Je, Watanzania tumelogwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Watanzania tumelogwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Expedito Mduda, Dec 8, 2010.

 1. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hakuna asiyejua mtu aliyetuingiza kwenye mkenge wa ajabu wa jitu linaloitwa Richmond ambalo sasa linazaa jitu kubwa zaidi linanyonya damu yetu linaloitwa Dowans.
  Hapo zamani tuliambiwa na PCCB kuwa mkataba na Richmond haukuwa na shida yoyote mpaka pale kamati ya Mwakyembe ilipotoa ukweli ulivyo. Sakata la Richmond limejadiliwa bungeni mwisho mmiliki wa kampuni hiyo hakupatikana maana hatukusikia jina lolote la nani anamiliki kampuni hiyo.
  Kila kukicha tunaambiwa TANESCO inalipa mabilioni ya mapesa kwa makampuni yanayozalisha umeme hapa nchini kama vile IPTTL.
  Leo hii tunaambiwa kuwa tunatakiwa kuwalipa Dowans Tsh. bilioni 185. Jamani, hivi sisi Watanzania tumekosa nini? Kwani hawa viongozi tunaochagua kutuwakilisha, wanawakilisha matumbo yao au wanataka sisi wenye nchi yetu tuseme nini!
  Jana au juzi tunamsikia waziri mkuu akikataa gari lenye gharama kama ya Tsh. 280! Hee nyela! Kwa kweli tumekwisha. Kwani Pinda hakujua kama atapewa gari hilo mapema? Nilitegemea asema waziri mkuu amekaza ununuzi wa magari ya kifahari! Eti wameshanunua gari halafu ya wananchi imeshaliwa kikubwa kwake ni kukataa gari!
  Serikali yetu unaundwa na watu gani jamani? Je, ni watu wa kawaida tu kama mimi kweli? Nahisi kama ni binadamu wa kawaida wangeshikwa na uchungu na hivyo kutanguliza maslahi ya nchi mbele. Wangeweza kuhakikisha huduma za jamii zinaboreshwa badala ya kujikita kwenye ununuzi wa magari ya kifahari kiasi hicho!
  Kila kunapokucha tunasikia upotevu wa mabilioni ya fedha za walipa kodi na wavuja jasho wetu. Hivi ndugu zetu viongozi hamuoni hali hii inatutisha sisi wananchi wenu?
  Mimi ninachoshangaa ni hiki hapa! Mmiliki wa Richmond hajulikani, na wakati huo huo mmiliki wa Dowans anajulikana na anatakiwa kulipwa hizo fedha, Je, Dowans hawezi kuulizwa amtaje Richmond maana Dowans ni mtoto wa Richmond?
  Tunawaomba taasisi zote za kututetea muone na msimame kidete kuhoji mambo haya yanakwenda kwa mtindo upi maana wavuja jasho wa nchi hii sasa wamechoka kuonewa!
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Waulize masikini wa fikra, elimu na kipato waliochagua CCM.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  "... mtu akikununulia kanga, akakupa na chumvi ukaunga kwenye mboga, kwa nini usimpe kura yeye aliyekupa hivyo vitu?"
  Haya ni maneno niliyowahi kusikia kwa masikio yangu kutoka kwa bibi mmoja! Can you deduce anything from this bro and relate it with your assertion!
   
 4. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sounds very anti-business!
  When people try to invest in this country, majority of you seem to be very skeptical and suspicious that these investors are trying to loot the country! Now Tanesco has to adhere to the contractual terms it entered during the signing of the agreement with Dowans.
   
 5. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wewe ni 'chaiwalla' huko india umekuja kutesa bongo.siku zenu zinahesabika.
   
 6. Mesh2lover

  Mesh2lover Member

  #6
  Dec 8, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Corrupt Governments cant avoid what you have witnessed. If the Government was not corrupt you wouldnt have Richmond and therefore you wouldnt have anything like DOWANS. Cyclic event caused by the people voted in power by a huge section of Tanzanians, Plus Ballot riging... welcome to the World.
   
 7. Mesh2lover

  Mesh2lover Member

  #7
  Dec 8, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ole wetu sis na vizazi vyetu.....
   
 8. Mesh2lover

  Mesh2lover Member

  #8
  Dec 8, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Lakini Siku inakuja...I can smell...it
   
 9. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli wachagua hovyo ndio walalamisha,mliambiwa elimu,afya bure mkadanganywa haiwekani,sasa wacha wawaonyeshe kazi mbadala wa hizo bilions maana hamkutaka hela yenu iwahudumie NA BADO ni kilio tu labda 2015 mtatia akiri wadanganyika haijalishi itikadi yako
   
 10. SUNGUSIA

  SUNGUSIA JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mungu ibariki Tanzania mungu nibariki niweze kuwa na uvumilivu wa kuyasikia haya maana bila wewe naweza kuwa sniper.
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Dec 8, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  siku ya nini?
   
 12. mpenda

  mpenda JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2010
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Is it Tanesco who signed the agreement with Richmond cum Dowans or was it the Ministry of Energy?? who is actually resposnible for these dubious contracts?
   
 13. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2010
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wajinga ndio waliwao, hii ndio bongo baba
   
Loading...