi. Ikitokea kwamba hakujiandikisha kupiga kura aruhusiwe kujiandikisha hapo hapo na kisha apige kura yake. Ikitokea kuna pingamizi dhidi yake, aruhusiwe kupiga kura kwanza huku ufumbuzi/utatuzi ukitafutwa.

Kura zinazopigwa wakati tatizo linashughulikiwa zinaitwa provisional votes na huwekwa sehemu maalum na huja kujumlishwa tu baada ya ufumbuzi kupatikana. Pia zipo kura zinazopigwa mapema kwa watu ambao siku ya kupiga kura ama watakuwa na dharura au hawatakuwepo kwa sababu mbali mbali. Hizi kura huitwa early votes. Na mwisho kuna kura zinazopigwa kwa njia ya posta kwa walio nje ya nchi.

Je Watanzania tuna lolote la kujifunza hapa?
 
Tofauti kubwa sana ya miaka 400+ na miaka 50 walahi
Hao walianza na hakuna mwanamke kupiga kura, ikaja mtu mweusi. NDUGU YANGU USIONE VYA ELEA VIMEUNDWA WALAHI
Naam, viliundwa na vyaelea, sasa taabu yetu ni nini? Waliunda magari na sasa tunatembelea hayo magari, mbona hatukusubiri hadi tuunde ya kwetu? Waliunda ndege na sasa tunatembelea hizo ndege, mbona hatukusubiri hadi tuunde za kwetu? Kila kitu wameturahisishia, sisi tunatakiwa tu twende na wakati, kwa nini hata hilo tushindwe? Ujinga au upumbavu?
 
Zilikuwa ni kampeni zilizogubikwa na hamasa kubwa lakini hatimaye siku imefika na kura ndizo zitaamua kama Wamarekani kwa ujumla wao wanaunga mkono taifa hilo linakoelekea chini ya utawala wa Rais wao Donald Trump. Kwa sasa nchi hiyo inakabiliwa na mgawanyiko mkubwa kufuatia hatua alizoamua kuchukua Rais huyo na mengi akiungwa na chama chake cha Republicans.

Katika kipindi amekuwa madarakani tofauti za kiitikadi, kidini, kirangi, kijinsia na hata kindugu zimejitokeza kiasi kwamba umoja wa taifa umetikiswa kwa kiwango fulani. Wapo ndugu hawatembeleani, wako majirani hawasalimiani, ziko familia zimegawanyika hata simu hawapigiani, wako marafiki hawaongei kama zamani na taifa limegawanyika pande mbili...wanaompenda Trump na wasiotaka hata kumuona.

Ni katika hali kama hiyo ya hewa uchaguzi wa leo unafanyika. Cha ajabu ambacho kimetuacha wengine tukikuna vichwa na kujiuliza, je nchi hiyo inao polisi? Kwa kweli tumebaki tunashangaa kwani hakuna sura, kivuli wala hata harufu ya polisi kwenye vituo vya kupigia kura, je vipi kama hali hiyo ingetokea hapa kwetu? Nadhani hapa kwetu idadi ya polisi labda ingekuwa sawa ama kuzidi idadi ya wapiga kura.

Hilo moja lakini la muhimu zaidi ni namna siku kama hiyo ya leo, kila mwananchi anayejitokeza kupiga kura ni lazima aruhusiwe kutumia haki hiyo ya kikatiba bila kikwazo hata kama kuna pingamizi. Ikitokea kwamba hakujiandikisha kupiga kura aruhusiwe kujiandikisha hapo hapo na kisha apige kura yake. Ikitokea kuna pingamizi dhidi yake, aruhusiwe kupiga kura kwanza huku ufumbuzi/utatuzi ukitafutwa.

Kura zinazopigwa wakati tatizo linashughulikiwa zinaitwa provisional votes na huwekwa sehemu maalum na huja kujumlishwa tu baada ya ufumbuzi kupatikana. Pia zipo kura zinazopigwa mapema kwa watu ambao siku ya kupiga kura ama watakuwa na dharura au hawatakuwepo kwa sababu mbali mbali. Hizi kura huitwa early votes. Na mwisho kuna kura zinazopigwa kwa njia ya posta kwa walio nje ya nchi.

Je Watanzania tuna lolote la kujifunza hapa?
Mag3 huna uwezo tena wakumshawishi mtu kufuata fikra zako mbovu, ndio sababu kipindi cha uchaguzi tulikukimbia kwenye jukwaa haukuwa na hoja bt ulijawa na vioja ukachanganya na mahaba. Kipofu hawezi kumuongoza anae ona. Kafie mbele!
 
Ha ha haa, umejiunga 2017! Ulinikimbia kwenye jukwaa wakati wa uchaguzi! Angalia kijana, maumivu huanza pole pole! Tulia kijana, meza aspro, oops, aspro utaijulia wapi!
 
Kweli we mtambo! Nipo jukwaani kitambo sana kijana wangu. Acha kukariri
 
Vipi Dada Mange mzima?
Samahani mambio, unajua JF kwa sasa imekuwa kama kokoro...je unajua kazi ya kokoro? Nakiri nimekosea kwani si kawaida yangu. Nimejishusha sana. Haya sasa naomba tujadili mada. Swali langu kwenye mada ni je, sisi Watanzania tuna chochote cha kujifunza katika uchaguzi nchini Marekani? Karibu.
 
Tofauti kubwa sana ya miaka 400+ na miaka 50 walahi
Hao walianza na hakuna mwanamke kupiga kura, ikaja mtu mweusi. NDUGU YANGU USIONE VYA ELEA VIMEUNDWA WALAHI
Hauna la kujifunza maana kwanza Demokrasia huijui hata ABC au unajua lakini tumbo linponza kichwa.

Pili dunia hii tuliyopo hakuna kinachoshindikana ila tu kutokan na ulevi na uchu wa madaraka viongozi wetu hawawezi kukubali kuendesha free and fair elections kwasababu wao sio machaguo ya wananchi watajikuta majalalani kama mbwa koko.

Endelea kula buku saba uteuzi unafuata. Ila ujue siku zenu zinahesabika.
 
Zilikuwa ni kampeni zilizogubikwa na hamasa kubwa lakini hatimaye siku imefika na kura ndizo zitaamua kama Wamarekani kwa ujumla wao wanaunga mkono taifa hilo linakoelekea chini ya utawala wa Rais wao Donald Trump. Kwa sasa nchi hiyo inakabiliwa na mgawanyiko mkubwa kufuatia hatua alizoamua kuchukua Rais huyo na mengi akiungwa na chama chake cha Republicans.

Katika kipindi amekuwa madarakani tofauti za kiitikadi, kidini, kirangi, kijinsia na hata kindugu zimejitokeza kiasi kwamba umoja wa taifa umetikiswa kwa kiwango fulani. Wapo ndugu hawatembeleani, wako majirani hawasalimiani, ziko familia zimegawanyika hata simu hawapigiani, wako marafiki hawaongei kama zamani na taifa limegawanyika pande mbili...wanaompenda Trump na wasiotaka hata kumuona.

Ni katika hali kama hiyo ya hewa uchaguzi wa leo unafanyika. Cha ajabu ambacho kimetuacha wengine tukikuna vichwa na kujiuliza, je nchi hiyo inao polisi? Kwa kweli tumebaki tunashangaa kwani hakuna sura, kivuli wala hata harufu ya polisi kwenye vituo vya kupigia kura, je vipi kama hali hiyo ingetokea hapa kwetu? Nadhani hapa kwetu idadi ya polisi labda ingekuwa sawa ama kuzidi idadi ya wapiga kura.

Hilo moja lakini la muhimu zaidi ni namna siku kama hiyo ya leo, kila mwananchi anayejitokeza kupiga kura ni lazima aruhusiwe kutumia haki hiyo ya kikatiba bila kikwazo hata kama kuna pingamizi. Ikitokea kwamba hakujiandikisha kupiga kura aruhusiwe kujiandikisha hapo hapo na kisha apige kura yake. Ikitokea kuna pingamizi dhidi yake, aruhusiwe kupiga kura kwanza huku ufumbuzi/utatuzi ukitafutwa.

Kura zinazopigwa wakati tatizo linashughulikiwa zinaitwa provisional votes na huwekwa sehemu maalum na huja kujumlishwa tu baada ya ufumbuzi kupatikana. Pia zipo kura zinazopigwa mapema kwa watu ambao siku ya kupiga kura ama watakuwa na dharura au hawatakuwepo kwa sababu mbali mbali. Hizi kura huitwa early votes. Na mwisho kuna kura zinazopigwa kwa njia ya posta kwa walio nje ya nchi.

Je Watanzania tuna lolote la kujifunza hapa?
Vipo vingi sana vya kujifunza na cha muhimu zaidi ni hamasa ya wapiga kura kujitokeza kwa wingi pia uhuru wa kufanya siasa na uhuru wa kuhoji chochote ambacho mpiga kura anaona kama kinaenda kinyume na kuna kitu kikubwa kinakuja ambacho Duniani kote kitakuwa Fundisho kubwa, ni kwanba endapo Democratic watapata viti vingi na kuwa washindi lazima watakuja na kura ya kutokuwa na imani na Rais Tramp na ikipigwa kura wakashinda inabidi Tramp afukuzwe kama Rais Zuma wa South Africa alivyofanyiwa, hivyo vipo njiani vinakuja kuushangaza Ulimwengu, hapa Ulaya kote na sehemu nyingi Duniani wanafuatilia huo uchaguzi kwa umakini mkubwa hususani China , Rusia na iran ambao ni Wapinzani wa Marekani ktk nyanja mbalimbali.
 
Baada ya uchaguzi kinachofuata ni kumpigia Tramp kura ya kutokuwa na imani nae na endapo republican hawatapa viti vingi vya kutosha ujue Babu Tramp atakuwa ni Rais mstaafu mda si mrefu huo ndiyo mpango wa Democratic kwani wamechoka na vioja vya Tramp.
 
Sidhani Hilo Kama Litatokea. Uwezekano Kiduchu Labda Ataserve Muhula Mmoja Lakini Sio Kuwa Impeached.
 
Hapa kwenu kila anaekwenda kituo cha kura tayari ana matokeo yake kichwani kiunoni ana panga la kwenda kumjeruhi msimamizi wa tume wacha polisi wawe wengi ukiachiwa na mkiachiwa kujiandikisha papo kwa papo msivyo na akili mtapiga kura mara ishirini kwa kukosa uaminifu!
 
vipo vingi sana vya kujifunza nitaandika ngoja nilale kwanza nitaipandisha hii thread/post yangu
 
Ha ha haa, umejiunga 2017! Ulinikimbia kwenye jukwaa wakati wa uchaguzi! Angalia kijana, maumivu huanza pole pole! Tulia kijana, meza aspro, oops, aspro utaijulia wapi!
Hao ndo vijana wa mwendo kasi mkuu.
 
Back
Top Bottom