Je, wanaCHADEMA watagomea kupeleka watoto wao shule na vyuo vitakapofunguliwa kama walivyofanya bungeni?

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
921
1,658
Wakuu,

kwa hali inavyojidhihiri yenyewe chadema wanaonekana kujali sana swala la afya na hatua mathubuti ya kujikinga na corona

Itakumbukwa mapema mwezi huu wabunge wa chadema waliamua kujitenga na kugomea kushiriki vikao vya bunge kwa tahadhari ya ugonjwa wa corona.. hii ilikuwa right move kiukweli japo bunge na serikali viliendelea na shughuli zao kama kawaida

Najiuliza hapa, corona bado ipo tena ya kiwango cha bombadia na mheshimiwa rais Magufuli ametangaza uwezekano wa kufungua shule na vyuo ilihali hali halisi ya corona bado iko kama kawaida

Je, tutarajie wanaCHADEMA na vyama vya upinzani kuwaongoza na kuzuia watoto wao kurudi shule na vyuoni kwa hofu ya kupata corona?
 
Hawawezi gomea ikiwa watahakikishiwa usalama wa watoto au vijana wao

It is never too late to begin. Start now
 
Mkuu shule zipi unazoongelea wakati jemedari bado yuko chimbo mwezi wa pili sasa?

Kwa takwimu zipi shule au ligi zifunguliwe?

Mbona mengine haya yako wazi mno mkuu? Keep them talking.

Ya uchaguzi mkuu umeyasikia tena?
 
Kama kweli korona ipo kwa kiwango cha bombadia kama ulivyosema, basi hilo wala haihitaji kuwa CHADEMA ili kuona kuwa ni hatari kufanya hivyo.

Au ni CHADEMA tu ndio ambao watoto wao wanaathiriwa na korona?
 
Sijui ni kwanini siasa zimeingia ndani ya maisha kiasi hiki. Hivi kweli kila jambo linaangaliwa kwa macho ya siasa.?

Kwani Rais alipofunga shule alikuwa anaokoa watoto wa wapinzani?? Au vifo vya korona ni vya wanapinzani tu? Au wito wa kuchapa kazi ulikuwa ni kwa CCM tu?

Kuna maisha nje ya siasa chafu hizi!!
 
..Jiulize kama amiri jeshi mkuu ataendelea kujificha wakati watoto wa chekechea wamerudi mashuleni na wanapambana na covid19?
 
Tuache siasa kwenye swala la uhai wa watoto wetu, wakiumwa ni sisi wazazi tunaohangaika sio chadema wala ccm, kwa hiyo wakati mwingine sio kila jambo lafaa kusekwa siasa

Hata tulipowazaa na kuwapeleka shuleni pia sio chadema wal ccm waliokuja kuwalipia ada wala kuchangia gharama za malezi au matumizi

Na hata wakifa uchungu n wa mzazi sio wa chadema wala ccm
Wakuu,

kwa hali inavyojidhihiri yenyewe chadema wanaonekana kujali sana swala la afya na hatua mathubuti ya kujikinga na corona

Itakumbukwa mapema mwezi huu wabunge wa chadema waliamua kujitenga na kugomea kushiriki vikao vya bunge kwa tahadhari ya ugonjwa wa corona.. hii ilikuwa right move kiukweli japo bunge na serikali viliendelea na shughuli zao kama kawaida

Najiuliza hapa, corona bado ipo tena ya kiwango cha bombadia na mheshimiwa rais Magufuli ametangaza uwezekano wa kufungua shule na vyuo ilihali hali halisi ya corona bado iko kama kawaida

Je, tutarajie wanaCHADEMA na vyama vya upinzani kuwaongoza na kuzuia watoto wao kurudi shule na vyuoni kwa hofu ya kupata corona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom