Je wapo wana CHADEMA wanaoamini sera za CCM ni nzuri ila zimekosa watekelezaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wapo wana CHADEMA wanaoamini sera za CCM ni nzuri ila zimekosa watekelezaji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 30, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Baadhi ya viongozi na hata wanachama wa kawaida wa upinzani wanapokosoa CCM wanakosoa zaidi watu na chama kama chama. Katika kikao cha Bunge kilichopita kwa mfano ni wachache sana ambao wamefanya mashambulizi ya moja kwa moja (direct assault) ya sera za CCM. Nimeanza kuwa na wasiwasi kuwa yawezekana wapo watu ambao wanaamini kuwa sera za CCM "kimsingi" ni nzuri na kuwa "ziko vitabuni" na hivyo wanaamini CCM ikibadilisha watendaji mbalimbali basi sera hizo zitaanza kutekelezeka.

  Matokeo ya maono haya ni kuwa CDM inaweza isijikte sana katika kuhamasisha wananchi kuelewa sera zake na mipango yake ambayo ni 'tofauti' na ile ya CCM. Hili linaweza kuwafanya baadhi ya viongozi na wanachama kutokujali sana kuzisoma na kuelewa makosa ya msingi (fundamental errors) za sera za CCM na hivyo kuzikosoa na kupendekeza sera za CDM kuwa ni bora.

  Hii inawezekana kutokea kwa sababu ama baadhi ya viongozi au mashabiki hao wa CDM hawaamini kuwa sera za CDM ni bora kuliko zile za CCM. Kwangu mimi huu ndio msingi wa mgongano unavyopaswa kuwa; kwamba tofauti zetu za kisiasa zisiwe kwa ajili ya msingi wa watu - yaani badala ya kushambulia mtu au kundi la watu ishambuliwe sera. Mfano mzuri wa kuelewa hili ni kuangalia kampeni ya urais ya Marekani ambapo watu wa Republicans hawasiti kuonesha waziwasi na kudai kuwa sera za Obama zimeshindwa katika maeneo mbalimbali huku Obama akirudia hoja ya kuwa wamarekani wasizirudie zile "sera zilizoshindwa za zamani". Iwe ni kwenye masuala ya kodi, nishati, mazingira, usalama n.k hoja ni kulinganisha sera za vyama hivyo viwili na sera zile zinazokubalika zaidi ndizo ambazo zitakipatia chama husika ushindi.

  Kwa muda sasa hatujasikia ukosoaji huu wa sera za CCM mara nyingi tunasikia ukosoaji wa matokeo ya sera zenyewe bila kujali sana sera zilivyo. Kwa mfano, tatizo la nishati nchini kwa watu wengi yawezekana likaonekana ni tatizo la nani anasimamia wizara ya nishati au watendaji fulani; lakini kwa mtu yeyote anayeangalia anaweza kuona kuwa tatizo ni sera nzima ya nishati ni mbovu tangu ilipoundwa upya mwaka 1992 na mabadiliko ya baadaye. Ni sera ambayo kushindwa kwake hakuna utata kwani matokeo yanajulikana. Watu lazima waseme pasipo utata kuwa sera ya CCM ya nishati imeshindwa! Lakini sera ya CDM ni ipi?

  Ukiamini kuwa tatizo ni 'watu' na siyo sera CCM na serikali itaitikia kwa kubadilisha watu na siyo sera! Matokeo yake wataingizwa watu na kutoka na matatizo yatabakia pale pale kwa sababu tatizo la msingi ni zaidi ya watu. Wapinzani (iwe CDM au wengine huru) wanapolalamikia matokeo ya sera - elimu, ajira au maji - na kutaka "serikali" ibadilishe au "ilete" mpango fulani wanafanya hivyo wakionesha kuamini kuwa wanakubaliana na sera yenyewe at least in principle! Hili ni kosa la kimkakati na ni kosa la kisiasa. Kwa sababu kama serikali ikisikiliza na kufanya mabadiliko ya juu juu wapinzani hawa wanaweza kujikuta wanatoa pongezi "kuwa serikali imetusikiliza" wakati sera ya msingi inabakia pale pale!

  Lakini hatari zaidi ambayo ninaiona ni kuwa kwa kushindwa kutangaza sera mbadala za sekta mbalimbali (alternative policies) CDM kama chama kinaweza kujikuta kikijulikana zaidi kwa kufichua ufisadi, kuilaumu sserikali na kuikosoa serikali kuliko kujulikana kwa sera zake mbadala. Kwa mfano, ni wangapi wanachama wa CDM wanaojua sera za CDM kuhusu nishati, elimu, maji, ulinzi na usalama, michezo n.k? Ni wangapi kwa mfano ambao huimba na kusema "people's power" kwa furaha wanajua CDM inamtazamo gani wa kisera kuhusiana na misaada ya kigeni? Je viongozi wote wa CDM wanajua sera zao na wanaweza kuzipambanua? Katika mikutano mbalimbali ya CDM ni lini na wapi ambapo kumewahi kuwepo na mkutano wa "policy discussion" ambapo wananchi walikaa na viongozi wao kuzungumzia sera zao? Kwa mfano, wadau wa sekta ya utalii wakiuliza hivi CDM sera yenu ya utalii ni ipi nani anaweza akatoa jibu ambalo kila mwana CDM analijua?

  Sasa majibu tuliyayozea ni yale yale - Sera za nini tunataka kwanza CCM watoke madarakani halafu tutazungumzia sera na kuwa sera za CDM zipo kwenye tovuti kwa mtu yeyote kujisomea! Majibu yote yana hatari ndani yake. Hatari yake ni kuwa watu wanaweza kujikuta wanajitahidi kukosoa serikali kwa nguvu sana na kukosoa matokeo ya sera za CCM kumbe wakifanya hivyo wanaonesha wanakubali moyoni uzuri wa sera za CCM na hivyo kumbe wanagombania kupata nafasi ya kuzitekeleza sera za CCM na siyo sera za CDM!

  Jiulize: Kama wewe ni mwana CDM au shabiki (kama mimi) je tatizo lako na CCM ni nini hasa? Je, ni kwamba CCM imekosa watu wenye uwezo na uadilifu wa kusimamia sera zao na hivyo wawaondoe ili waitawale nchi vizuri au tatizo lako ni sera za CCM kuwa zimeshindwa na hivyo ni bora CCM wote waondoke ili hatimaye CDM ije kushika madaraka na kutekeleza sera zake ambazo yumkini ni bora kuliko za CCM? Je unaamini sera za CDM kwa kila eneo ni bora kuliko za CCM?
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  mkuu sera bora ni zile zinazo tekelezeka. Kimsingi sera za ccm hazitekelezeki na zinabaki vitabuni labda cdm wakipata dola wanawezakutekeleza zakwao.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  wengine wanaweza kusema hazitekelezi kwa sababu zimekosa watekelezaji kwa hiyo wakipataikana watekelezaji - hata kutoka upinzani - zinaweza kutekelezwa!
   
 4. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,763
  Likes Received: 8,036
  Trophy Points: 280
  Mkuu MM, sera za CHADEMA na za CCM na chama chochote kile lazima kwa kiasi fulani zifanane kwani mahitaji ya wananchi ni yale yale. Hata CHADEMA au TLP ikiingia madarakani wananchi bado watahitaji barabara, maji, huduma za afya na kadhalika. Tunakopishania na magamba ni MFUMO WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UMMA NA UONGOZI (mgawanyo wa madaraka).

  Kwa msingi huu, utakuwa ni UJUHA kwa CDM kupanda majukwaani na kuwaeleza wananchi kuwa tukiingia madarakani tutajenga barabara na kuleta mbolea vijijini. Haya serikali yoyote ile duniani lazima iyafanye. Kinachofanya CDM ni kuwaeleza wananchi ni wapi utekelezaji wa ahadi za upatikanaji wa huduma kuna mikwamo. Na ndio maana tunaohitaji mabadiliko tunalia na mfumo wa udhibiti na usimamizi wa rasilimali.

  Lkn hata hivyo sikupingi moja kwa moja, upo uwezekano mkubwa nguvu ya umma ikawa sera na tukajikuta baadaye hatukumbuki ni nini cha ziada katika kutuunganisha zaidi ya COMMON ENEMY ambaye ni CCM na RUSHWA ZAKE. Pamoja sana mkuu MM
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  SIAMINI KATIKA SERA

  naamin katika utekelezaji.........kwa sera CUF wana wazidi vyama vyote
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280

  Labda huelewezi sera ni nini; kusema tutajenga barabara siyo sera! kusema tutajenga hospitali siyo sera! au kusema tutaelimisha watu wengi zaidi siyo sera na huko hakuwezi kuwa kufanana. Kwani hakuna chama ambacho kitasema "hatutajenga barabara, au hospitali au mashule". Tunapozungumzia sera tunazungumzia namna ya kufikia malengo hayo. Yaani, kanuni za msingi za kufikia malengo tuliyojiwekea na namna ya kuyafikia malengo hayo na vile vile mwelekeo wa kisheria ambao utatokana na sera hizo.

  Kwa mfano, ofisi ya CAG sasa hivi ni ya kiuchunguzi tu - hii ndiyo sera ya CCM. Jukumu lake ni kuchunguza sana na kuonesha ubovu lakini haina nguvu ya kwenda zaidi ya hapo. Je CDM nayo sera yake ni hiyo hiyo?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  sasa kwanini tusirudi kwenye chama kimoja na kupata sera nzuri na watekelezaji wazuri? au kuanzisha kukopeshana watekelezaji?
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  sera za ccm ni viini macho..hakuna sera kule zaid ya sera a udokozi
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kama ilivyo kwa sera/ilani za ccm ndivyyo ilivyo kwa sera za kitaifa. Watakuwa nazo nzuri ila tatizo hamna watekelezaji
   
 10. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Naamini sera za CCM ni nzuri ila hazina watekelezaji na hawawezi tokea ndani ya CCM labda watoke chmama tofauti.
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mwanakijiji umeuliza swali gumu na nadhani umeona kwamba watu hatuelewi sera ni nini na ahadi ni nini? Wana CCM hawajui sera za CCM na wana CDM hawajui sera za CDM. Achilia mbali sera hata itikadi za vyama watu wazijui. Watanzania huwa tunasubiri kuona tunaahidiwa nini majukwaani na wala siyo sera. Mgombea akiahidi kwamba atatynunulia meli basi tunampa kura akisema nitashusha bei ya unga basi naye anapata kura. Mkuu ungezileta sera za vyama vyote tuzulione na kuzisoma ili tujue kama zinatekelezeka ama la. Na kama hazitekelezeki ni kwa sababu y watekelezaji au sera zenyewe hazieleweki au ni ngumu mno.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  unazijua kwa kiasi gani sera za CDM kulinganisha na za CCM?
   
 13. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  mkuu kama ni mfumo tunatakiwa ku overhaul kila kitu. Kama tatizo ni serikali ya ccm utamweka nani atekeleze? Mbona wote ni walewale wakubebana? Labda tutupe wote na tuweke watekelezaji wengine wa sera.
   
 14. M

  Marytina JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hata kikirudi chama kimoja itakuwa poa kama wakiwepo watekelezaji wazuru wazalendo.
  Kumbuka Jerry Rowlence alivyoitwaa ghana kijeshi akaiongoza kufikia mafanikia mazuri kabisa

  SERA za CCM hazina ubaya ila hamna mtekelezaji na atakayejaribu kuzitekeleza ataaandamwa na VIONGOZI WA JUU WA ccm
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote lazima nikubaliane na wewe kwa 100% kwamba siasa zetu, kuanzia kwa wanasiasa wenyewe hadi kwa mashabiki/wapenzi wao; ni siasa dhidi ya wanasiasa na katu si sera! Huu, ni udhaifu mkubwa....kwa namna nyingine inawezekana kabisa tunashabikia tusichokijua!!

  Nikirudi kwa upande wa CCM, tatizo ni yote mawili; sera na watekelezaji/wasimamiaji wa sera husika! Zipo baadhi ya sera ambazo ni mzuri tu lakini utekelezaji wake ndio mbovu! Kwa sera hizi hizi zilizopo, lau kama pangekuwa na watendaji waadilifu na wenye kuwajibika(sio kuwajibika baada ya kuharibu), basi leo hii tungekuwa somewhere ahead. Sera mbovu, ama zenye mapungufu zinapokutana na watendaji na watekelezaji wabovu ndipo inageuka kuwa dhahama zaidi! Sera hizi mbovu zinakuwa 100% failure ni kwavile tu watekelezaji wenyewe ni wabovu....hata hivyo, ubovu unaotokana na kujali zaidi maslahi binafsi!!
   
 16. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  well said,nakubaliana na wewe.nakumbuka kipindi cha kampeni 2010 ndio CDM ilikuwa inanadi zaidi sera zake lakini baada ya hapo naona iliyobaki ni kukosoa matokeo ya sera za ccm.Nadhani itabidi uongozi wa CDM walitilie maanani kwani watu wengi wanakimbilia CDM sio kwa sababu wanafahamu sera ya CDM bali ni kwa sababu wamepoteza matumaini na ccm baada ya maisha kuwa magumu.sasa hii ni hatari kwani ccm ikibadilika ghafla na kurudisha matumaini kidogo kwa wananchi,basi utashangaa watu wanaanza kurudi kwa ccm kwa sababu tu hawakuelimishwa na kuaminishwa ktk sera za CDM ili kuona tofauti na ccm.
   
 17. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,763
  Likes Received: 8,036
  Trophy Points: 280
  Na ndio nikakueleza focus ipo kwenye kubomoa mfumo wa ugawanywaji wa madaraka kwani uliopo unaleta udumafu. Na ndio msingi wa vuguvugu la kudai katiba mpya, kupunguza madaraka ya rais kuteua wakuu wa mikoa na wilaya. Sera hapa ni kurudisha nguvu hiyo kwa wananchi au bado hujanipata?
   
 18. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Mimi nilikuwa Mwanachama damu wa CCM nakiri kwamba sijazisoma sera za chadema zote baadhi nazifahaamu lakini naamini CCM wana sera nzuri sana labda kwasababu ya ukongwe wake ishu wamekosa viongozi wazalendo watekelezaji na kile kitabia cha kulindana ndani ya chama dhidi ya wanao kwenda tofauti na sera ndicho kimenifanya niachane na CCM kwasababu naamini haitatokea hata siku moja sera za chama zikafanyiwa kazi, na nilifikia mahala pa kuichukia kabisa CCM baada ya kuona inafanya mambo kama zima moto, hebu fikiria pamoja na kuwa na sera nzuri kwanini mambo mengi inayafanya baada ya kuona upinzani ukija juu? Hebu fikiria kwa chama makini na sera zake kulikuwa kuna haja ya kuanza mchakato wa katiba mpya sasa? mimi nijuavyo hii haipo hata kwenye ilani ya chama. Ninaamini hakuna chama chenye sera za kuangamiza nchi, hata kama chadema itakuwa haina sera nzuri kama CCM still ina watu wanaoonyesha uchungu na nchi na hizo sera chache nilizokwisha zipitia naamini wanawza kutupeleka mbele. Mimi kama mwajiri wa wanasiasa nimejihakikishia kwamba CCM hawawezi nataka niwajaribu chadema
   
 19. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu MM,Nionavyo mimi,tatizo la Tz sio sera nzuri,tuna sifa ya kuandika mipango mizuri sana lakini utekelezaji ndio tatizo.Kinacholeta taabu ni kule kuhama kwenye misingi iliyosimamia utekelezaji wa sera hizo yaani,uwajibikaji,uzalendo,uadilifu,maslahi ya Taifa n.k
  Kinacholeta mvuto wa Chadema kwa wananchi si sera(naamini hata wanachadema wengi hawazijui sera za chadema)bali ni zilke ahadi na matumaini ya kurejesha misingi ya utekelezaji sera iliyosahaulika.Kwa maana hiyo basi ikitokea CCM wakaamua kurejesha misingi hiyo kwa kumaanisha na kwa vitendo vitakavyoonekana dhahiri kwa wananchi,upinzani waweza kukosa kitu cha kupigia debe,sasa kwa vile ccm ilishaanguka dhambini na haitaki kutubia dhambi zake kwa wananchi,ndio maana CDM inaonekana mbadala.Binafsi nakubali kabisa kuwa kuna sera nzuri ccm lakini misingi ya utekelezaji imepotea ama kupuuzwa baada ya dhambi za rushwa,ufisadi ubinafsi n.k kushamiri
   
 20. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Ninavyofahamu mimi ni kwamba, majukumu ya CAG yanaishia kwenye ukaguzi. Hata hivyo,hivi sasa wanaenda mbali zaidi kwa kuangalia na VALUE FOR MONEY....tofauti na zamani. CAG, bila shaka wanaishia hapo lakini kuna DCI na TAKUKURU wamekuwa attached.....kwenye ukaguzi husika pakionekana pana harufu ya RUSHWA, hapo TAKUKURU anaingia, na pakionekana na harufu ya wizi, DCI anafanya kazi yake! Tatizo, TAKUKURU, DCI (pamoja na DPP) are all dead!
   
Loading...