Uchaguzi 2020 Je, Wapinzani wana uwezo wa kuunda Serikali imara?

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wana bodi,

Kampeni zime pamba moto, ahadi zinazidi kumwagwa kila kona, wana siasa wakongwe wanazidi kuserebuka kwenye kila hafla, kitu ambacho kime kuwa cha kawaida kwenye mchakato huu wa kuweza kuwa fikia wapiga Kura.

Swali ambalo nina jaribu kujiuliza ni: Je, wagombea wa Vyama vya Upinzani wanaweza kuunda serikali imara. Kuna mengi ambayo wapinzani wanasema kuhusu chama tawala lakini endapo wapinzani watashinda uchaguzi huu, baraza la mawaziri litakuwaje? Mabalozi watakuwa wakina nani? Watawezaje kuendesha nchi?

Ni rahisi kuwa shambulia wana CCM kwa maneno lakini tuki jaribu kutafakari kwa undani zaidi tutagundua kwamba Wapinzani hawana uzoefu wowote wa ku endesha nchi na ina wezekana kwamba hawana mahusiano mazuri ya kutosha na nchi zingine.

Viwanda vyote wanavyo panga kufufua vita kuwa havina muendelezo wowote bila mahusiano mazuri yakutosha na nchi zingine. Huo ni mfano mmoja tu lakini undeshaji wa nchi bila mahusiano mazuri na yakutosha na nchi zingine ni kitu ambacho haki wezekani.

Kuwa na chama kikongwe kilicho wekeza kwenye mambo hayo kina uwezo wa ku mjengea mtu yeyote mahusiano ambayo ni ya muhimu sana.

Tafakari,

Jumatatu njema.
 
Uzoefu? Kipindi Nyerere anapewa nchi alikua na uzoefu wa Urais au kuongoza nchi before? Solution ilitolewa na Katiba ya warioba kuwa mawaziri wasitokane na wabunge ili kutoa nafasi kwa wataalamu kusimamie sekta nyeti.

So CHADEMA ikiingia wao ni kusimamia sera ila utekelezaji utahusisha wataalam ambao hawana chama. Kwahiyo don't picture serikali ya upinzani kuwa itajaa amateurs ilihali taasisi kma BOT iwe CCM iwe CHADEMA watendaji ni walewale.

Kinachofurahisha wapinzani wengi wakienda CCM be it Kitila, Mtatiro, Mghwira, Kafulila, Shonza, Waitara ,n.k walipewa promotions serikalini. Ssa kma Rais wenu amewaamini hao, kivipi ww uone upinzani hawawezi deserve kuongoza serikali?
 
Uzoefu? Kipindi Nyerere anapewa nchi alikua na uzoefu wa Urais au kuongoza nchi before? Solution ilitolewa na Katiba ya warioba kuwa mawaziri wasitokane na wabunge ili kutoa nafasi kwa wataalamu kusimamie sekta nyeti...
Huwezi ku linganisha Tanzania tuliyo nayo mwaka 2020 na Tanzania tuliyo kuwa nayo mwaka 1961. Nyerere kuwa rais wa kwanza kuna tokana na yeye kuwa mtu aliye ongoza Tanzania kutoka katika mifumo ya ki koloni. Kupata undani wa kilicho tokea kipindi hicho ni ngumu lakini vile vile katika masuala haya ni vyema kuji uliza kama kulikuwa na mtu mwingine ambaye angekuwa sahihi zaidi kuliko mwalimu Nyerere.

Uliyo yaeleza yana weza kuwa sahihi lakini hatua ambayo wizara zina endeshwa na wataalam ita tubidi tu ingie mchakato wa kupata katiba mpya. Katiba tuliyo nayo haitu ruhusu kufanya hivyo. Hoja niliyo jenga ni kama wapinzani wana ma husiano ya kutosha na nchi zingine. Mahusiano na nchi zingine ni muhumi sana, na hisi kitu namba moja katika uendeshaji wa nchi.
 
Nyerere alikuwa na uzoefu gani na alipataje kuunda serikali tafakari.

Nchi yenye wasomi wengi na vyuo vingi hawawezi kukosekana wakuteuliwa kuwa watendaji was serikali, lakini pia tunajua na tunaamini watendaji wa serikali ukiondoa mawaziri ambao Ni wanasiasa hao wengine siyo wanasiasa.
 
Nyerere alikuwa na uzoefu gani na alipataje kuunda serikali tafakari.

Nchi yenye wasomi wengi na vyuo vingi hawawezi kukosekana wakuteuliwa kuwa watendaji was serikali, lakini pia tunajua na tunaamini watendaji wa serikali ukiondoa mawaziri ambao Ni wanasiasa hao wengine siyo wanasiasa.
Mada kuu ni kama wapinzani wana mahusiano mazuri na yakutosha na nchi zingine.
 
Jibu swali langu!Unavyodai CCM wako imara katika kuunda serekali imara unamaanisha akina Bashite,Ndugai,Chenge,Tulia,e.t.c ambao ndiyo wataunda serekali ya CCM wako imara?!Nikisema umelogwa nitakuwa nimekuonea?
Mada kuu ni kama wapinzani wana mahusiano ya kutosha na nchi za nje. Hicho ni kitu muhimu sana, au vipi mzee wa Sumbawanga
 
Mkuu umeandika vizuri ila umekosea kusema wapinzani hawana uwezo wa kuunda selikari, hivi Tanzania ambayo Ina watu mil hamsini wanashindwaje kwa mfano, hata kumchukua afande Mroto kuwa waziri Mambo ya ndani itashindikana acha madharau mkuu.
 
Tuwe wakweli, Lissu anaweza kuongoza Serikali? Kwa akili ipi? Siwezi kumzunhumzia Salum Mwalimu maana huyo hata U Sheha hawezi seuse Umakamu wa Rais?
 
WATU WAKO WANAUANA KISA UENYEKITI WA CHAMA, SEMBUSE KUUNDA SERIKALII??
Hapo ndio maajabu yanapoanzia. Hii nchi sio saccos, watanzania lazima wajue huu ukweli. Kule kurukaruka jukwaani kwa jazba, kukashfu kila Serikali ifanyacho hakuwezi kuwasaidia. Watanzania wanaona, wanaelewa na wataamua.Nyie na saccos yenu, jipangeni kwanza 2040.
 
Mkuu umeandika vizuri ila umekosea kusema wapinzani hawana uwezo wa kuunda selikari ,hivi tz ambayo Ina watu mil hamsini wanashindwaje kwa mfano ,mkuu mfano hata kumchukua afande mloto kuwa waziri Mambo ya ndani itashindikana acha mazalau mkuu
Soma kichwa cha habari pamoja na maelezo. Mada kuu ni kama wana mahusiano mazuri na nchi zingine
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom