Je watanzania ni wakimya sana?

MD25

JF-Expert Member
Jan 28, 2012
3,074
1,018
Habari wana Bodi….

Kuna maswala mengi sana yananitatiza kuhusu hii nchi yangu, ningependa tujadili wote.

Madini.

Nchi hii ina madini kila kona ya nchi na hiyi sio siri tena, kila mtu anajua. Sasa linapokuja swala la uvunaji/uchimbaji wa haya madini, kwa hakika hakuna sehemu yoyote ile ya linalozunguka eneo la uchimbaji ambalo limefaidika kutokana na hayo madini. Wananchi wameendelea kuishi katika maisha ya dhiki sana, hakuna tofauti kati ya kipindi kabla ya uchimbaji na baada.

Na sio kwamba hao wachimbaji hawapati madini, la hasha, wanayapata, tani kwa tani, lakini sisi wananchi tunaozunguka hayo maeneo, hakuna lolote la maana tunalofaidika nalo.

Pamoja na hayo yote, sisi waTanzania tumendelea kuwa kimya bila kuchukua hatua yoyote kana kwamba tunachofanyiwa ni sawa tu.

Ajira.

Ajira sana imekuwa ya raia wa kigeni, hasa wa-Indi, hao ndio wanaajiliwa kuwa maBoss wetu na kulipwa mishaara minono. Yaani wanatoka India kuja kututawala sisi. Kana kwamba sisi hatuna elimu na wala hatuwezi kujiatawala.

Ukija kwenye hizi biashara ndogo ndogo za uchuuzi, huko ndio waChina wamejaa, wanauza hadi pipi, midoli, nguo,you name it…. Hata kwenye sekta ya ujenzi, waChina ndio wameishikilia, hata kujenga jingo la ghorofa 2 au 3 wachina wao, sasa jamani sisi wakandarasi wadogo na wa kati tukafanye kazi zipi?

Lakini wakati yote haya yanaendelea sisi kama waTanzania tunaendelea kukaa kimya kana kwamba, tunapendezwa na haya mambo.

Mikataba ya siri

Hii serikali ambayo inapaswa kuwajibika kwetu, sasa hivi, imeanza kuingia kwa siri mikataba mingi sana. Tena sasa hivi kila kukicha wanaingia mikataba yenye usiri. Sasa hivi speed yao ya kuingia mikataba yenye usiri imekuwa kubwa mno na yenye kutia shaka.

HITIMISHO

Haya yote yanayotokea sasa, yanakuja kuaribu moja kwa moja, maisha yetu ya sasa nay a watoto wetu. Ingawa haya yote yanatokea, lakini sisi waTanzania hatuchukui hatua stahiki za kuieleza hii serikali kuwa HAPANA, huku mnapotupeleka SIKO na inawapasa make pembeni kupisha serikali nyingine. Sisi waTanzania hatufanyi hayo, tupo tupo tu, ndio maana nauliza je, SISI waTanzania ni MAZEZETA?
 
hivi sasa wakazi wa kurasini wamelala barabarani ( kilwa road ) kupinga bomoabomoa , eti ardhi kapewa mwekezaji !
 
wewe ndiyo zezeta hakuna sehemu yoyote dunia mikataba ya nchi ikawa siyo siri. vua gwanda kwanza ndo ulete hoja yako hapa.
 
wewe ndiyo zezeta hakuna sehemu yoyote dunia mikataba ya nchi ikawa siyo siri. vua gwanda kwanza ndo ulete hoja yako hapa.

kwa kauri yako hiyo nimeamini nimazezeta iwe siri kwa nani?
kwani ni ulinzi wa nchi we KWELI ZEZETE X 100
 
kwa hoja yako hii inawezekana kabisa kauli ya Mh. Mkapa ilikuwa sahihi kwamba watanzania sisi tu wavivu wa kufikiri
 
Back
Top Bottom