Je wapo wana CHADEMA wanaoamini sera za CCM ni nzuri ila zimekosa watekelezaji?

Sitaki kulaumu sera za ccm direct ila mimi nadhani watekelezaji kwenye kile chama kwa sasa hawapo.Waliokuwa kipindi kile ndo walikuwa wanaziweza mwalimu,Kawawa,Sokoine hicho ndo kizazi cha utekelezaji.Ila hawa waliobaki kama hawazielewi sera zenyewe au kwa maslahi yao hazifai.Yote ya yote hata sera za chadema watu hatuzijui ila watu wanachotaka ni mabadiliko ya uongozi bila hata kujua kwenye hivi vyama vya upinzani kuna nini ndani yake.Huu ufisadi unaopigiwa kelele hata sera za ccm navyojua zinapinga ila nadhani unajua kwamba ndo wanaongoza kwa kujilimbikizia mali.
 
Wananchi wengi, si wanasiasa tu, hawazijui sera za ccm ama za chadema.
Nadhani wanasiasa tulionao, hasa toka upinzani hawajatumia muda wa kutosha kuwaelimisha wananchi juu ya sera za vyama vyao, hii inatokana na aina ya watu wenyewe tulio nao. Na bahati mbaya sana hata ccm tangu wamekaa madarakani hawajafanya jitihada zozote kuwaelimisha wananchi juu ya kitu kinaitwa sera.

Sasa kwakuwa tumejikita zaidi katika kutafuta uungwaji mkono ili kupata kura za kutuwezesha kushika madaraka, tunajikuta tunajikita zaidi katika kuhubiri ahadi kwa wananchi, na wananchi nao wanaonekana kuvutiwa zaidi na ahadi hivyo kupiga kura kwa misingi ya ahadi, hata kama hazitekelezeki bila kuangalia sera za vyama zinasemaje.

Kimsingi nikubaliane nawewe Mwanakijiji kwamba, wengi hatujui sera hata za vyama vyetu, hasa kwa wale ambao ni wanasiasa. Kwahiyo kutokana na hali hiyo tunashindwa kuzielezea kwa wananchi, na kwa kutokufanya hivyo wananchi wataendelea kubaki hawajui sera za vyama vyetu. Tumejikita zaidi kutafuta madhaifu binafsi ya watu katika maisha yao ya kila siku kwakuwa hatujui sera za vyama zinasema nini.

Kwa mtazamo wangu, sidhani kama ni sahihi kusema ccm wana sera nzuri, bali zimekosa watu wa kuzisimamia. Kimsingi sera za ccm hazitekelezeki pamoja na kwamba hawana watu wenye utashi wa kuzitekeleza. Tunakumbuka kauli ya raisi mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kukiri kwamba sera za ccm hazitekelezeki, sasa sijui mtu unahitaji nini tena kutambua kwamba sera za ccm hazitekelezeki!!
 
Naamini sera za CCM ni nzuri ila hazina watekelezaji na hawawezi tokea ndani ya CCM labda watoke chmama tofauti.

Kwa nini hawawezi tokea ndani ya CCM? Kuna viongozi wa CCM mahiri wanaokerwa sana na utendaji mbovu wa serekali tawala na ndo hapo itakapotokea revolution ndani ya CCM.
 
Mkuu Mwanakijiji,

Binafsi sioni utofauti kati ya kuwa na sera mbovu au zisizotekelezeka na kuwa na sera nzuri zisizo na watekelezaji...ubovu unabaki palepale kwenye sera!

Kama una sera nzuri lakini watekelezaji wabovu si unawaondoa? Lakini kama unaendelea kuwalea basi hata sera zenyewe pia zinakuwa hazina maana yoyote. Kama system inayounda sera nayo ina walakini then haijalishi kama sera ni nzuri au la, matatizo yatabaki pale pale.

Mfano mzuri ni hiki kigugumizi cha Serikali kuhusu kuwajibisha mawaziri wazembe...hapa utasema tatizo ni watekelezaji wa sera au mfumo mzima unaounda sera hizo??
 
Ndio mwana kijiji zipo sera na taratibu nzuri walizojiwekea kwa mfano hii nimeikuta kwenye kitabu chao Kanuni za uongozi na maadili toleo la 2010 inasema
Maadili ya kiongozi yakitetereka, Chama kitavurugika na nchi itakwenda mrama. Hivyo Jukumu la kila kiongozi litakuwa ni:-
  1. Kukijenga na kukilinda Chama
  2. kuwa na maadili mema na kutotenda maovu
  3. kutimiza wajibu wake kwa ukamilifu.
Mwisho wa kunukuu
My Take.
Je maadili ya kina Kikwete , Maghembe, Mukama, nape , Maghembe, Lusinde, Wasira, Ngeleja, Ridhiwani,Shigela, Adamu Malima (Changuoa vs laptop 4, Bunduki smg 2 na bastola 4 guest ) Mwigulu Nchemba nk.
wangekuwa waumini wazuri yaani wangekaa mbali na katazo hili la chama Chadema au chama kingine cha Upinzani kingekosoa nini?
 
Kimsingi SERA za CCM hazijawahi kutekelezwa kabisa katika nchi hii. Sera za CCM ukizisoma ni nzuri sana, ukiangalia Dira zao za maendeleo utasema hiki ndio chama. Mfano mzuri ni MKUKUTA, ukisoma mkukuta au hata MKURABITA vitabuni utaona kuwa ndio vitu vitakavyoondoa nchi hii katika umaskini. Ukirasimisha biashara na rasilimali za wanyonge ina maana watalipa kodi, watapata vipato rasmi, wachuuzi watapatiwa maeneo maalum nk. Lakini utekelezaji wa hizo sera za CCM haujawahi kufanyika kwa hiyo hatujui kama kinadharia ni nzuri au mbaya.

Binafsi naona kama CDM ndio njia ya kuiondoa ccm madarakani ili tuje na chama mbadala ambacho kitakuwa tayari kujifunza kule alikoshindwa mwenzie na kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa. CCM wameshindwa kabisa kupambana na rushwa na ndio sababu hakuna mtu mwenye woga na kutowajiba kwake
 
Sera zinazosubiri maamzi ya wafadhiri kamwe hazitatekelezeka, ndio maana CCM haina sera zake za kutekeleza ila za world bank na IMF.
 
well said,nakubaliana na wewe.nakumbuka kipindi cha kampeni 2010 ndio CDM ilikuwa inanadi zaidi sera zake lakini baada ya hapo naona iliyobaki ni kukosoa matokeo ya sera za ccm.Nadhani itabidi uongozi wa CDM walitilie maanani kwani watu wengi wanakimbilia CDM sio kwa sababu wanafahamu sera ya CDM bali ni kwa sababu wamepoteza matumaini na ccm baada ya maisha kuwa magumu.sasa hii ni hatari kwani ccm ikibadilika ghafla na kurudisha matumaini kidogo kwa wananchi,basi utashangaa watu wanaanza kurudi kwa ccm kwa sababu tu hawakuelimishwa na kuaminishwa ktk sera za CDM ili kuona tofauti na ccm.

Mkuu mlaizer umenena vyema sana. Inabidi CDM watumie mwanya huu kuwalisha watu sera hadi ziingie mioyoni. Watu hawaendi CDM kwa kuwa wamekubali sera bali wamekosa matumaini na wanatafuta mbadala ndiyo maana kuna kauli kama "Hata ukiweka jiwe na CCM wananchi watachagua jiwe". Hii ni hatari sana kwa CDM
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji hayo uliyosema ni sawa lakini sio sahihi katika hadhira na wakati husika.



Ingelikuwa ktk mdaharo wa Wanadhuoni, ktk Uchaguzi Mkuu (e.g. Presidential Debate), utunzi wa insha au Makala ya Mhariri hapo umahiri unatakiwa katika kupambanua tofauti za sera.


Leo hii tayari Serikali ni ya CCM namna pekee ya kuichallenge kimkakati ni kutumia nafasi na muda mchache ulionao (kumbuka vibali vya mihadhara, maandamano n.k ni zaidi ya kuitaarifu Polisi!), kutamka MACHACHE KWA NGUVU (HATA IKIBIDI KWA MACHOZI) YANAYOWAGUSA WANANCHI WA KAWAIDA (HUSUSANI VIJIJINI) NA KUAMSHA HISIA ZAO TAYARI KUKUUNGA MKONO NA KUUCHUKIA UPANDE MWINGINE!


Katika azima hiyo, unafikiri mwananchi (mwenye elimu ya msingi & sekondari) yuko tayari kuichukia CCM ukianza kueleza utofauti wa fiscal policies zinazotetewa na CCM dhidi ya za CHADEMA au ukimweleza kuwa Mh. Mbunge na Waziri wa tiketi ya CCM, Baby Kailama ameingia mkataba wa kifisadi ambao unaliingizia Taifa Ths Biilion 10 kila baada ya miezi miwili ambazo zingetosha kuwajengea na kuendesha kituo cha afya na kpia uwachimbia visima 5?



Kwamba ni lipi linalo mkuna huyo Mwanakijiji (sio wewe) kati ya kusema kuwa “Mh. Kikwete anafuata sera ya zamani toka enzi za Mwl. Nyerere ya kuendelea kukukuongoza katika Mikoa yote chini ya Serikali moja wakati Dr. Slaa anasisitiza kila Jimbo lijitawale”; au kusema “Mtakumbuka kuwa wakati wa uchaguzi Mh. Kikwete aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania je sasa mna maisha bora?” Au kuuliza kadamnasi kuwa “Wakati wa uchaguzi kauli mbiu chini ya kiongozi A. Kinana ilikuwa Ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi, je hayo ni kweli kwa Baraza la Mawaziri wa tiketi ya CCM nchini leo? “


Pili, ni bora nikukumbushe kuwa hakika kuna sera kibao tu ambazo ni nzuri zinazopigiwa debe na CCM kama ilivyo kwa CHADEMA , CUF etc. Kumbuka kuwa hata Wataalamu waliofanya tahmini kabla ya kuandaa Tz Vision 2025 kwenye utangulizi wao, walikiri kuwa tuna sera nyingi na mikakati mingi mizuri tu iliyowekwa kwenye makaratasi lakini haitekelezwi!



Nakuambia hata kama leo hii tutateremshiwa KATIBA MPYA iliyoandikwa na Malaika wenye sifa kedekede na uzoefu utakiwao; lakini kukawa hakuna utekelezaji au niseme hakuna kuheshimu hiyo KATIBA, hiyo ni mbaya mwanzo mwisho! Ni sawa na kumwalika mwenye njaa kunawa mikono, na baada ya muda usirudi toka huko jikoni kuleta chakula!
 
well said,nakubaliana na wewe.nakumbuka kipindi cha kampeni 2010 ndio CDM ilikuwa inanadi zaidi sera zake lakini baada ya hapo naona iliyobaki ni kukosoa matokeo ya sera za ccm.Nadhani itabidi uongozi wa CDM walitilie maanani kwani watu wengi wanakimbilia CDM sio kwa sababu wanafahamu sera ya CDM bali ni kwa sababu wamepoteza matumaini na ccm baada ya maisha kuwa magumu.sasa hii ni hatari kwani ccm ikibadilika ghafla na kurudisha matumaini kidogo kwa wananchi,basi utashangaa watu wanaanza kurudi kwa ccm kwa sababu tu hawakuelimishwa na kuaminishwa ktk sera za CDM ili kuona tofauti na ccm.

Mkuu mlaizer umenena vyema sana. Inabidi CDM watumie mwanya huu kuwalisha watu sera hadi ziingie mioyoni. Watu hawaendi CDM kwa kuwa wamekubali sera bali wamekosa matumaini na wanatafuta mbadala ndiyo maana kuna kauli kama "Hata ukiweka jiwe na CCM wananchi watachagua jiwe". Hii ni hatari sana kwa CDM
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umesema kweli. CDM na CCM lazima zitofautishwe na sera zake ambapo mwisho wa siku huathiri namna ambavyo huduma mbalimbali kama elimu, nishati, afya, usalama wa raia, utawala boras, kodi, mgawanyo wa rasilimali huweza kutolewa kwa wananchi. Kwa mfano, CCM bado wanaamini siasa ya Ujamaa kwa Kujitegemea (kwa maneno tu wakati wao wanaamini ubepari holela). Je CDM siasa yao ni ipi?

Je kuhusu muundo wa Serikali sera ya CDM inasemaje?
Je kwenye uhusiano wa kimataifa CDM kama chama kinaamini nini?
Je kuhusu elimu, technolojia, utamaduni nk CDM kina sera gani?

Kuuza sera ni suala muhimu sana kwa chama cha siasa. Wakati tunapigania kuinua maisha ya Mtanzania, bila ya kuwa na sera bora na uongozi madhubuti juhudi zetu haziwezi kufanikiwa.
 
Mimi ni mmoja ninaoamini kwamba sera za CCM ni nzuri lakini watendaji wote ni wabovu. Kwa hali hiyo hakuna atakayeweza kuzi-practise hizo sera, hivyo ni bora tuanze moja na CDM badara ya kutegemea kuwa CCM watajirekebisha. Kama wameshinda kwa miaka 50 iliyopita, wakisimama kwenye majukwaa utawasikia "ccm hoyeeee - tunachukua, tunaweka - waaa! " huoni kuwa hata wao hizo sera za chama chao hawazijui? na kama wanazijua basi wanaona ugumu kuzitekeleza kwa sababu hazina mwanya wa rushwa wala ubadhirifu wa mali za Umma. MNISAMEHE WATOTO WA MAGAMBA NA MAGAMBA YENYEWE.
 
nILIBAHATIKA KUSOMA ILANI YA UCHAGUZI 2010 YA CDM; SIJUI ULIKUWA MBALI NA SERA ZA CDM?
 
Ninaamini sera za CCM zinakosa watelezaji makini, waadilifu na watumishi bora kwa wananchi.
 
kwa uelewo wangu sera ni policy na hizi policy ndizo zinzotumika kutekeleza ahadi, kutatua na kukabiliana na matatizo na changamoto nyingi za ndani na nje ya taifa husika. kama alivyoonyesha MM sera siyo ahadi (kujenga madaraja nk) kwa mfano sera mojawapo ya serikali za CCM ni kama ile ya kuuza na kunabinafsisha mashirika ya umma, ile ilikua sera ya CCM muda wa Mkapa kukabiliana na hasara za mashirika haya, kutaka kuongeza pato la taifa nk sera mojawapo ya serikali ya Jk ilikua/ au bado ni kilimo kwanza ambayo ililenga/inalenga katika kuongeza ufanisi katika sekta ya kilimo na hivyo kuongeza pato la taifa..hii ni mifano ya sera.

Hapa kinachochanganya watu wengi ni tofauti ya sera, itikadi, mfumo na filosofia binafsi ya chama husika. utunzi na utekelezi wa hizi sera unatokana na vitu hivi nilivyovitaja sasa hapa ili kujua kweli kama sera za CCM ni nzuri au la inabidi kwanza ujiulize haya ;1. itikadi iliyopo ni ipi? 2. ni nini mfumo wa utawala wa CCM? 3. ni nini filosofia ya CCM kuhusu uongozi, na jamii inayoongozwa kiujumla? na baada ya kujibu haya utaona kama sera za CCM kiujumla zinaendana na itikadi yake, filosofia, na mfumo wake kiutawala

1. itikadi iliyopo ni ya kiliberali (demokrasia, haki na uhuru wa binadamu, soko huria)
2. mfumo wa utawala kwa sasa ni Kleptokratia (watu wachache kujinufaisha na uongozi wa umma kwa gharama ya walio wengi)
3. CCM imechanganyikiwa haina filosofia maalum, (bado wanaishi kwenye maandishi ya ujamaa huku wakila kivulini kwenye ubepari)

Hitimisho; sera nyingi zina malengo ya kukuza pato la taifa, (lakini mfumo wa uongozi na kukosekana kwa filosofia mahsusi ya chama kuwaongoza viongozi wake wakuu kunafanya utekelezaji kua ndoto.
 
Back
Top Bottom