Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Zilikuwa ni kampeni zilizogubikwa na hamasa kubwa lakini hatimaye siku imefika na kura ndizo zitaamua kama Wamarekani kwa ujumla wao wanaunga mkono taifa hilo linakoelekea chini ya utawala wa Rais wao Donald Trump. Kwa sasa nchi hiyo inakabiliwa na mgawanyiko mkubwa kufuatia hatua alizoamua kuchukua Rais huyo na mengi akiungwa na chama chake cha Republicans.
Katika kipindi amekuwa madarakani tofauti za kiitikadi, kidini, kirangi, kijinsia na hata kindugu zimejitokeza kiasi kwamba umoja wa taifa umetikiswa kwa kiwango fulani. Wapo ndugu hawatembeleani, wako majirani hawasalimiani, ziko familia zimegawanyika hata simu hawapigiani, wako marafiki hawaongei kama zamani na taifa limegawanyika pande mbili...wanaompenda Trump na wasiotaka hata kumuona.
Ni katika hali kama hiyo ya hewa uchaguzi wa leo unafanyika. Cha ajabu ambacho kimetuacha wengine tukikuna vichwa na kujiuliza, je nchi hiyo inao polisi? Kwa kweli tumebaki tunashangaa kwani hakuna sura, kivuli wala hata harufu ya polisi kwenye vituo vya kupigia kura, je vipi kama hali hiyo ingetokea hapa kwetu? Nadhani hapa kwetu idadi ya polisi labda ingekuwa sawa ama kuzidi idadi ya wapiga kura.
Hilo moja lakini la muhimu zaidi ni namna siku kama hiyo ya leo, kila mwananchi anayejitokeza kupiga kura ni lazima aruhusiwe kutumia haki hiyo ya kikatiba bila kikwazo hata kama kuna pingamizi. Ikitokea kwamba hakujiandikisha kupiga kura aruhusiwe kujiandikisha hapo hapo na kisha apige kura yake. Ikitokea kuna pingamizi dhidi yake, aruhusiwe kupiga kura kwanza huku ufumbuzi/utatuzi ukitafutwa.
Kura zinazopigwa wakati tatizo linashughulikiwa zinaitwa provisional votes na huwekwa sehemu maalum na huja kujumlishwa tu baada ya ufumbuzi kupatikana. Pia zipo kura zinazopigwa mapema kwa watu ambao siku ya kupiga kura ama watakuwa na dharura au hawatakuwepo kwa sababu mbali mbali. Hizi kura huitwa early votes. Na mwisho kuna kura zinazopigwa kwa njia ya posta kwa walio nje ya nchi.
Je Watanzania tuna lolote la kujifunza hapa?